Tatizo lako linaakisi matatizo ya watu wengi sana.......
Unaposoma maandiko halafu ukashindwa kuyaelewa unayatupia maandiko hayo lawama badala ya kuchunguza kama wewe ndiyo hujaelewa na maandiko hayo hayana tatizo kabisa.Ni sawa na wewe uwe umesimama barabarani na jamaa zako wanne ambao wanakuambia kuna gari la rangi ya bluu linapita barabarani na wewe unaendelea kukodoa na hulioni gari hilo,badala ya kufikiria tu kuwa inawezekana macho yako yana matatizo hivyo yanakufanya usilione gari hilo,wewe unakimbilia kusema jamaa zako ni waongo na gari hilo halipo.....
Nimezungumzia dunia flat ya CD,haiwezekani uwe na flat ya namna hiyo halafu kuwe na upande wa pili wa duara.Tatizo nililoliona hapa ni wewe kushindwa kusoma maandiko mengi na kuyaelewa.Kwenye maandiko yangu hapo juu nimezungumzia dunaia duara ya tufe kwa namna tofauti na dunia duara ya CD kwa namna tofauti,nikatoa na mifano. Nadhani mfano wa chungwa ndiyo umekuchanganya kabisa maana niliutoa nikionesha tofauti kati ya duara ya CD na duara ya tufe [chungwa] na uwezekano wa kuuona mti.....
Suala la upande wa pili lilikuwa kwenye duara ya chungwa na siyo duara ya CD.Nilisema mti uliosimikwa kwenye chungwa huwezi kuuona kwenye duara ya chuingwa unapokuwa upande mwingine wa duara ile hata ukitumia chomb cha kuonea mbali lakini, kwenye duara ya CD ambapo hakuna upande wa pili,ukisimika mti kisha ukaenda umbali wa kilomita 10 hutaweza kuuona mti huo pia lakini,ukitumia kifaa cha kuonea mbali unauona.....
Sasa kwa kutumia logic hiyo,meli inapokuwa haionekani kwenye macho yako baada ya kwenda mbali,wale ambao wanasema dunia ni duara ya tufe hudai kuwa unakuwa huioni kwasababu inakuwa imeshapotelea kwenye duara ya dunia hivyo inakuwa kwenye upande mwingine wa duara hiyo.Lakini ukichukua kifaa cha kuonea mbali unaiona meli hiyo.Swali la msingi,je kwanini uione wakati iko kwenye upande mwingine wa duara ya dunia?
Kama dunia ni duara ya tufe usingeweza kuiona meli hiyo na ungeishia kuona maji tu pale yalipopinda lakini ni kinyume chake,meli inaonekana bado na hii inathibitisha kuwa dunia ni flat lakini duara kama CD.Kama vile mti ukiusimika kwenye barabara ya urefu wa kilomota 10,halafu mti ule ukausimika mwanzo wa barabara ile kisha ukaenda umbali huo wa kilomita 10 ukatazama hutaweza kuuona mti ule,hii haimaanishi dunia imepinda kutokana na duara yake kama tufe bali huuoni kwasababu macho yako hayana tu uwezo wa kuona umbali huo.Ukichukua kifaa cha kuonea mbali utauona huo mti bila matatizo yoyote,hii inaonesha kuwa dunia haijapinda bali ni flat.....
Nadhani umenielewa....