Sipendezwi na jinsi inavyolazimishwa sasa CDF kuwa chini ya Waziri wa Ulinzi 'Kiprotokali' wakati Waziri wa Ulinzi ndiyo anapaswa kuwa chini ya CDF

Acha uongo. IGP hampigii saluti CDF.
 
Marekani hawana waziri wa ulinzi, wana secretary General ambae ni Lloyd
Uongo mwingine huu. Marekani wana waziri wa ulinzi. Mawaziri wao hawatumii title ya "minister" bali huitwa "secretary". Ndio maana kuna Secretary of State (waziri wa mambo ya nje), Secretary of Treasury (waziri wa fedha), Secretary of Defence (waziri wa ulinzi) n.k
 
Yani unataka waziri apokee order toka kwa CDF??? hapana waziri lazima awe mkubwa kuliko cdf kiliko IGP. Hii nchi sio ya kijeshii
 
sio jeshi tu inawezekana chanzo cha haya matatizo ie ujinga, maradhi na umasikini inatokana na hii kasumba kuweka siasa mbele ya utaalamu ndio maana mambo mengi tunafeli saana.
 
Wapi uliona MKUU WA MAJESHI ANAKUWA MKUBWA WA WAZIRI WA ULINZI? Hapo USA tu tunaona Waziri wa Ulinzi ndio Top.
Anakuwaje chini ya waziri wa ulinzi hebu tuelekeze wewe unaefahamu itifaki.
 
Buruguja hongera kwa kujiamini saana ila umeenda speed umepitiliza kituo.

CDF.

Ni mkuu wa majesh ya ulinz na ni mkuubwa kwa majeshi yoote.

Ndio maana ukakuta mzee aliweza move na cheo chake toka tpdf hadi magereza, amran kombe alimove na cheo chake toka tpdf hadi tiss na mifano mengine miiiiingi.

But kinachotokea ni ugawanyajw wa madaraka tu... Training ya igp sio sawa na jwtz ndio maana kunakuwa na mipaka...
 
Nimeishia pale uliposema kuwa Afrika ikiwa na viongozi kama Kagame na Museven tungeendelea.

Mimi nakuuliza, hao Kagame na Museven si wapo na ni maraisi?! Nchi zao zimeendelea kuzidi nchi zingine? Au hadi wafikie Madkiteta 50 ndio tuendelee, sio kwamba akina Kaguta na swahiba wake Paulo wangeonyesha kwanza mfano?
 
Hakimu mfawidhi anapigiwa salute na CDF? you are joking.Ngoja vita ije au yatokee machafuko ndio utajua sio sawa mambo mengine ni siasa hazima mashiko waliotutangulia walikosea sana kama ni kweli hiko cheo kinachezewa
Hayo mambo ya kupiga saluti kwa mahakimu na majaji,wanayafanya polisi sijawahi kuona mwanajeshi anapiga saluti kwa jaji au hakimu.
 
Umenena vyema kabisa, japo mi ningependa hata ikiwa Waziri wa ulinzi na usalama atakuwa juu ya CDF kimamlaka basi awe anateuliwa tokea humo humo kwenye Jeshi ili awe anasimamia inshu za Jeshi kimikakati sababu ya kuwa mzoefu wa kazi na kujua namna gani ya kukabiliana na changamoto zote za Askari.
 
Huwa mnapata wapi muda Wenu wa Kupoteza Kuwaelimisha Watu Wapumbavu na Wendawazimu kama huyo?
 
Mzee alimove na Cheo chake Kwa Sababu alitoka JWTZ,
Huku alikohamia hawezi na hakuweza kutambulika kama Mej Gen. Ila alitambulika kama CGP yaani Mkuu wa Jeshi la Magereza ambae Kwa wadhifa wake wa CGP anakuwa level moja na hawa Wakuu wengine (CDF,IGP,CGI na DTISS).
Kumbuka Kwa upande wa JWTZ, waliokuwa au wenye Cheo kama Cha Mzee wapo wengi ambapo Mzee alipokuwa huko JWTZ alikuwa level moja na Wenzie (wanatofautiana Tu seniority) na alivyohamia Magereza, automatic akawa level nyingine kulinganisha na hao aliowaacha JW ambapo Kwa vyovyote vile lazim wamsalute hata kama Hakuwa senior alipokuwa JW.
 
Ushasema trainings ni tofauti,halafu mmoja awe mkubwa kwa mwenzake,how?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…