Sisi Wakristo huwa ni wachoyo sana kwenye sikukuu zetu ukilinganisha na Waislamu

Sisi Wakristo huwa ni wachoyo sana kwenye sikukuu zetu ukilinganisha na Waislamu

Kwani kukaribisha lazima??!!...majirani zangu wasubiri x mass sikaribishagi watu pasaka😀
 
Changamoto ni kwamba huwa hawana imani na chakula cha waKristo.Mara huyo kuku alichinjwa na nani?Hivyo vyombo mara ya mwisho kusafishia pua na masikio ya "ng'ombe" ilikuwa lini?Mara sikukuu yenu haijulikani halafu weye ni kafiri!Unapeleka msosi ili usimangwe halafu kimwagwe?Bora kuwa "lichoyo" tu.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Huo ndio ukweli.
 
Kuna dini fulani ni walafi sana, mbona hata sisi huwa tunafunga ila kelele za vyakula hutasikia.
Binadamu tunaunafiki sana yan watu wakifunga yan matangazo kama yoteee. MUNGU hataki yakoo. Utasikiaaa ohhb mwezi huuu mwezi huuu
 
Changamoto ni kwamba huwa hawana imani na chakula cha waKristo.Mara huyo kuku alichinjwa na nani?Hivyo vyombo mara ya mwisho kusafishia pua na masikio ya "ng'ombe" ilikuwa lini?Mara sikukuu yenu haijulikani halafu weye ni kafiri!Unapeleka msosi ili usimangwe halafu kimwagwe?Bora kuwa "lichoyo" tu.😂😂😂😂
Ishi maisha halisi na hayo ndio maisha halisi unafiki si issue.
Maswala ya kuulizana kachinja nani huo ni uduanzi
 
Mimi jamaa yangu kwa kuwa anajua nimefunga mwezi mtukufu wa Ramadhani ananialika mara mbili mbili aisee kesho Usikose bwanaaa ufike saa tatu asubuhi tuanze na mchemsho daaah..
Anajivua lawama huyo
 
Kwema wakuu?

Tuseme ukweli tu sisi wakristo kwenye sikukuu zetu ni wachoyo sana ukilinganisha na waislamu.

Mfano hapa mtaani kwetu ninapoishi ,tunaishi watu wa dini tofauti lakini dini zilizotawala ni Islam na Christian.

Sasa bana sisi wakristo kwenye sikukuu zetu huwa kila mtu kajifungia getini kwake na familia yake, ila kiukweli hawa wenzetu waislamu wakiwa na sikukuu zao au hata shughuli zao tu za kifamilia ebana mtaa mzima mtakula na mtasaza chakula.

Mfano last year ilikua iddy sijui ile yani hapa mtaani ilikua unabembelezewa mualiko, ila sisi wakristo sasa hatuna huo ukarimu.

Tubadilike jamani.
Sio wachoyo ila tukiwakaribisha hawa respond sababu ya issue za kuchinja nazani
 
Kyagata wee Kiagata mpaka dk hii umemkaribisha nani?
Usiwajumuishe wakristo wote kwenye uchoyo wako.

Najua mama angu kule home atapika na atawapakulia kina bibi Swabra na Mama Ostadhii… na wao Eid watamkaribisha bi mdashi.

Mimi sijakaribisha mtu sababu sina ratiba ya kupika, kesho kuna nyumba naenda kuvamia bila taarifa [emoji16]
Nikaribishe basi shem darling
 
Kwema wakuu?

Tuseme ukweli tu sisi wakristo kwenye sikukuu zetu ni wachoyo sana ukilinganisha na waislamu.

Mfano hapa mtaani kwetu ninapoishi ,tunaishi watu wa dini tofauti lakini dini zilizotawala ni Islam na Christian.

Sasa bana sisi wakristo kwenye sikukuu zetu huwa kila mtu kajifungia getini kwake na familia yake, ila kiukweli hawa wenzetu waislamu wakiwa na sikukuu zao au hata shughuli zao tu za kifamilia ebana mtaa mzima mtakula na mtasaza chakula.

Mfano last year ilikua iddy sijui ile yani hapa mtaani ilikua unabembelezewa mualiko, ila sisi wakristo sasa hatuna huo ukarimu.

Tubadilike jamani.
Mwaliko ni hiari
 
Back
Top Bottom