Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?

  • Total voters
    710
Kaka hivi moudytunechi anaweza kutuambia kwa nini rainbow inakuwa na shape ya sphere? Na sio line moja tu kama inavyokuwa kwa zile ndege zinazosafiri umbali mrefu?
Kwanini anga ina umbo kama la duara?

Je anga nalo ni duara?

Hao hao wataalam unaowasikiliza wanasema kuwa unaona duara ya anga kama duara kutokana na macho yako tu lakini haipo hivyo.Lakini linapokuja suala la kuona mbali na kuibuka kwa meli wanasema ni kwasababu ya duara tufe ya dunia,ajabu kabisa hii.....
 
Mi kinachoniumiza kichwa ni hili la dunia kujizunguusha yenyewe kwenye muhimili wake "ROTATION" kwamba hiyo gravitation force ni hadi kwenye atmosphere? coz Kwa mfano ikitokea something labda ndege kikaganda hewani kwa maana ya atmosphere kwa masaa kadhaa kikitua chini c kitajikuta kipo America!!
Wanasema kuwa dunia inazunguka na atmosphere yake hivyo kama ndege ikiganda itajikuta iko pale pale kwasababu nayo itakuwa inazungushwa na dunia kwasababu iko ndani ya atmosphere.....

Lakini hii bado ni dhana tu kwakuwa hakuna ushahidi wowote wa kueleweka wa dhana hii.....
 
Mada yako ipo kisayansi zaidi nami Naomba nikuulize kisayansi zaidi
Kama dunia iko flat na haizunguki inakuwaje jua likizamia magharibi lisichomozee huko huko badala yake linachomozea mashariki na kuzama magharibi,na mwezi je si ungekuwa ukionekana marekani Leo kuja kuonekana huku ni baada ya siku za kutosha?
Soma thread ina majibu ya kijiswali chako hiki acha uvivu....
 
Sio jibu sahihi hata kidogo. Hata ukiwa na darubini kali ukiwa dar zenji huioni na hayo mabonde na milima huioni. Imewahi enda bichi hapa dar na kuiona boat toka zenji inavyotokea ikiwa inatoka zanzibar?? Inatokea kwa chini kama inaibuka. Zenji iko kwa "chini"!
Yaani unashindwa tu kujua kuwa hicho kifaa kina limitation ya uwezo wa kuona mbali?

Je hicho kifaa unachotumia kina uwezo wa kuona umbali upi?

Unataka kutumia kifaa cha kuonea umbali wa maili 2 uone umbali wa maili 10 itawezekanaje?

Hata jambo dogo kama hili umeshindwa kujielewa?
 
Wanasema kuwa dunia inazunguka na atmosphere yake hivyo kama ndege ikiganda itajikuta iko pale pale kwasababu nayo itakuwa inazungushwa na dunia kwasababu iko ndani ya atmosphere.....

Lakini hii bado ni dhana tu kwakuwa hakuna ushahidi wowote wa kueleweka wa dhana hii.....
Mi naona hawa wasomi wanatuzingua tu kwa sababu hata huo muhimili ulioshikilia dunia hata cjui unapatikana maeneo gani ya Dunia hii
 
Mi naona hawa wasomi wanatuzingua tu kwa sababu hata huo muhimili ulioshikilia dunia hata cjui unapatikana maeneo gani ya Dunia hii
Mhimili ni neno tu linalowakilisha nguvu ya mvutano ambayo haionekani......

Nadhani hii siyo hoja nzuri kabisa.....
 
Mi naona hawa wasomi wanatuzingua tu kwa sababu hata huo muhimili ulioshikilia dunia hata cjui unapatikana maeneo gani ya Dunia hii
Hizi ni akili mbaya sana kwa maendeleo ya taifa, hivi unategemea kuwa kuna "physical axis" imeshikilia dunia??
 
image.jpeg
Tatizo lako linaakisi matatizo ya watu wengi sana.......

Unaposoma maandiko halafu ukashindwa kuyaelewa unayatupia maandiko hayo lawama badala ya kuchunguza kama wewe ndiyo hujaelewa na maandiko hayo hayana tatizo kabisa.Ni sawa na wewe uwe umesimama barabarani na jamaa zako wanne ambao wanakuambia kuna gari la rangi ya bluu linapita barabarani na wewe unaendelea kukodoa na hulioni gari hilo,badala ya kufikiria tu kuwa inawezekana macho yako yana matatizo hivyo yanakufanya usilione gari hilo,wewe unakimbilia kusema jamaa zako ni waongo na gari hilo halipo.....

Nimezungumzia dunia flat ya CD,haiwezekani uwe na flat ya namna hiyo halafu kuwe na upande wa pili wa duara.Tatizo nililoliona hapa ni wewe kushindwa kusoma maandiko mengi na kuyaelewa.Kwenye maandiko yangu hapo juu nimezungumzia dunaia duara ya tufe kwa namna tofauti na dunia duara ya CD kwa namna tofauti,nikatoa na mifano. Nadhani mfano wa chungwa ndiyo umekuchanganya kabisa maana niliutoa nikionesha tofauti kati ya duara ya CD na duara ya tufe [chungwa] na uwezekano wa kuuona mti.....

Suala la upande wa pili lilikuwa kwenye duara ya chungwa na siyo duara ya CD.Nilisema mti uliosimikwa kwenye chungwa huwezi kuuona kwenye duara ya chuingwa unapokuwa upande mwingine wa duara ile hata ukitumia chomb cha kuonea mbali lakini, kwenye duara ya CD ambapo hakuna upande wa pili,ukisimika mti kisha ukaenda umbali wa kilomita 10 hutaweza kuuona mti huo pia lakini,ukitumia kifaa cha kuonea mbali unauona.....

Sasa kwa kutumia logic hiyo,meli inapokuwa haionekani kwenye macho yako baada ya kwenda mbali,wale ambao wanasema dunia ni duara ya tufe hudai kuwa unakuwa huioni kwasababu inakuwa imeshapotelea kwenye duara ya dunia hivyo inakuwa kwenye upande mwingine wa duara hiyo.Lakini ukichukua kifaa cha kuonea mbali unaiona meli hiyo.Swali la msingi,je kwanini uione wakati iko kwenye upande mwingine wa duara ya dunia?

Kama dunia ni duara ya tufe usingeweza kuiona meli hiyo na ungeishia kuona maji tu pale yalipopinda lakini ni kinyume chake,meli inaonekana bado na hii inathibitisha kuwa dunia ni flat lakini duara kama CD.Kama vile mti ukiusimika kwenye barabara ya urefu wa kilomota 10,halafu mti ule ukausimika mwanzo wa barabara ile kisha ukaenda umbali huo wa kilomita 10 ukatazama hutaweza kuuona mti ule,hii haimaanishi dunia imepinda kutokana na duara yake kama tufe bali huuoni kwasababu macho yako hayana tu uwezo wa kuona umbali huo.Ukichukua kifaa cha kuonea mbali utauona huo mti bila matatizo yoyote,hii inaonesha kuwa dunia haijapinda bali ni flat.....

Nadhani umenielewa....

Nimeelewa maandiko yako lakini sikubaliani nayo.

Yaani unashindwa tu kujua kuwa hicho kifaa kina limitation ya uwezo wa kuona mbali?

Je hicho kifaa unachotumia kina uwezo wa kuona umbali upi?

Unataka kutumia kifaa cha kuonea umbali wa maili 2 uone umbali wa maili 10 itawezekanaje?

Hata jambo dogo kama hili umeshindwa kujielewa?

Duh, "kaka" sijui upeo wako wa uelewa, ila naona ngoja niachie hapa.
You are defying science with some irrelevant, unproven evidences that the planet earth is not spherical.
Suala la dunia ni duara ya cd kama unavyodai ndivyo nilivyo kuelewa (kama picha ya mleta uzi juu hapa nimeambatanisha) na bado sikubaliani nalo. Hapo ni wewe ndie umeshindwa kunielewa!! Suala la darubini ndio maana nimesema hata darubini kali bado zenji hautaoona, aliyekwambia mwisho wa uwezo wa darubini ni maili 2 ni nani?? wewe kusema kuwa kwa naked eyes zenji huioni ila wanasema kwa darubini unaiona, ni nani kasema hivyo au unaongeza ukubwa wa goli ufunge kiurahisi??
Common sense pia itumike mkuu!
You are playing devil's advocate to spice up the topic but the truth is very obvious, just common sense!
The earth flat society hata upatikanaji wa usiku na mchana haujajitosheleza!!
 
Kwa hyo hilo bara la Antractica limezunguuka dunia nzima.. Maana kama ni duara ukingo hauwezi kuwa sehem moja ya dunia!
Nasema hivyo kwa ajili ya route ya australia na bara la south america... north pole likewise ni hivyohivyo
 
View attachment 429652

Nimeelewa maandiko yako lakini sikubaliani nayo.
Sawa......

Kutokubaliana na maandiko yangu ni haki yako ya msingi,hapa hatuangalii unakubali au haukubali isipokuwa ni kwanini hukubaliani na hayo maandiko yangu.....
Duh, "kaka" sijui upeo wako wa uelewa, ila naona ngoja niachie hapa.
You are defying science with some irrelevant, unproven evidences that the planet earth is not spherical.
Hakuna mahali popote nilipoielezea sayansi kwenye maelezo yangu isipokuwa nimeelezea hali halisi,hali halisi inaweza kuwa ni sayansi kwa sehemu tu na inaweza ikawa siyo sayansi kwa sehemu kubwa.Makosa yako ni kuanza kufikiri namna hii.....
Suala la dunia ni duara ya cd kama unavyodai ndivyo nilivyo kuelewa (kama picha ya mleta uzi juu hapa nimeambatanisha) na bado sikubaliani nalo. Hapo ni wewe ndie umeshindwa kunielewa!! Suala la darubini ndio maana nimesema hata darubini kali bado zenji hautaoona, aliyekwambia mwisho wa uwezo wa darubini ni maili 2 ni nani??
Unasoma maandiko yangu huku unaongozwa na mihemko,nitakueleza ni kwanini nakuambia hivyo....

Hakuna mahali nimesema kuwa mwisho wa darubini ni maili 2 isipokuwa nimekuambia kuwa huwezi kutumia darubini yenye uwezo mdogo kutaka kuona sehemu inayohitaji darubini yenye uwezo mkubwa na nikatoa mfano wa umbali wa maili 2.Wewe umesema "hata ukitumia darubini 'kali' kiasi gani huwezi kuona",hivi Zenji kuna umbali upi? unajua darubini ya uwezo wa juu zaidi iliyoko duniani ni ya uwezo upi?

Ushawahi kuitumia?

Unahemkwa hadi unashindwa kuzingatia vitu vidogo kama hivi kwenye maandiko yako....
wewe kusema kuwa kwa naked eyes zenji huioni ila wanasema kwa darubini unaiona, ni nani kasema hivyo au unaongeza ukubwa wa goli ufunge kiurahisi??
Common sense pia itumike mkuu!
Kwa logic ya kuiona meli ambayo huioni kwa macho yako inashindikana nini kuiona Zenji?
You are playing devil's advocate to spice up the topic but the truth is very obvious, just common sense!
Usijali,soon utajua ni nani kati yangu mimi na wewe anayeifanya kazi ya Shetani,nadhani hata Shetani humjui wewe.....
The earth flat society hata upatikanaji wa usiku na mchana haujajitosheleza!!
Kivipi?
 
Sawa......

Kutokubaliana na maandiko yangu ni haki yako ya msingi,hapa hatuangalii unakubali au haukubali isipokuwa ni kwanini hukubaliani na hayo maandiko yangu.....

Hakuna mahali popote nilipoielezea sayansi kwenye maelezo yangu isipokuwa nimeelezea hali halisi,hali halisi inaweza kuwa ni sayansi kwa sehemu tu na inaweza ikawa siyo sayansi kwa sehemu kubwa.Makosa yako ni kuanza kufikiri namna hii.....

Unasoma maandiko yangu huku unaongozwa na mihemko,nitakueleza ni kwanini nakuambia hivyo....

Hakuna mahali nimesema kuwa mwisho wa darubini ni maili 2 isipokuwa nimekuambia kuwa huwezi kutumia darubini yenye uwezo mdogo kutaka kuona sehemu inayohitaji darubini yenye uwezo mkubwa na nikatoa mfano wa umbali wa maili 2.Wewe umesema "hata ukitumia darubini 'kali' kiasi gani huwezi kuona",hivi Zenji kuna umbali upi? unajua darubini ya uwezo wa juu zaidi iliyoko duniani ni ya uwezo upi?

Ushawahi kuitumia?

Unahemkwa hadi unashindwa kuzingatia vitu vidogo kama hivi kwenye maandiko yako....

Kwa logic ya kuiona meli ambayo huioni kwa macho yako inashindikana nini kuiona Zenji?

Usijali,soon utajua ni nani kati yangu mimi na wewe anayeifanya kazi ya Shetani,nadhani hata Shetani humjui wewe.....

Kivipi?
Duh, mbona unaandika kwa mihemko kiasi hiki mkuu?? Kuna nini??
Ishu hapa nibkwamba hatujakubaliana kimtazamo, mfanyakazi wa shetani anatoka wapi tena!!
Tufanye "nimekuelewa", case closed kati ya mimi na wewe, HAPPY NOW??
Cheerz!
 
Mtoa post mim niljua nawewe umefanya utafit wako binafsi nakuja na ushahid kamil kuthibitisha ilo ila naonà umekot tu hao hao wazungu wenye mtizamo tofaut na wale wanaosema dunia ni duara.Na wanaosema dunia ni duara wanahoja zaid maana wanasema kitu kinachofikirika ata kwa akil ya kimaskin ambao hatuwez kwenda uko anga ya juu nakupiga picha ila tunaweza kwenda uchina ama amerika nakuona tofaut ya masaa na majira na wameleta angalau na picha ya dunia.Jambo jingine unaposema kuna vitu vinafichwa wakat aya mambo yote yako kwenye mitandao mtu yoyote dunian anaweza soma kama wewe ulivyosoma nakutuletea.Mim nikushaur kua badala yakuleta mawazo ya binadam wengine wabish wasio na uthibitisho kua dunia ni tambarare ungefanya kwanza nawewe tafit ili uje na kitu kipya zaid vinginevyo ngoja tuendelee kuamin wanaosema dunia ni duara.
 
Kwa hiyo wewe unataka kuniambia nyota mchana tunaziona kwa macho yetu , wakati gani nyota zibaonekana kwa macho yetu, ni kipi kinachozuia mchana tusione nyota .
Nimemjibu mwezako kuwa kuna mabonde, milima, mitelemko na miinuko misri hatuwezi tukaiona na kubaliana na wewe kabisa . Hakuna kitu chochote kilichopo katika kinachozuia Mars isionekane.
Alafu kingine uliwahi kujiuliza kwa Nini baadhi ya wanyama wakati wa usiku macho yao yanang'aa, Binadamu tunaweza kujificha usiku pasipo macho yako kuonekana. Ingekuwa vizuri ungekuwa una juwa jicho la Binadamu linatoa volt ngapi?
Huu ni mstali Wako "" Mwanga wa blue ni mwanga wa jua sio mwisho wa macho kuona"" hivi unapoambiwa Mwisho wa uwezo Wako wa kuona unajuwa tunamaanisha Nini.

Ukisimama juu ya mlima Kilimanjaro kuna kitu gani kinachozuia usiione misri? Au kuna mlima mrefu zaidi ya Kilimanjaro ambao unazuia? Dunia kuwa duara ndio Inatuzuia tusiione misri. Sio milima wala bonde.
Na mwanga wa blue sio mwisho wa macho yetu kuona labda mimi sijaelewa ulimaanisha nini. Ila ule ni mwanga tu wa jua ambao pia unatuzuia tusione nyota mchana, au wewe unajua mchana nyota huwa zinapotea ndo mana hatuzioni?..
 
Yani na wewe unamuamini kabisa...
Nyota hutoa mwanga ndo maana tunaiona... sayari ya mars hutoa mwanga ndo maana tunaiona...

Zanzibar na misri zingekuwa bondeni au kilimani ungeziona kama zingekuwa znatoa mwanga wa taa zake usiku...
Mars haitoi mwanga. Mars tunaiona kwasababu inamulikwa na mwanga wa jua ambao pia unamulika misri na Zanzibar. Tena dunia upo karibu na jua kuliko mars so dunia ingekua flat misri ingeonekana vizuri kuliko mars kwasababu kuna mwanga zaidi.
 
Dunia flat kama CD???... Hahahaaa... nacheka kwa dharau
 
Kwanini anga ina umbo kama la duara?

Je anga nalo ni duara?

Hao hao wataalam unaowasikiliza wanasema kuwa unaona duara ya anga kama duara kutokana na macho yako tu lakini haipo hivyo.Lakini linapokuja suala la kuona mbali na kuibuka kwa meli wanasema ni kwasababu ya duara tufe ya dunia,ajabu kabisa hii.....
Kaka hope unafahamu nini kinasababisha rainbow, reflection na refraction ya mwanga wa jua kwenye waterdrops, na rainbow inatokea duniani na since Dunia iko Spherical basi hizo droplets za maji zinafata hiyo spherical shape ya dunia na zinapopigwa na mwanga zinaonyesha hiyo round petern
 
Back
Top Bottom