Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MSAADA PLEASEKwanza nianze kwa kuelezea ndoto maana yake,
Ndoto ni mkusanyiko wa matukio ambayo binadamu huyaweka kichwani kwake ambayo humjia bila zuio (involuntary) kwenye ubongo wakati akiwa amelala,matukio haya huwa hayaeleweki na saa nyingine huwa kinadharia zaidi mfano kuota unapaa wakati kiualisia haiwezekani.
Kiujumla sayansi imeshindwa kuja na jibu kamili kuhusu ndoto ,na matokeo yake wameishia kutoa tafsiri hiyo .
Ukija kwenye dini ndoto huwa ndio njia maalumu ambayo ulimwengu wa Roho hutumia kuwasiliana na binadamu, hapa sasa ndio nataka tuanze.
Kibibilia Mungu hutumia matukio tuliyoyaifadhi au kumbukumbu za vitu tulivyoifadhi moyoni ,ili kutengeneza codes za mawasiliano kati yake yeye na sisi .
Sasa kuna mambo kadhaa ambayo huwa ukiota lazima ujue kufungua hizo codes ,ni maarifa rahisi ila inahitaji uwe mcha Mungu na mwerevu.
Mfano
1:Ukiota unapaa angani
Ndoto ya namna hii ukitaka kuifahamu lazima ujue kwa nini Mungu katumia anga,anga maana yake ni ulimwengu wa nuru ,ardhi ni ulimwengu wa giza ,hivyo ukiota unapaa ni taadhari kutoka kwa Mungu kwamba uache kutembea kwenye ulimwengu wa giza ,hamia ulimwengu wa nuru, nikuhakikishie ukifanya hivyo hutakaa uote tena kupaa sure.
2: Kuota unafanya mapenzi
Codes za ndoto hii ni mbili kulingana na mazingira yako,mfano ukiota unafanya mapenzi na ukiamka unajihisi mchovu na mara nyingine kama mwanaume unahisi umemaliza ,basis ujue kuna pepo wachafu wanakuchezea.
Ila ukiota unafanya mapenzi na ukiamka hakuna ishara yoyote nikimaanisha uchovu au uchafu basi ndoto hii huwa ni njema code ya mapenzi ni pesa maana ni kipi kinapendwa zaidi ya mapenzi kama si pesa hivyo ukiota unafanya mapenzi ni ishara ya kupata pesa, kama unayefanya naye humjui basi utapata pesa kwenye vyanzo usivyotarajia.
Kama umeota unafanya mapenzi na mtu unayemjua basi ujue utapata pesa zaidi kwenye vyanzo vyako vya kiuchumi unavyovijua.
3;Kuota uko darasani ,na kufanya mitihani
Hii ndoto code yake ni hivi jiulize ni nini hukupa wasiwasi kama kama kipindi uko shule hasa wakati wa mitihani kama kukosa pesa wakati wa matatizo, hivyo ndoto hii ukiota ni onyo kutoka ulimwengu wa roho kwamba kuna matatizo makubwa yatakujia na yanahitaji pesa hivyo unahitaji kuweka akiba ya pesa ,upunguze matumizi la sivyo hilo tatizo litakuaibisha.
4;Kuota kusalitiwa kimapenzi
Code yake ni hivi ni nini huumiza moyo na kuuvunja moyo kama usaliti wa kimapenzi? jibu ni msiba.
Hivyo kama umeota mwenzi wako anakusaliti na kiuhalisia si kweli basi ni ujumbe wa kifo kwa huyo uliyemuota either yeye, familia yake watakumbwa na tukio la msiba hivyo muombee huenda bado ulimwengu wa roho haujaidhinisha hilo janga.
Itaendelea kesho, pia ukumbuke somo la ndoto lilikuwapo tangu zamani Yusuph alisoma kupitia vitabu alivyoiba mama yake RHaheli wakati anatoka kwa baba yake aliyekua mganga na mtabiri alijulikana kama Laban, Danieli alisomea huko uajemi enzi za utumwa.
Na binadamu huota zaid ya ndoto 20 kwa siku ,ndoto yenye ujumbe huwa unaikumbuka vema na huwa inaushtua moyo.
Nyingine huwezi kuzikumbuka maana huwa kazi yake ni kuufanya ubongo ufanye kazi vizuri ,hivyo siyo ndoto zote ni ujumbe unatakiwa uwe mwerevu wa kusoma mazingira na hali yako.
@mtarimboMSAADA PLEASE
Nilikuwa nasafiri kwenda mahali. Njiani nikamuota mtu ambae hatujawasiliana muda kidogo. Nimemuota mara mbili
Mara ya kwanza alikuwa anatembea usiku
Mara ya pili hivyo hivyo anatembea usiku nikawa namwambia usiende huko akawa hanisikii
JE HII NDOTO INA MAANA YOYOTE AU NI WENGE TU LA SAFARI?
Maagano hayo, tena baado mapya kabisa.. Omba toba, na umkabidhi Mungu maisha yako.mm niliota kua nilipita karibu na sehem ya duka alilokua anafanya kaz marehemu rafiki angu aliefariki week3 zilizopita.ghafla tulikua eneo lile lakini tulikua tunakunywa chai ya moto sana.cha ajabu alikua anatoka jasho sana na alikua anavuja damu kidg kwenye jeraha lake kichwani .akaniambia anaomba awe mrinzi wangu.yan shadow ili awe ananilinda
Ndio unakumbuka hapo tu?MSAADA PLEASE
Nilikuwa nasafiri kwenda mahali. Njiani nikamuota mtu ambae hatujawasiliana muda kidogo. Nimemuota mara mbili
Mara ya kwanza alikuwa anatembea usiku
Mara ya pili hivyo hivyo anatembea usiku nikawa namwambia usiende huko akawa hanisikii
JE HII NDOTO INA MAANA YOYOTE AU NI WENGE TU LA SAFARI?
Akina nani wanamwambia acheue? Je kaka yako ni muhimu/mtu mwenye msaada sana katika familia yenu?Mmm mama angua alimuota kaka angu tumbo lake lilikuwa linaonekana kama glass nikimaanisha unaonatumboni kilichomo ndani na alikuwa anaona limejaa maziwa mengii wa anamwambia acheue au ateme mate chini alipotema likapasuka maziwa ya kaanza kumwagika hii ina maana gani kiongozi?
Shukrani BossInaweza isiwe na maana kubwa zaidi ya kuota mawazo au hisia zako mwenyew juu ya hofu uliyonayo kila siku kuhusiana na ajali au chombo chako
Nakumbuka hivyo tu hata mazingira siuakumbukiNdio unakumbuka hapo tu?
Umeota muda wa usiku.. anaenda aehemu.. ukamuambia asiende..
Au ndo unakumbuka hapo tu?
Je mazingira unayafahamu? Na aliko kuwa anaelekea unakufahamu?
Tubu, kisha muombe Mungu akufunulie kwa upya ujumbe wa hiyo ndoto.Nakumbuka hivyo tu hata mazingira siuakumbuki
Ujumbe wa ndoto hii umefichwa hapo mwisho kabisa ambapo ulishtuka kabla hujachukua hiyo namba... Nikisema ujumbe umefichwa, namaanisha KUNA MAELEKEZO HUJAYAFAHAMU BADO, Nenda Mbele za Mungu Omba Toba kwanza kisha Muombe akupe huo ujumbe uliofichwa.Na mm ngoja niseme yangu
Niliota nipo ikulu kuna shughuli zinaendelea ghafla akaja askari mmoja akaniambia msafara wa raisi unapita na kweli nikaona iveco ya jeshi imekuja kwa kasi ikiwa na wanajeshi wamejaa basi nikasogea pembeni ghafla akaja yule askari na kikaratasi akaniambia kampe yule akataja jina ila akasema watu wasijue unachofanya sikumuona sura ila alinitajia Jina basi mm nikajiongeza nikaanza kumtafuta kwenye kundi la maaskari sikumuona itabidi niwe naita jina chinichini ili ajue namtafuta
Ghafla yule askari aliyenipa kikaratasi akamuona yule askari akampa kingine na mm nikampa changu baadae yule askari akaniambia nifuate huku tunakimbia palepale ikulu kuna chumba tukaingia nikakuta maaskari wengi wanamachine za kushona nguo yule aliyeniingiza mule chumbani akaingia chumba kingine nikabaki na niliowakuta mule ndani, wakasema tutajie Jina lako nikawatajia lakini alivyoliandika akalikosea nikarekebisha baadae akasema nipe force namba yako mm sijui lolote nawaza hii ni nn? Ghafla yule aliyeniuliza akasema nishajua kazi yako basi akaja yule nikiyekuwa nae akaniambia kuna hela utalipwa ila kabla hujalipwa utatakiwa uzime simu zako zote kwa muda harafu baadae ndio uwashe utakuta pesa yako nikamuachia namba yangu wakati nataka kuchukua yake nikastuka
Ndoto hii maana yake nn wakuu
AmenMtumaini Mungu, Muomba Mungu hachoki kwani hiyo ndio kazi yetu sisi tulioumbwa na Mungu
sijaelewaMaagano hayo, tena baado mapya kabisa.. Omba toba, na umkabidhi Mungu maisha yako.