Siri usiyoijua kuhusu ndoto na tafsiri zake

Asante kwa tafsiri za ndoto nimejifunza kitu pia na majibu mengine nimepata humohumo
 
Mkuu mie karibia kila siku naota ndoto ila huwa nakumbuka kipengele kidogo sana katika hiyo ndoto au nisikumbuke kabisa.
Je,hili ni tatizo au hali ya kawaida? Na ninaweza kuondokana vip na hii hali ya kusahau ndoto zangu?
Natanguliza shukrani
 
MSAADA PLEASE
Nilikuwa nasafiri kwenda mahali. Njiani nikamuota mtu ambae hatujawasiliana muda kidogo. Nimemuota mara mbili
Mara ya kwanza alikuwa anatembea usiku
Mara ya pili hivyo hivyo anatembea usiku nikawa namwambia usiende huko akawa hanisikii
JE HII NDOTO INA MAANA YOYOTE AU NI WENGE TU LA SAFARI?
 
@mtarimbo
 
mm niliota kua nilipita karibu na sehem ya duka alilokua anafanya kaz marehemu rafiki angu aliefariki week3 zilizopita.ghafla tulikua eneo lile lakini tulikua tunakunywa chai ya moto sana.cha ajabu alikua anatoka jasho sana na alikua anavuja damu kidg kwenye jeraha lake kichwani .akaniambia anaomba awe mrinzi wangu.yan shadow ili awe ananilinda
 
Maagano hayo, tena baado mapya kabisa.. Omba toba, na umkabidhi Mungu maisha yako.
 
Ndio unakumbuka hapo tu?

Umeota muda wa usiku.. anaenda aehemu.. ukamuambia asiende..

Au ndo unakumbuka hapo tu?

Je mazingira unayafahamu? Na aliko kuwa anaelekea unakufahamu?
 
Akina nani wanamwambia acheue? Je kaka yako ni muhimu/mtu mwenye msaada sana katika familia yenu?
 
Ndio unakumbuka hapo tu?

Umeota muda wa usiku.. anaenda aehemu.. ukamuambia asiende..

Au ndo unakumbuka hapo tu?

Je mazingira unayafahamu? Na aliko kuwa anaelekea unakufahamu?
Nakumbuka hivyo tu hata mazingira siuakumbuki
 
Na mm ngoja niseme yangu
Niliota nipo ikulu kuna shughuli zinaendelea ghafla akaja askari mmoja akaniambia msafara wa raisi unapita na kweli nikaona iveco ya jeshi imekuja kwa kasi ikiwa na wanajeshi wamejaa basi nikasogea pembeni ghafla akaja yule askari na kikaratasi akaniambia kampe yule akataja jina ila akasema watu wasijue unachofanya sikumuona sura ila alinitajia Jina basi mm nikajiongeza nikaanza kumtafuta kwenye kundi la maaskari sikumuona itabidi niwe naita jina chinichini ili ajue namtafuta
Ghafla yule askari aliyenipa kikaratasi akamuona yule askari akampa kingine na mm nikampa changu baadae yule askari akaniambia nifuate huku tunakimbia palepale ikulu kuna chumba tukaingia nikakuta maaskari wengi wanamachine za kushona nguo yule aliyeniingiza mule chumbani akaingia chumba kingine nikabaki na niliowakuta mule ndani, wakasema tutajie Jina lako nikawatajia lakini alivyoliandika akalikosea nikarekebisha baadae akasema nipe force namba yako mm sijui lolote nawaza hii ni nn? Ghafla yule aliyeniuliza akasema nishajua kazi yako basi akaja yule nikiyekuwa nae akaniambia kuna hela utalipwa ila kabla hujalipwa utatakiwa uzime simu zako zote kwa muda harafu baadae ndio uwashe utakuta pesa yako nikamuachia namba yangu wakati nataka kuchukua yake nikastuka
Ndoto hii maana yake nn wakuu
 
Ujumbe wa ndoto hii umefichwa hapo mwisho kabisa ambapo ulishtuka kabla hujachukua hiyo namba... Nikisema ujumbe umefichwa, namaanisha KUNA MAELEKEZO HUJAYAFAHAMU BADO, Nenda Mbele za Mungu Omba Toba kwanza kisha Muombe akupe huo ujumbe uliofichwa.

Yaweza kuwa ndoto ya MAFANIKIO, ombea pia MTU ALIYEBEBESHWA MAONO KWA AJILI YAKO
 
Naomba uniambie na mm hii in maana gani. Nimeota mm Ni mlinzi wa rais kikwete pia kipindi Cha magufuli nimeota nipo ikulu namlinda magufuli na ananipa maelekezo nafuata, wakati wasamia pia nimeota namlinda waziri mkuu majaliwa. Pili naota Sana naokota matunda Aina ya parachichi sanyingine najaza kapu wakati mwingine nachuma machache hizo ndoto haishi mwezi zinakuja za rais kila akija rais mpya mm nakua mlinzi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…