Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Uzi huu unaonyesha jinsi Watanzania walivyokata tamaa. Yaani hakuna mtu mwenye ambition. Wote ni magoigoi tu. Chochote sawa tu. CCM itaendelea kuiba chaguzi inavyopenda, na sisi tutaendelea kulala tu kwa attitude za aina hii!

Majumba saba - kupanga ni kuchagua. Kila kitu kinawezekana. Nimefurahi kusikia kuwa una mpango wa kutoa kilicho cha Mungu katika mapato yako. Mungu atakubariki. Thamani yako unaijua wewe. Lakh 2.5 kwa mwezi ni nauli ya kwenda kazini na kurudi nyumbani tu hakuna kitu kitabaki.
 
Mkuu kuliko zile pisi ambazo wako vitengo vya sales kwenye makampuni makubwa mfano tigo, airtel, cocacola wanaotembeza vipeperushi africana, tangibovu, mwenge, makumbusho

Kuliko zile pisi ambazo zinapiga graduate trainee program crdb, nmb, tib tena hawa ndio wako smart nama gpa makubwa kutoka udbs ifm +cpa na wanapata tu posho, tena crdb unapiga kwa miezi 36 ukimaliza ndio wakufikirie ajira

Kuliko wale shombe shombe ambao wako kkoo wanaokaribisha wateja kwenye maduka naelimu zao wameweka pembeni

Bora hata ingekuwa kozi ya maana, hiyo ambayo anaweza kuwa replaced na malaki ya wahitimu huku mtaani asilimia 90 ya vyuo vyote wanatoa Bcom

Yaani sijui wale jamaa wa ifm, cbe,tia ,udbs ,institute of accountancy government huwa inawapeleka wapi[emoji22][emoji22] bora hata wanaosoma ba education
 
Ulikuwa hujui mishahara ya nchi hii?
 
we bwege unayejiita msomi huku huna uzoefu wa kazi hata miezi 6 endelea kujijaza upepo hapo kwenu hujui unachokifanya
 
Haya bhana, Nadhani utapata utachostahili!
 
Mwanza mjini Kuna mdada mmoja wa kichaga Ana masters in banking and finance alisoma nje ya nchi ( USA) alitafuta ajira Hadi Sasa anauza makande maofisini nakutafuta video yake soon nakupeni Ila wewe subilia huo mshahara na one degree yako
 
Labda uajiriwe kwenye kampuni ya baba yako ndio utapata iyo 1m subiri jiwe la mtaa likupige akili itakukaa sawa.
 
Mwanza mjini Kuna mdada mmoja wa kichaga Ana masters in banking and finance alisoma nje ya nchi ( USA) alitafuta ajira Hadi Sasa anauza makande maofisini nakutafuta video yake soon nakupeni Ila wewe subilia huo mshahara na one degree yako

Kaz kaz mzee.
 
Kama uwez siukae kimya? Sasa unakuja huku kutafuta nn fala ww? Unajifanya msooomi! Wewe umepata kazi unachezea mbwa ww? Watu wanalipwa 100000 kwa mwez wanaendesha maisha yao ww unajifanya mjuaji?
Alafu nahisi unatudanganya huna lolote.
 
Huyu jamaa yaani nahisi kwa haraka aliyo nayo atashikishwa rushwa kazini mapema Sana ama anaweza chonga dili na majambazi wakavamia eneo lake la kazi so wa kuajiliwa huyu
 
Ndugu, Bora ningepata hio laki nane, fursa nyingi napata microfinance, na wanataka niwe tayari kuanza na shilingi laki tatu na nusu. Sasa nawaza, maisha ndio yatakuaje? Hio Nile, nipange, niende saloon, nitoe sadaka kha
Wakati huo kuna watanzania wanalipwa 5k a day na wanaendesha familia zao wewe unawaza kwenda saloon tu ?
 
Tumia title ya Afisa Mwandamizi wa Usalama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…