Sisi Wakristo masikini tunanufaika vipi na shule za Kanisa?

Kumbe hili swali tunajiuliza wengi...
Pamoja na mafanikio haya ,Shule nyingi za Kanisa ,gharama zake za masomo ni ghali sana! Pengine kuliko hata shule za watu binafsi!
Hali hii huwafanya Wakristo wengi masikini wasinufaike na hizi shule!


Mmechangia kweli kanisa au mnalalamika tu kwa kuwa wengine walichangia? Mara nyingi wanaohojihoji matumizi ya kanisa ni wale ambao huwa hawachangi au wakichanga basi ni kwa mbinde na kwa masimango
 
Vitega uchumi vinatokana na nini ?
 
Msingi wa maendeleo ya kanisa ni michango ya waamini iwe zaka iwe sadaka vyote viko termed kama michango yao. Msingi wa ujenzi wa chuo, zahanati,benki, kanisa etc vyote hivyo % kubwa inatokana na michango ya waumini.
Swali fikirishi, je, hiyo michango baada ya kulinufaisha kanisa muumini wa kawaida ananufaika na nini?!
Au anaishia kupata ibada ya kuzikwa na kubatiza watoto wake?!
 
Ndio mjifunze makanisa sio taasisi za yesu ni taasisi za ujasiriamali kupitia jina la Mungu na Yesu !!!!na wajinga ndio waliwao!!ni pamoja na hao wanaopeleka watoto wao kwenye hizo shule!!
 
Mfumo uliopo ni wa kinyonyaji 100%. Shule hizo zinajenga kupitia sadaka Za maskini. Shule ikikamilika wanaoweza kusoma huko ni Watoto wa matajiri ambao pia hawakuijenga hiyo shule.
 
Sasa kama unaona hupendezwi si utoke??!mijitu mingine hovyo sasa unawaambia din nyingine ili iwaje??πŸ™„πŸ™„πŸ™„ umasikini utawauwa nyie nyumbu, nenda kwenye din nyingine
Collective Imbecilization victim....pole sana!
 

Kwanza ungejiuliza umekuwaje masikini wakati Bibilia inasema uliumbwa utawale? Ungejiuliza Kwanini huyo Mungu awanague? Wachache wawe matajiri huku nyie wengi ndo masikini?
 
Una hoja unayopaswa kujibiwa basi zama zimebadilika pesa imetamalaki hadi altareni
 
Ukiwa na pesa na ukaoa na kuzaa nje ya ndoa utazikwa na padre ila ukiwa kapuku hata katekista haji utazikwa kiongozi wa kwaya.
 
Na usipochanga halafu wanakujua una kakipato wananuna kishenzi hawajui tu watu wanapitia mangapi mtaani!?
 
huu ni mfano wa majibu yanayotolewaga na viongozi wetu wa dini
Majibu ya kikauzu balaa πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Shule za dini zinazofaulisha vizuri ada ni kubwa hivyohivyo, za kiislamu nazo ni hivyo ila tofauti ni kwamba hazijengwi kwa michango ya waumini. Taasisi inayoanzishwa ndiyo inajenga, huku Tanga zipo zilianza kama madrassa, wanafundisha kwa ada na baadaye wakaja kufikia kuanzisha chekechea na kisha msingi mtaji ulipopanuka. Hatimaur wakaja kuleta sekondari zao.

Pia zipo taasisi zingine zilianzishwa na waislamu wanaojiweza, zikaja kumiliki shule zao.

Mfano Tanga kuna shule ya sekondari ada ni Sh Mil 5, na sijawahi kusikia imetoa div 4 au zero. Mwaka huu ina div 1 53, 2 zipo 19 na 3 zipo 5 tu.

Shule za kidini kuwa na ada kubwa si tatizo balo tatizo ikiwa inaendeshwa kwa michango na wanaotoa kiwa hawanufaiki. Ila kama iliundwa kwa nguvu za taasisi wakawekeza pesa ya kutosha si jambo baya hilo. Maana taasisi ni watu na hao watu wana maisha pia, inabidi wapate riziki kupitia huko.
 
Kuna shule inaitwa St.Joseph Cathedral, St. Francis hio ya mbeya hapo bila 4.5m kwa mwaka mtoto wako hasomi, shule za kanisa zote ada zao ni ghali sana...
 
Wakisomesha bure masikini elimu yao itashuka. Kanisa linafanya biashara na halipo tayari kupata hasara nendeni huko kayumba
Kwani yesu haangushi manoti kanisani?
 
Nyie masikini mnapata sifa shule zenu zimeongoza na kuwacheka waislam, kwani kwenye mpira timu yako ya ulaya ikishinda wewe shabiki wa nanjilinji unapata nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…