Sipendezwi na jinsi inavyolazimishwa sasa CDF kuwa chini ya Waziri wa Ulinzi 'Kiprotokali' wakati Waziri wa Ulinzi ndiyo anapaswa kuwa chini ya CDF

Sipendezwi na jinsi inavyolazimishwa sasa CDF kuwa chini ya Waziri wa Ulinzi 'Kiprotokali' wakati Waziri wa Ulinzi ndiyo anapaswa kuwa chini ya CDF

naunga mkono hoja,jeshi letu liheshimiwe !! NI jeshi lenye sifa zilizotukuka Africa yote ,Sasa tusianze kulichukulia poa . Jeshi halifungamani na siasa zaidi lina monitor wanasiasa na siasa zao ,na kulinda mipaka ya nchi na raslimali za nchi!! CDF sawa anateuliwa na rais lkn baada ya uteuzi ,ni mtu mkubwa kuliko ,ameshika hatma ya rais na nchi pia .salute kwa ma generals na soldiers wote,kwa kulilinda taifa letu na kulipa heshima taifa letu ,kimedani!!
 
Niwaambie ukweli aliyeleta hii hali ni baba wa Taifa kwa kuliingiza jeshi kwenye siasa.Wakati ule kulikuwa na kitu kinaitwa mkoa wa majeshi.Yote sababu ilikuwa chama kimoja.
Mimi kwa upande wangu Jeshi ni taasisi ya kipekee kabisa.Ukitaka kulijua hilo kuna mihimili mitatu Bunge,Serikali na Mahakama lakini jeshi halikutajwa katika mhimili wowote hapo hii inaonyesha ni jinsi gani ilivyo taasisi nyeti.
Jeshi japo haijaandikwa kikatiba mihimili yote hii mitatu jeshi likidinda hakuna kinachofanyika na kufanikiwa.

Kwa waziri wa ulinzi sina usemi hapo kwa kweli mi ninachojua tu CDF huwa hampigii salute mtu yeyote bali ni Raisi ambaye ni amiri jeshi mkuu,maiti(marehemu yeyote hata kama ni raia) haya basi na waziri wa ulinzi maana kumteua CDF waziri wa ulinzi anaweza husika.

Lakini kitendo cha CDF kumpigia salute mkuu wa wilaya kisa tu ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya hii sio sawa kabisa ni mambo ya siasa haya hayana mashiko.Ukitaka kujua tulikosea ni kwanini ilifika mahali jeshi likatolewa kwenye siasa? ikaonekana kama ukiamua kubaki na nyadhifa za kisiasa ujitoe jeshini ndio wakatoka kina Kinana,Kikwete,Makamba n.k.Miaka ile unaweza kuta askari flani mkubwa ni mkuu wa mkoa

CDF ni mtu wa kipekee sana na mzito maamuzi yake yanaweza leta mtafaruku raisi mwenyewe anamuheshimu sana.Jeshini hakuna vyama vya wafanyakazi,hakuna ilani wao ni amri tu.Mambo yakiharibika hawa jamaa wanaacha familia zao na wake zao wanakwenda uso kwa uso kwenye mvua za risasi kutupambania sisi tukiwa tume starehe na watoto wetu na wake zetu.Sisi tukiwa tumefunga mkanda kwenye suruali zetu wao mikanda kwao ni ule mkanda wa risasi.Kumbukeni Iddi Amini alivyotuvamia kama sio hawa jamaa leo historia ya nchi hii ingekuwa ni ingine kabisa si ajabu ungesikia bandari ya Tanga ni bandari ya Uganda.

Naomba nirekebishwe kama nimekosea na mimi ni binadamu
Watu ( Members ) walio Werevu ( Intelligent ) kama Wewe hapa JamiiForums mpo Wachache sana. Hongera kwa Ulichokiandika Mkuu.
 
Hakuna Kitendo Kimenishangaza na Kimeniuma kama kuona Juzi CDF na Chief of Staff wake wakienda Kiunyonge na Kiuhuruma kwa Waziri wa Ulinzi Kujitambulisha.

Sijawahi kuona popote pale Waziri wa Ulinzi anakuwa Juu ya Jeshi tena Kiprotokali wakati Jeshi ni Serikali Kificho ya Kimedani na inayojitegemea na ambayo ikiamua muda wowote ule ichukue hatamu ya nchi inaweza na huyo ( huyu ) Waziri wa Ulinzi anakuwa si lolote wala si chochote.

Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Hayati Mkapa na kidogo Mzee Kikwete waliwaheshimu mno CDF's wa Vipindi vyao na walihakikisha hawalazimishi Jeshi kuwa ni sehemu ya Siasa na Utawala wa Kiserikali.

Hayati Rais Dkt. Magufuli alianza kwa mbaali kutaka Kummiliki CDF (japo alikumbana na Ugumu kidogo) kwakuwa CDF Mstaafu Mabeyo anajitambua na ameiva Kimedani (Kijeshi ) pamoja na Protokali zake zote.

Kama kuna Kitu kimenishangaza na naona HATARI fulani mbeleni huko ni kuona Awamu hii ya Rais Samia huyu Waziri wa Ulinzi Bi. Stegormena Tax akipewa Madaraka makubwa juu ya Jeshi na CDF wake kitu ambacho si Kizuri na siyo cha Kiutaratibu kabisa.

Kwa Kawaida ilitakiwa baada ya CDF Kuteuliwa basi Kiitifaki Waziri wa Ulinzi ndiyo alipaswa kwenda kwa CDF ila siyo CDF na Chief of Staff kwenda kwa Waziri wa Ulinzi huku wakiwa na Nyuso za Huruma kana kwamba Wameamrishwa na Mtu wakati Wao ndiyo wana Mandate ya Kuamrisha.

Namalizia kwa Kuwaasa na Kuwaonya enyi Watawala ( Wanasiasa ) kuwa chezeni na Vitu vyote ila msicheze na Taasisi Nyeti kama ya Jeshi na kutaka nao wawe Wanasiasa kama nyie wakati Kiuhalisia wao ni Wanamedani na wako kwa ajili ya Ulinzi na Usalama Uliotukuka wa Taifa letu hili la Tanzania.

Nichukieni, ila yafanyieni Kazi yote!!!
Tatizo hp jamii forums unaweza ukawa una-argue na mtu ambaye hajamaliza hata darasa la saba, Tutafutieni namna ya kuwa na forum zinazoendana na viwango vya elimu na uelewa tunaweza kuchangia vizuri na kuelewana vinginevyo tutaishia kutukanana na wa watu ambao siku ukibahatika kuwaona utajutia ulichokifanya. Huyu mtu hajuia hata muundo wa serikali, hajui maana ya wizara. Hajui kuwa taasisi yoyote nchi hii lazima iwe chini ya wizara fulani na kila wizara bosi wake ni waziri. Sahv ameishia kutukana tu. Hana anachoelewa pengine amelewa.
 
Kuchanganya siasa na jeshi ni kama kuchanganya mafuta na maji, lazima moja itakuwa juu na nyingine chini na siku zote mwanajeshi hawezi kukubali kuwa chini hiyo ni asili (Nature) nenda kokote duniani hata kama atakubali kujifanya chini ni ile ya kinafiki, unapoapa jeshini wewe unakuwa jamii nyingine ndio maana wanatengwa, siasa isipokuwa na mipaka inaleta muingiliano wa majukumu na kufundishana kazi ambazo sio utaratibu ndiposa mara nyingi jeshi linaamua kuasi.
Nawasilisha
 
Hakuna Kitendo Kimenishangaza na Kimeniuma kama kuona Juzi CDF na Chief of Staff wake wakienda Kiunyonge na Kiuhuruma kwa Waziri wa Ulinzi Kujitambulisha.

Sijawahi kuona popote pale Waziri wa Ulinzi anakuwa Juu ya Jeshi tena Kiprotokali wakati Jeshi ni Serikali Kificho ya Kimedani na inayojitegemea na ambayo ikiamua muda wowote ule ichukue hatamu ya nchi inaweza na huyo ( huyu ) Waziri wa Ulinzi anakuwa si lolote wala si chochote.

Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Hayati Mkapa na kidogo Mzee Kikwete waliwaheshimu mno CDF's wa Vipindi vyao na walihakikisha hawalazimishi Jeshi kuwa ni sehemu ya Siasa na Utawala wa Kiserikali.

Hayati Rais Dkt. Magufuli alianza kwa mbaali kutaka Kummiliki CDF (japo alikumbana na Ugumu kidogo) kwakuwa CDF Mstaafu Mabeyo anajitambua na ameiva Kimedani (Kijeshi ) pamoja na Protokali zake zote.

Kama kuna Kitu kimenishangaza na naona HATARI fulani mbeleni huko ni kuona Awamu hii ya Rais Samia huyu Waziri wa Ulinzi Bi. Stegormena Tax akipewa Madaraka makubwa juu ya Jeshi na CDF wake kitu ambacho si Kizuri na siyo cha Kiutaratibu kabisa.

Kwa Kawaida ilitakiwa baada ya CDF Kuteuliwa basi Kiitifaki Waziri wa Ulinzi ndiyo alipaswa kwenda kwa CDF ila siyo CDF na Chief of Staff kwenda kwa Waziri wa Ulinzi huku wakiwa na Nyuso za Huruma kana kwamba Wameamrishwa na Mtu wakati Wao ndiyo wana Mandate ya Kuamrisha.

Namalizia kwa Kuwaasa na Kuwaonya enyi Watawala ( Wanasiasa ) kuwa chezeni na Vitu vyote ila msicheze na Taasisi Nyeti kama ya Jeshi na kutaka nao wawe Wanasiasa kama nyie wakati Kiuhalisia wao ni Wanamedani na wako kwa ajili ya Ulinzi na Usalama Uliotukuka wa Taifa letu hili la Tanzania.

Nichukieni, ila yafanyieni Kazi yote!!!
Genta hivi unajua kuwa waziri wa ulinzi akifa anapigiwa mizinga 17? au umejisahaulisha! halafu unajisahaulisha kuwa hili ni jeshi la wananchi! wananchi ndio wanamchagua Rais ambaye anakuwa ndio Amiri jeshi mkuu!?
pia nafkiri huelewi vizuri majukumu ya mawaziri wewe
 
anajizima data.

waziri ni msimamizi wa sera wa wizara.
utakuwa ni upunguani kumzidi protocal mtu anayepigania maslahi yako.
waziri wa ulinzi ni incharge wa CDF ila sio boss wa CDF,anachanganya huyu.

CDF ana wakubwa wake kiutendaji wizarani,ana katibu mkuu wizara ana waziri wake pia,hao watu huwapelekea mipango na maombi yake ya matumizi mwaka mzima.
 
Hakuna Kitendo Kimenishangaza na Kimeniuma kama kuona Juzi CDF na Chief of Staff wake wakienda Kiunyonge na Kiuhuruma kwa Waziri wa Ulinzi Kujitambulisha.

Sijawahi kuona popote pale Waziri wa Ulinzi anakuwa Juu ya Jeshi tena Kiprotokali wakati Jeshi ni Serikali Kificho ya Kimedani na inayojitegemea na ambayo ikiamua muda wowote ule ichukue hatamu ya nchi inaweza na huyo ( huyu ) Waziri wa Ulinzi anakuwa si lolote wala si chochote.

Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Hayati Mkapa na kidogo Mzee Kikwete waliwaheshimu mno CDF's wa Vipindi vyao na walihakikisha hawalazimishi Jeshi kuwa ni sehemu ya Siasa na Utawala wa Kiserikali.

Hayati Rais Dkt. Magufuli alianza kwa mbaali kutaka Kummiliki CDF (japo alikumbana na Ugumu kidogo) kwakuwa CDF Mstaafu Mabeyo anajitambua na ameiva Kimedani (Kijeshi ) pamoja na Protokali zake zote.

Kama kuna Kitu kimenishangaza na naona HATARI fulani mbeleni huko ni kuona Awamu hii ya Rais Samia huyu Waziri wa Ulinzi Bi. Stegormena Tax akipewa Madaraka makubwa juu ya Jeshi na CDF wake kitu ambacho si Kizuri na siyo cha Kiutaratibu kabisa.

Kwa Kawaida ilitakiwa baada ya CDF Kuteuliwa basi Kiitifaki Waziri wa Ulinzi ndiyo alipaswa kwenda kwa CDF ila siyo CDF na Chief of Staff kwenda kwa Waziri wa Ulinzi huku wakiwa na Nyuso za Huruma kana kwamba Wameamrishwa na Mtu wakati Wao ndiyo wana Mandate ya Kuamrisha.

Namalizia kwa Kuwaasa na Kuwaonya enyi Watawala ( Wanasiasa ) kuwa chezeni na Vitu vyote ila msicheze na Taasisi Nyeti kama ya Jeshi na kutaka nao wawe Wanasiasa kama nyie wakati Kiuhalisia wao ni Wanamedani na wako kwa ajili ya Ulinzi na Usalama Uliotukuka wa Taifa letu hili la Tanzania.

Nichukieni, ila yafanyieni Kazi yote!!!
Mkuu you are dead WRONG!
CDF siku zote yupo chini ya Waziri wake wa Ulinzi kiserikali.
Hii ni licha ha ukweli kwamba Waziri wa Ulinzi hana mamlaka wala madaraka ya kumuingilia CDF na jeshi kwa ujumla.
Waziri wa Ulinzi ni kama muwakilishi wa jeshi kiserikali ila hawezi kuliamrisha jeshi kwa aina yoyote.
Kiutendaji CDF yupo chini ya Commander in Chief moja kwa moja.

Waziri Maokola Majogo alijaribu kuliamrisha jeshi wakati fulani, cha moto alikipata, na akaondolewa unceremoniously uwaziri.
 
Hii taasisi ya Jeshi ni ya kipekee inayotakiwa kuheshimiwa.
Jeshini kuna kila taaluma iliyoko uraiani kasoro taaluma ya Magereza japo wana jela zao. wana mahakama zao zinaitwa court martial kule hakimu ni mkuu wa kikosi na hakuna kujitetea wala wakili

Jeshini wapo ma prof na ma dr wa phD.Ukitaka kujua jeshini kuna kila taaluma kuna siku ma dr Muhimbili waligoma wanajeshi wakaenda kuchukua hatamu kusaidia maisha ya watu.Kuna siku waongoza ndege waligoma wataalamu wa jeshi wakaenda uwanjani kukamata hatamu.
Jeshini kuna madaktari wa kutibu,wahasibu,walimu,ma injinia wa umeme,majengo mechanical,chemical nk wataalamu wa IT.Iddi Amini alivobomoa daraja la Kagera ma injinia wa Jeshi walijenga la muda kwa mda wa chini ya wiki moja kazi ikaendelea ingekuwa ma injia wa uraiani wa 10% lingechukua muda mrefu na Iddi Amini angeikalia Kagera vizuri zaidi.
Nchi ya Marekani na Urusi pia mambo makubwa ya kiutafiti yanafanywa na wanajeshi.Hata waliokuwa wanakwenda anga za mbali hadi mwezini walikuwa wanajeshi kina Neil Armstrong huyu alikuwa ni profesa na mwanajeshi na alikuwa ndio mission commander ya kwenda mwezini.

Nimeona niongezee haya kuonyesha msisitizo taasisi hii ilivyo muhimu sio taasisi ya kuchukuliwa ki spot spot kwa waziri ulinzi kupigiwa salute hapo sina objection ninachokataa mkuu wa wilaya eti CDF anampigia salute kisa tu eti ni mkuu wa ulinzi na usalama kwenye wilaya yake wakati CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa nchi nzima kwa maana changa vikorokoro vingine polisi,magereza,uhamiani, vyote yeye ndio mkuu.
Hili halijakaa sawa mkuu wa wilaya kupigiwa salute na CDF
 
Hii taasisi ya Jeshi ni ya kipekee inayotakiwa kuheshimiwa.
Jeshini kuna kila taaluma iliyoko uraiani kasoro taaluma ya Magereza japo wana jela zao. wana mahakama zao zinaitwa coarat martial kule hakimu ni mkuu wa kikosi na hakuna kujitetea wala wakili

Jeshinia wapo ma prof na ma dr wa phD.Ukitaka kujua jeshini kuna kila taalama kuna siku ma dr Muhimbili waligoma wanajeshi wakaenda kuchukua hatamu kusaidia maisha ya watu.Kuna siku waoongoza ndege waligoma wataalamu wa jeshi wakaenda uwanjana kukamata hatamu.
Jeshini kuna madaktari wa kutibu,wahasibu,walimu,ma injinia uwa umeme,majengo mechanical,chemicla nk wataalamu wa IT.Iddi Amini alivobomoa daraja la Kagera ma injinia wa Jeshi walijenga la muda kwa mda wa chini ya wiki moja kazi ikaendelea ingekuwa ma injia wa uraiani wa 10% lingechukua muda mrefu na Iddi Amini angeikalia Kagera vizuri zaidi.
Nchi ya Marekani na Urusi pia mambo makubwa ya kiutafiti yanafanywa na wanajeshi.Hata waliokuwa wanakwenda anga za mbali hadi mwezini walikuwa na wanajeshi kila Neil Armstrong huyu alikuwa ni profesa na mwanajeshi na alikuwa ndio mission commander ya kwenda mwezini.

Nimeona niongezee haya kuonyesha msisitizo taasisi hii ilivyo muhima sio taasisi ya kuchukuliwa ki spot spot kwa waziri ulinzi kupigiwa salute hapo sina objection ninachokataa mkuu wa wilaya eti CDF anampigia salute kisa tu eti ni mkuu wa ulinzi na usalama kwenye wilaya yake wakati CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa maana changa vikorokoro vingine polisi,magereza,uhamiani, vyote yaya ndio mkuu.
Hili halijakaa sawa mkuu wa wilaya kupigiwa salute na CDF
Safi Mkuu, ila ni Court Martial!
 
Nadhani siyo kwamba hauelewi itifaki za serikali zinavyofanya kazi.

Umeandika kwa malengo yako maalumu unayoyajua mwenyewe.

Tangu lini Cdf kiitifaki akawa juu ya Waziri wa ulinzi?

Si Waziri wa ulinzi tu pekee ambaye yupo juu ya Cdf kiitifaki, ni kwa waziri yeyote.

CDF awe chini ya Waziri aliyetokea wapi mkuu.?

Ni heshima TU lakini sio kiuhalisia na haitakuja kuwa hivyo. CDF ni habari nyingine kabisa. Achana na hicho cheo mkuu. Mawaziri wapo kwenye level ya mabrigadier General hata stahiki zao zinaendana lakini sio General.

Uzuri tunao magenerala wastaafu wengi TU angalia heshima walizotununukiwa kimataifa na kitaifa.

Waziri si Mbunge TU.
Waziri anaweza akapigwa hata vibao na Polisi unasema Nini wewe mkuu.
Kama unabisha kamuulize Aliyekua Waziri wa Sanaa ,utamaduni na Michezo. Alishikiwa bastola akaufyata. CDF ukimshikia bastola unachapwa risasi on the sport na hakuna hata kesi itakayofunguliwa popote itakua kama mbu TU amepukuziwa rungu. Mambo mengine tuyaache mkuu.
Achana kabisa na habari ya mkuu wa majeshi. 4 Star General ni habari nyingine kabisa. Ile ni serikali Mbadala muda wote na ipo standby kushika nchi muda wote. Ukiona nchi Ina Jeshi la hovyo hovyo ambalo halijajianda kuilinda katiba Muda wote ujue hiyo ni nchi ya manyani wanayoishi mwituni. Utulivu wa nchi ni pale Jeshi linapokuwa na raia mmoja TU anayetia amri Kwa CDF na sio wanasiasa wengine. Rais wa awamu ya Tano JPM alipoapishwa aliendesha nchi vizuri sana bila wabunge wanaoitwa Mawaziri alikaa karibu Mwezi mzima. Haiwezi kutokea nchi kuendeshwa bila mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama hata Kwa dakika Moja. Anaweza kukosekana Waziri wa Ulinzi bila athari yoyote.
Nchi sio Mawaziri mkuu ,Nchi ni Jeshi mkuu. Ni amiri Jeshi peke yake mwenye mamlaka juu ya CDF . Peke yake , yaani Rais peke yake ,unajua maana ya peke yake.? Ndio hivyo mkuu. Hizo zingine ni stori za vijiweni.
 
Mkuu you are dead WRONG!
CDF siku zote yupo chini ya Waziri wake wa Ulinzi kiserikali.
Hii ni licha ha ukweli kwamba Waziri wa Ulinzi hana mamlaka wala madaraka ya kumuingilia CDF na jeshi kwa ujumla.
Waziri wa Ulinzi ni kama muwakilishi wa jeshi kiserikali ila hawezi kuliamrisha jeshi kwa aina yoyote.
Kiutendaji CDF yupo chini ya Commander in Chief moja kwa moja.

Waziri Maokola Majogo alijaribu kuliamrisha jeshi wakati fulani, cha moto alikipata, na akaondolewa unceremoniously uwaziri.
Vijana msome katiba, mtu pekee ambae yupo juu ya CDF ni raisi wa nchi ambae ndie amiri jeshi mkuu
 
Uwe na Iq ndogo au kubwa jukumu lako raia ni kutii sheria bila shuruti na hutapata matatizo mpaka unazikwa. Mengine yote ni mbwembwe tu.
 
Maelezo mengi ila..Umepuyanga.
 
Vijana msome katiba, mtu pekee ambae yupo juu ya CDF ni raisi wa nchi ambae ndie amiri jeshi mkuu
Soma tena post yangu uilewe na si kukariri .
Halafu rudi ukaisome tena katiba uniambie mahali na lini CDF anaingia kwenye Cabinet.
 
Duniani Kote nchi ni ya Jeshi . Nchi yenye Jeshi Kubwa ndiyo nchi imara. Tanzania hatuoni umuhimu wa majeshi yetu Kwa sababu Mwalimu alikua msomi Halisi wa siasa na jamii na Dunia aliijua vizuri Kwa alikua ni Msomi aliyeelimika Kwa kiwango kikubwa sana. Nyerere hakuwa mjinga alipokua analitumia Jeshi lake kwenye vita za Ukombozi na kusaidia nchi nyingine. Aliwaweka Wanajeshi Bize na mambo ya nje na kuwasaidia majirani. Na hicho ndicho wanachofanya Marekana ni nchi za NATO. Nchi za Kiraia zinapaswa kulitumia Jeshi Kwa umakini mkubwa. Huwezi ukasikia Rais wa Marekani anawakoromea wanajeshi Kwa lugha za kudhalilisha. Hata Kagame analiheshimu sana Jeshi lake ikiwemo Jeshi la Polisi. Huku Afrika na hata Tanzania ni rahisi kusikia Rais au mwanasiasa analidhalilisha Jeshi au Polisi wakati huo huo anategemea kuiba kura Kwa sababu Majeshi yatamlinda. Yani ni Hopeless kabisa.

Jeshi ni serikali Mbadala ndio maana imepewa jukumu la kulinda Katiba Muda wote. Kuna maana kubwa uliyojificha nyuma ya Jukumu Hilo . Wanasiasa UCHWARA HAWAWEZI KUELEWA MAANA YAKE. IPO SIKU AMBAYO HAIPO MBALI WATAJUA MAANA YAKE. Historia Duniani Kote hua inatabia ya kuwapitisha wanadamu kwenye nyakati zinazofanana endapo hawatajifunza Kwa waliowatangulia katika nyakati zinazofanana.
Afrika maendeleo ya pamoja yatatokea Kwa mapinduzi na sio Kwa kugonga meza. Afrika ikiwa na Marais 5O kama Kagame na Museveni na Museveni Hakika Kwa utajiri uliopo tungekua tunauza mtungi wa Gesi KG 15 Kwa sh. 20000 na mafuta Petroli Sh. 1200/- kwa Ltr.

Kutoliheshimu Jeshi na kulipa heshima yake inatokana na matatizo ya nchi jirani.Hali inayopelekea wanajeshi wetu angalau kupata sehemu wanapoweza kwenda kuweka roho zao rehani ili wapate anagalu fedha za kuboresha maisha yao na hivyo kutulia na kuwaachia wanasiasa wa ndani ya nchi zao wakilamba asali na kuwakejeli wanajeshi wao . Hiyo ipo pia Kwa majeshi ya Polisi Afrika wanaachwa kama Kuku wa Kienyeji waishi Kwa rushwa na kubambikia watu Kesi ili waweze kuendesha maisha yao na kusomesha watoto wao ili watoto wao wasije wakarithi matusi na kejeli Toka Kwa wanasiasa kuwa hawajasoma ,hawana uwezo wa kuchanganua mambo ,hawajui kupeleleza, ni wababaishaji,wasumbufu, hawajui Sheria n.k lakini ndio wanaowatumia kuiba kura na kuchafua Hali ya utulivu kisiasa na wakishaingia madarakani wanawakejeli na kuwaona hawana maana yoyote na hawastahili kulipwa mishahara ya kuwafanya waendeshe maisha yao Kwa misingi ya Haki na uadilifu . Matokeo yake ni kuwa na mifumo isiyoeleweka na yenye mikanganyiko mikubwa. CDF ni International Rank na vyeo vingine vyote vya Kijeshi chini yake. Hawatakiwi kuwa watumwa wa kisiasa . Wanapaswa kuwa huru mbali na siasa. Raia mmoja TU ndiye mwenye kauli juu ya Jeshi ,yaani Rais basi mana ana mamlaka ya kumteua CDF na Kumtengua muda wowote. Wengine wote hawana jambo lolote la kiutendaji juu ya Jeshi na hivyo hawana maelekezo yoyote Kwa Jeshi zaidi ya blabla za sijui ilani sijui Nini wakati Jeshi na ilani ni vitu visivyoendania Kwani Jeshi linapaswa kulinda Mipaka ya nchi na Katiba ya nchi hata kama hakuna Rais Wala Chama. Yaani hata ikatokea Serikali yote wakaangamia Kwa baridi Kali au Upepo mkali wa kisulisuki Ukalizoa Jengo la Bunge la Kameruni Bado Jeshi litalinda mipaka ya nchi na Katiba mpaka Hali itakapokaa sawa. Hivyo nakubaliana na wewe kabisa kuwa Jeshi linahitaji kuheshimiwa na kuepuka jambo lolote linaloweza kuwafanya wanasiasa kujiweka juu ya Taratibu za Kijeshi Kwa namna yoyote ndani ya nchi zetu za Afrika.

Ni bahati TU Afrika Kuna nchi zenye Vita kama Kongo ,Sudani,Somalia ,Msumbuji, Burundi n.k. Hali inayowapa fursa baadhi ya wanajeshi wa nchi nyingine kufadhiliwa na Mabeberu wa nchi za magaharibi Kwa kulipwa fedha ili wakalinde kile wanachokiita amani. Hapo wanaopata fursa hiyo wanajipatia nafasi ya kuboresha maisha yao na kuvumilia manyanayaso ya wanasiasa waliojaa dharau na kejeli Kwa kushiba asali na kujiona wao wanajua kila kitu mpaka Medani za kivita Kwa sababu TU ya kuangalia Move za Kina Rambo wanadhani kuwa kumbe inawezekana mtu mmoja akalinda mipaka ya nchi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Nakuunga mkono hata kama hawatakuelewa lakini Iko siku watakuelewa. Siku Sudani na Kongo wakipata amani akili zitakaa sawa Kwa wanasiasa wa nchi za Kiafrika ,Watajua kuwa hakuna Serikali bila majeshi,hakuna heshima ya mahakama bila Majeshi ,hakuna heshima ya Bunge bila Majeshi. Hakuna amani bila Majeshi. Hakuna kula Bata na starehe bila Majeshi. Watu wamwagilia mioyo yao Kwa sababu Kuna majeshi yanayolinda usalama wa nchi.
Hapa nadhani maoni mengi ni ya Hisia.

Uko utawala wa Kijeshi-Dunia haitamani Serikali iwe na utawala wa Kijeshi..isipokuwa tu pale ambapo kuna mazingira yasiyokuwa na Amani.

Serikali ya Wananchi ni Serikali inayowapa Raia kujitawala kadiri wanavyoona inafaa.

Jeshi ni Nguvu ya Serikali.

Nguvu ni Nguvu siyo lazima ukunje misuli.

Nguvu hutumika wakati inahitajika.

Wakati mwingi wa utawala wa serikal ya wananchi ni utawala bila Nguvu.

Kwa hivo Nguvu iko kutizama ni wapi inahitajika...lakini kama haihitajiki basi maisha ya kiraia yanapendeza kuendeshwa kuraia.

Serikali ya Kiraia inakuwa na Katiba...

Hiyo katiba ndiyo hulindwa na Vyombo vyenye Nguvu!

Wanaotekeleza katiba ni wawakilishi wa wananchi waliounda Serikali yao kulingana na katiba waliyoikubali.

Waziri wa ulinzi ndiye kiungo kikubwa cha Serikali ya wananchi na Vyombo.

Serikali ndiyo yenye uwezo wa kusababisha mapato...

Mapato yanatokana na wananchi
..

Mwisho wa saa wananchi ndiyo wenye Jeshi lao...

Vyombo vipo chini ya Serikali yao iliyoundwa kutokana na wananchi.

Hata mwili una jeshi...

Lakini kinachoongoza mwili siyo jeshi...

Jeshi lina tii Serikali!
 
Safari umechemsha kwa busara zako. Hujui kabisa itifaki. Waziri ni mwakilishi wa kisiasa wa taasisi hiyo. Na siasa ndio inatawala nchi.
 
Back
Top Bottom