Siri usiyoijua kuhusu ndoto na tafsiri zake

Ingekua hivyo basi ingekua balaa kweli kweli
 
Mimi nimeota nipo shule na nilikuwa nataniana na wenzangu kuhusu maswali ya shairi, Mimi nikatania kuwa utakuta swali linasema mstari wa pili katika ubeti wa 50 na ngapi huko unasemaje au baada ya nukta Fulani yanafuata maneno gani? Yaani nikawa natania vitu ambavyo sidhani Kama vipo ,mwishowe nimecheka kicheko kitamu kweli na kicheko kile sijawahi kukicheka maishani mwangu hatimaye nikashituka (hii ndoto Ina maana gani boss?)
 
Niliota nimepata ajali ya gari nikatoka salama,nikaona gari inaendelea kunguruma ikiwa chini nikaenda kuizima nilipo lizima hapo hapo likawaka moto hii inamaana gani.maana kweli natumia gari kila siku.
 
[emoji1][emoji1]
Mbona umecheka ?

Nimeuliza swali la msingi sana
Na mleta mada hajanijibu...

Ni sawa na kumpa mtu chakula kitamu halafu akakuuliza umepika pikaje hiki chakula? Ili na mimi nikapike nile?

Ukikataa kumjibu kuna sababu zifuatazo

1. Kama ni chakula cha biashara basi unaogopa kutoa ujuzi ili kulinda soko lako

2. Kama ni chakula cha Nyumbani basi itakuwa ni uchoyo tu wa maarifa...
 
Nimeota tupo kwenye mashua tunavuka maji mara ghafla kukatokea dhoruba kubwa cjui ni baharn au mtoni lakn tuliweza kufanikiwa kuvuka na kifika ng'ambo salama ckumbuki kama kwenye ndoto hyo nilikuwa nahofu wakat wa dhoruba hiyo.
 
Mwaka jana kati sikumbuki ni mwezi gani ila kati ya june-august hivi. Kuna ndoto niliota aisee niliogopa kuwahadithia watu, maana kama kakichekesho wewe sasa ukutane na wazito hivyo ukae nao ah wapi sikuipa umuhimu.

NDOTO YA KWANZA

Niliota nipo sebleni mimi Hayati Magufuli (R.I.P) na Lowasa sikua muongeaji hata huko ndotoni baada ya muda Lowasa akatoka ndani nikajikuta nina kisu nikamchoma nacho Magufuli tumbuni nikakivuta kutoka upande a kwenda upande b (mf. kutoka kushoto kwenda kulia) sikuumia wala kushtuka wala kuona kuumizwa na tukio hilo huko ndotoni ndipo nikashtuka kurudi mwilini. Hii naikumbuka vyema.

Ndoto nyingine ya pili ni hii;

Usiku wa kuamkia jana.

Niliota nipo na mdada(namjua) mmoja hivi mahali kwenye watu gafla nikamshikana mkono nikaanza kumkimbia nae tunaelekea pori flani hivi ila tukafanye ngono. Tukafika huko, nikawa namchezea mwili wake ile hali ya kuiba iba sasa shughuli ikawa kufanya nae ngono anataka na mimi nataka ila hatufanikiwi kufikia lengo...
Baada ya muda kidogo nikashtuka.

Nini hasa maana ya hizi ndoto.?
 
Naota sana harusi mkuu,tena sherehe kubwa na watu wamejaa wamependeza saa zingine wameshona hadi sare ila katika ndoto zote maharusi siwaoni ila tu tunasherehekea,ndoto hii nmeota mara tatu ndani ya miezi miwili hii
 
Elimu ya kutafsili ndoto ni ngumu sana anyway mkuu jitahidi kusoma maana nimesoma unayoyaandika ni machache ambayo uko sawa acha kuwalisha wenzako matango poli
 
Elimu ya kutafsili ndoto ni ngumu sana anyway mkuu jitahidi kusoma maana nimesoma unayoyaandika ni machache ambayo uko sawa acha kuwalisha wenzako matango poli
Toa wewe tafsiri kama unaona kaz nyepes ,binadamu siku zote hujiona wajuaji hata Mungu akishuka mtampinga tuu. To a fact zako ueleweke unasema kama wadada wa uswahilin yaan hiyo tunaita mipasho ,na mwanaume kuwa na mipasho ni dhahiri una matatizo yamekusibu si bure .Na ukitaka naweza kukujulisha nini haswa huwasumbua watu kama nyie kwenye akili zenu,hili ni somo pana sana,maana nakuona uko mtupu kabisa umeamua kujiandikia tuu,ila una tatizo kubwa sana usipoangalia litaathiri mpaka imani yako,na maono yako,Kaa na Mungu mkuu la sivyo .......
 
Kuota unapaa! Wakati huo upo angani unarushwa na wachawi, kitandani pamebaki kitu kinachofanana na wewe! Wanakuchezea na kukurudisha .
 
Pia epuka kula ukashiba sana kipindi cha usiku maana ndoto zake hazielezeki unaweza.
 
Ndio umeambiwa usitusahau wenzio kwenye mafanikio yako sasa.
 
Niliota tunachimba Kaburi pembeni ya kaburi la Ndugu yangu, halafu nikakutana na Mifupa ya Ndugu yangu inaporomokea kwenye Kaburi tunalochimba la karibu.
Naomba tafsiri yake Mkuu!

Mpaka leo inanitesa maana ilinistua saana.
 
Elimu ya kutafsili ndoto ni ngumu sana anyway mkuu jitahidi kusoma maana nimesoma unayoyaandika ni machache ambayo uko sawa acha kuwalisha wenzako matango poli
Ni kweli kabisa hata mimi naona mengi anaenda chaka
 
Baba yangu jana aliota kuwa nimezungukwa na maaskari, na mimi nikaota nimemeza nyama iliyokuwa imekaangwa kwenye mafuta bila kuitafuna. Nikaota tena kuna sehemu nilikuwa nimekaa ghafla nikajihisi kama kuwashwa flani hivi, kuja kucheki nikaona kama kinyonga flani hivi kikiwa kimevimba hatari
 
Nimeota chui ama simba anataka kuni shambulia
 
Mkuu habari Mimi huwa naota nimekunja miguu napaa hewani kunakundi lawatu linanikimbiza hao watu siwa jui.huwa wananikimbiza hawanikamati Ila wao hawapai angani Mimi tuu ndo huwa napaa nikiwa nimekunja miguu.
 
Kuota uko uchi mbele za watu na unapambana kuijisitiri ila unashindwa hadi ukishtuka unaona kama nikweli. Hii imekaaje Mkuu!!?

Pia kuota kila mara uko kwenye kipindi cha mitihani na unakua hujajiandaa,unakua na hofu mpaka ukishtuka inakua kama kweli vile,nayo vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…