Siri niliyoipata katika kufunga siku 21 kila mwanzo wa mwaka

JAMBO NI KUFANYA SIYO KUONGEA

Mambo haya siyo ya kuongea tu.
Mimi ninachokisema kipo kinafanyika. Wewe ni uchaguzi wako. Maarifa haya yapo na wengi huyatumia.

Kuna dini na madhehebu yapo yameandaa SALA na DUA katika maandishi. Wale watu wakikaa wiki au zaidi ya wiki wamejifungia kwa jambo hilo hilo huku wamefunga, hakika nakuambia litatokea.

Halafu haya mambo ninayoyaongelea hapa ni masuala ya IMANI. IMANI(Hisia) lazima ihusiane na MATAKWA(will)

FAITH AND WILL
vikiungana kwa pamoja lazima jambo litokee.

Wengine wanasema huwezi kumshawishi Mungu kupitia kufunga na kusali.
Watu hapa wanaongelea kitu tofauti kabisa. Hapa tunaongelea kuingia katika ulimwengu wa roho.
 
Ahsante kwa muongozo, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Dah sie mbwa tumenyimwa chakula cha watoto
 
Maelezo yako hayatoshelezi kujibu swali kuu. Je, unafundisha watu kufunga kwa msingi wa Mungu yupi?

Unaposema hakuna manabii una maana unapingana na maandiko katika Yoeli 2:28, 1 Wakorintho 12:10 na Warumi 12: 6
Unabii ni karama itokanayo na Roho Mtakatifu hivyo unaposema hakuna manabii maana yake unapingana na Neno la Mungu.

Kwenye suala la kuzungumza na wafu. Neno la Mungu limekataza kabisa (forbidden) kuzungumza na wafu. Soma Kumbukumbu la torati 18:10-12. Kwa kwesi ya Sauli na Samweli hili ni somo kamili lakini kwa ufupi ijulikane kuwa kabla ya Yesu kuja, kufa na kufufuka yeyote aliyekufa alikuwa anaenda kuzimu na kuzimu ilikuwa imegawanyika chini na juu, chini walienda walio na dhambi na juu walienda wasio na dhambi soma Luka 16:19-23 Sasa ileweke Samweli alienda kuzimu lakini juu na matokeo ya Sauli kuzungumza na Samweli mfu yalikuwa ni kifo soma 1 Samweli 28:1.......; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami;.... sasa maneno haya mtakuwapo pamoja nami yaliimaanisha Sauli na wanawe watakufa na kweli Sauli na wanawe walikufa keshoyake.

Utaratibu wa watu wasio na dhambi kwenda kuzimu ulikoma baada ya Yesu kufa msalabani na kushuka kuzimu kufanya vita na kumnyang'anya shetani funguo za kuzimu na mauti ndio maana saa tisa Yesu alipokata roho miili ya watakatifu ilifufuka soma Mathayo 27:52-53.

Hivyo kufunga kwetu kusitukoseshe na Mungu, na iwelewe kufunga hakubadilishi mapenzi ya Mungu ila kunakubadilisha wewe kukubali mapenzi ya Mungu yatendeke.
 
Boss chapisho hili ni zuri sana, je una maarifa juu ya tahajudi(meditation).
 
Soma nilichokiandika kabla ya kuanza kujibu kitu ambacho sichakiongelea hapa.

Wapi nimesema hakuna manabii!?
Nimesema kunatofauti ya Nabii na mtu anayeweza kuona.
Nikasema wale wanaojiita manabii kwa sasa asilimia kubwa ni waonaji hawana tofauti na wapiga ramli.

Halafu hapa ninaongelea suala la kufunga. Je unaweza kuniuliza kuhusu suala hilo!?

Cha pili ungefuatilia uzi huu na ukaelewa msingi wa mtu aliyekuwa anauliza swali. Kukatazwa kuongea kwenye vitabu vya dini haiwezi ikaondoa uwepo wa ulimwengu wa roho na existence yao katika ulimwengu huo.
 
Asante kwa mada nzuri, nimeipenda sana na ninaamini itabadili maisha yangu. Swali langu kwa vile ni wa siku 21 je tunaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa na wenza? maana mwingine anaweza asielewe. Pia kama mie ni beginner, usually nafungaga ya saa 12, je siwezi nikawa nakunywa kitu kizito zaidi ya asali na maji? Mfano vegetable/green juices?
 
Nasubiria funga aina nyingine.. nimewahi kuweka nia ya kufunga na nkafunga mwaka jana kipindi cha kwa resima.

Ila ilivyofika saa 9 ntapambana na njaa na hasira na myu naye qkaja akanivuruga end of the story nkashusha hasira na kitimoto
Kwani kufunga lazima uache kula??.Mimi nafikiri kufunga inahusisha mambo mengi zaidi ya kujinyima kula, Nijuavyo Mimi unaweza kula tu kiasi kwaajili ya kuendeleza uhai,lkn ukajinyima vitu visivyo vya lazima,km vile unywaji wa bia au soda,ulaji wa Vyakula vizuri vizuri na vya gharama,n.k.Kisha pesa uliyoisevu kutokana na kujinyima kupeleka kwa wahitaji km vile kwenye nyumba za kulelea Wazee, watoto yatima, wagonjwa walioko mahospitalini au majumbani, watoto wa mitaani,n k.,Jambo jingine muhimu ni sala na kuomba toba na pia kutoa msamaha kwa waliokukosea au wewe kuomba radhi kwa wale uliowakosea.Ukiyafuata haya, naamini funga yako itakuwa na maana sana.
 
Neno la Mungu linataka ukifunga ufunge kwa Siri mtu asijue, Yani hata mdomo upakwe mafuta usipauke.

Sasa mbona mnatangaza kufunga na kujulikana fulani kuwa kafunga?
 
Hivyo kufunga kwetu kusitukoseshe na Mungu, na iwelewe kufunga hakubadilishi mapenzi ya Mungu ila kunakubadilisha wewe kukubali mapenzi ya Mungu yatendeke.

Nime note hili kufunga hakubadilishi mapenzi ya Mungu,bali kufunga kunatufanya sisi kukubali mapenzi ya Mungu yawe kama alivyokusudia.
 
Nimefuatulia bandiko lakini sijaona hitimisho la faida ambayo wewe uliipata baada ya kufanya hiyo meditation '

Yaani baada ya kumaliza huo mfungo ulinufaika kwakupata Nini ,

Let say uliamua kufunga kwaajili ya kuomba Kazi je ulipata (mfano tu )
 
Vip ndani ya hizo siku sex inaruhusiwa, au ndio itakuwa huwazi kabisa
 
Vip ndani ya hizo siku sex inaruhusiwa, au ndio itakuwa huwazi kabisa
Ukiona unaingia kwenye mfungo kama huo na bado unawaza sex basi fanya kuhairisha mpaka wakati mwingine. Maana kama una dhamira ya kweli ya kufanikisha jambo, wazo la sex huwa linapotea kabisa kichwani.

Alafu sidhani kama utakuwa na hiyo energy baada ya kama siku nne za mwanzo, wengine siku tatu tu mwili unaanza kujikataa.
 
Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…