Sisi Wakristo masikini tunanufaika vipi na shule za Kanisa?

Ingawa umejikita kwa KKKT lakini mimi nimeshakutana na hiyo adha pale nilipojaribu kumtafutia Mwanangu nafasi kwenye moja ya shule zinazisimamiwa na Kanisa Katoliki kupitia moja ya tawi lao la Masista.

Ada zipo juu sana na hata uombe vipi sidhani kama utapata bahati ya kusikilizwa.

Ninachojiuliza hizi shule si ndio zinapata 'ruzuku' kutoka Makanisa tunayoyatolea sadaka kila wakati wa Ibada?.

Hivi hizi shule zilizo chini ya Kanisa/ Masista/Mapadri n.k kwa nini zisiwe na uataratibu kama unaofanywa na Shule ya st Jude Arusha?.
 
Suluhisho ni kutafuta njia ya kupata ufadhili kwa watoto wa masikini wanaofaulu vizuri mitihani ya kujiunga na shule hizi. Bila kufanya hivi tabaka la masikini na matajiri litazidi kuwa kubwa.
Inasikitisha ndani ya Jamii moja kuna Watoto wanasoma shule yenye miundo mbinu yote ya kumuwzsha Mtoto asome vizuri na wengine ndio hao wa kutebea kilpmita saba kila siku kwenda shule isiyo na hata robo ya miundo mbinu iliyokamilika kwa Mtoto kuapata elimu.

Haya Makanisa na Taasisi yoyote ya Dini wajitafakari ni nini majukumu yao hapa Duniani...hiki kinachofanyika ni ubaguzi tu na hakuna tafsiri nyingine.
 
Ingawa umejikita kwa KKKT lakini mimi nimeshakutana na hiyo adha pale nilipojaribu kumtafutia Mwanangu nafasi kwenye moja ya shule zinazisimamiwa na Kanisa Katoliki kupitia moja ya tawi lao la Masista.

Ada zipo juu sana na hata uombe vipi sidhani kama utapata bahati ya kusikilizwa.

Ninachojiuliza hizi shule si ndio zinapata 'ruzuku' kutoka Makanisa tunayoyatolea sadaka kila wakati wa Ibada?.

Hivi hizi shule zilizo chini ya Kanisa/ Masista/Mapadri n.k kwa nini zisiwe na uataratibu kama unaofanywa na Shule ya st Jude Arusha?.
KKKT ,nilitumia kamq mfano TU!
 
Inasikitisha ndani ya Jamii moja kuna Watoto wanasoma shule yenye miundo mbinu yote ya kumuwzsha Mtoto asome vizuri na wengine ndio hao wa kutebea kilpmita saba kila siku kwenda shule isiyo na hata robo ya miundo mbinu iliyokamilika kwa Mtoto kuapata elimu.

Haya Makanisa na Taasisi yoyote ya Dini wajitafakari ni nini majukumu yao hapa Duniani...hiki kinachofanyika ni ubaguzi tu na hakuna tafsiri nyingine.
Kwa hiyo ni lazima ,tuchukue hatua!
 
Kwanini uwe masikini tuanzie hapo..?pia tambua hizo taasisi hazijiendeshi bure..kuna bills wanalipa kama mishahara..maji..umeme..ulinzi..chakula..n.k
Unadhani sadaka yako ya buku kila siku ya ibada inatosha kulipia hizo gharama?

Kama uonaona elimu ni gharama jaribu ujinga.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mnachangia kanisa kujenga shule, vyuo na hospitali ilihali gharama zinazotozwa baada ya ujenzi ni kubwa na nyie nyie mliochanga hamuwezi kuafford..

Serikali ikiintroduce tozo mchangie ujenzi wa madarasa, mahospitali...mnapiga kelele balaa..
Mnaonaje sasa nguvu hiyo hiyo ya kujenga mashule na mahospitali ya makanisa tukaielekeza kuchangia ujenzi wa shule za umma na mahospitali ya umma na Watanzania wote wakasoma?
 
Leo matokeo ya Mitihani ya Darasa la nne na Form Four yametoka!

Kama kawaida shule zinazoongoza nyingi ni zile zenye Uhusiano na Kanisa ,iwe kwa umiliki au kwa njia nyingine! Hii bila shaka inatoka na misingi Bora iliyowekwa!

Pamoja na mafanikio haya ,Shule nyingi za Kanisa ,gharama zake za masomo ni ghali sana! Pengine kuliko hata shule za watu binafsi!

Hali hii huwafanya Wakristo wengi masikini wasinufaike na hizi shule!
Kwangu mm nafikiri hiki ni kinyume na misingi ya Ukristo na hata ubinadamu!
Ilitarajiwa basi wenye shule nao wanufaike!

Wote ni mashahidi Kwa mfano,upande wa KKKT kumekuwa na michango ya kuchangia Seminary kadhaa hapa nchini!
Lakini n vipi hawa masikini Wananufaika ambao ndio wanaochanga kuku na mbuzi wao,na wengine huchangia kwa maombi
Ilhali ada za shule hizi ni sawa na kipato Cha familia masikini kwa mwaka mzima!

Je, hao hawana haki ya hii Elimu Bora!
Je, Kanisa linaona hii hali!?

Hali haipo tofauti pia ktk Hospitali za Kanisa,Waumini wengi hawana ubavu wa kuingia hospitali kadhaa za ambazo ni ghali.

Ni vipi Msharika wa Maskini wa Loita Dayasisi ya Meru anaweza kupata huduma Bora za afya ktk Hospitali ya Selian aliyaoichangia kwa miaka mingi!

Nafikiri kuna kitu hakipo SAWA! Ndani ya Kanisa na Sisi Waumini pia!

Tutafakari!
Kwani wana CCM masikini wananufaika nini na viwanja vya mpira ambavyo kwa wakati mmoja watanzania wote walichangia kuvijenga na sasa umiliki uko CCM?
Shule nyingi zilizoongoza na zinazomilikiwa hasa na kanisa katoliki si zao la moja kwa moja la michango ya waumini Bali kanisa limejenga kwa vyanjo vyake lenyewe.
Ukiangalia historia ya nchi hii elimu ililetwa na kanisa na shule nyingi zilikuwa zakanisa zikifundisha wanachi wote bure.....Wakati wa azimio la Arusha shule hizi zilitaifishwa na serekali ikaanza kuziendesha
Kanisa lilianza tena jenga shule zingine na mojawapo ni hizo zinazoongoza sasa...so kanisa katoliki limesaidia sana watanzania maskini kielimu na afya sidhani kama wanastahili lawama yeyote kwa status ya shule zao sasa.
 
Ni wakati sasa wakubadili mindset zetu, baadala ya kuchangia ujenzi wa mashule ya makanisa na misikiti au mahospitali ya makanisa na misikiti sasa uwe wakati wa kila Mtanzania kuchangia michango hiyo kujenga shule na hospitali za umma..

Serikali ipige marufuku michango ya kujenga mashule, mahospitali, mavyuo ya taasisi za kidini baadala yake waumini wachangie tu majengo ya ibada, madarasa ya sundayschool au madrasa tena ndani ya eneo la kanisa au msikiti... SHULE, HOSPITALI, VYUO VIBAKI MALI YA UMMA NA WATU BIANAFSI pasipo mafungamano na dini yeyote ile..

Mwalimu Nyerere alipobinafsisha mashule ya dini na mahospitali ya dini alikuwa sawa sana ili kuja kuondoa matabaka kwenye jamii hasa yahusuyo imani za kidini..
 
Mkuu maada yako ina mashiko sana tena sana...

Ila mm naona sis kama wenye uwezo wa chini ambao tunaumizwa moja kwa moja...ni bora tutoe mapendekezo yaani namna gani ziendeshwe ili asilimia kubwa ya wazazi wawezi kupeleka watoto wao huko....
Maana kuendesha hizi shule pia ni ghalama sana kutokana na ubora wake...

Pia kumbuka kunashule nyingi watu wanaosma bure ..mfano pale ndanda kuna chuo zaidi y watahiniwa 5000 wanaosomeshwa na kanisa..
Kuna shule ya sec ipo Mwanza pale misungwi ya masister..hii mtoto akifanya interview yao akafaulu basi mzazi hulipi chochote..mapaka form 4.hawa wote ni machango ya waumini inawasomesha..
Zipo na nyingine..
Labda mm ningependekeza kwa upande wa katoriki..huku najuia kila jimbo kunawatoto linasomesha bure kabisa..kwenye seminary zao mbali mbali...
Japo bado kwa shule ada zao ni kubwa.mno..

Sasa tufanyaje?

Kila mtu apendeke wazo lake
 
Kwani wana CCM masikini wananufaika nini na viwanja vya mpira ambavyo kwa wakati mmoja watanzania wote walichangia kuvijenga na sasa umiliki uko CCM?
Shule nyingi zilizoongoza na zinazomilikiwa hasa na kanisa katoliki si zao la moja kwa moja la michango ya waumini Bali kanisa limejenga kwa vyanjo vyake lenyewe.
Ukiangalia historia ya nchi hii elimu ililetwa na kanisa na shule nyingi zilikuwa zakanisa zikifundisha wanachi wote bure.....Wakati wa azimio la Arusha shule hizi zilitaifishwa na serekali ikaanza kuziendesha
Kanisa lilianza tena jenga shule zingine na mojawapo ni hizo zinazoongoza sasa...so kanisa katoliki limesaidia sana watanzania maskini kielimu na afya sidhani kama wanastahili lawama yeyote kwa status ya shule zao sasa.

ni sawa tu waachiwe kujenga na kujenga mashule na mahospitali na wakatoriki wakasome huko, na waislam nao kesho nao waanze sasa kujenga mashule na mahospitali yao na waislam wakapate huduma huko..

Kesho na keshokutwa, misikiti na makanisa yaanze kujenga hoteli zao, kuwa na mabasi yao, ndege zao nk huduma nyinginezo na watu wadini hizo wazifuate huduma huko...
 
Dini yetu ya ukristo imekaa kiupigaji zaid. sio elimu tu hata huduma zao zingine mfano za hospital ni gharama mno, dini ni baishara tu kama biashara nyingne.. ngoja maskin wafia dini watavyokuja kukushika mashati hapa.
Yawezekana ukawa kwako ukiristo ni huduma kama ngurumo za upako au hujui mchango wa ukiristo katika elimu na afya ya watanzania....makanisa ya Roman Catholic, Lutheran,Anglican n.k yamefanya makubwa katika kumsaidia mtanzania maskini.kielimu na Afya....sasa wenye jukumu la kutoa elimu bure ni serikali si makanisa..makanisa tayari yalishatekeleza hilo na serikali ikazichukua shule zao (za makanisa)
 
Leo matokeo ya Mitihani ya Darasa la nne na Form Four yametoka!

Kama kawaida shule zinazoongoza nyingi ni zile zenye Uhusiano na Kanisa ,iwe kwa umiliki au kwa njia nyingine! Hii bila shaka inatoka na misingi Bora iliyowekwa!

Pamoja na mafanikio haya ,Shule nyingi za Kanisa ,gharama zake za masomo ni ghali sana! Pengine kuliko hata shule za watu binafsi!

Hali hii huwafanya Wakristo wengi masikini wasinufaike na hizi shule!
Kwangu mm nafikiri hiki ni kinyume na misingi ya Ukristo na hata ubinadamu!
Ilitarajiwa basi wenye shule nao wanufaike!

Wote ni mashahidi Kwa mfano,upande wa KKKT kumekuwa na michango ya kuchangia Seminary kadhaa hapa nchini!
Lakini n vipi hawa masikini Wananufaika ambao ndio wanaochanga kuku na mbuzi wao,na wengine huchangia kwa maombi
Ilhali ada za shule hizi ni sawa na kipato Cha familia masikini kwa mwaka mzima!

Je, hao hawana haki ya hii Elimu Bora!
Je, Kanisa linaona hii hali!?

Hali haipo tofauti pia ktk Hospitali za Kanisa,Waumini wengi hawana ubavu wa kuingia hospitali kadhaa za ambazo ni ghali.

Ni vipi Msharika wa Maskini wa Loita Dayasisi ya Meru anaweza kupata huduma Bora za afya ktk Hospitali ya Selian aliyaoichangia kwa miaka mingi!

Nafikiri kuna kitu hakipo SAWA! Ndani ya Kanisa na Sisi Waumini pia!

Tutafakari!
Kuanza kufikiri hivi ni mwanzo wa kupata akili kwa waumini wengi ambao mmefungwa na ujinga wà kwenye dini..
Mnatumiwa sana na huko kanisani huhubiriwa upendo, na kama kuna pendo la kweli, hili wazo hebu lipeleke kwenye umma wa waumini wote, unaweza kufukuzwa ushirika mara moja
 
ni sawa tu waachiwe kujenga na kujenga mashule na mahospitali na wakatoriki wakasome huko, na waislam nao kesho nao waanze sasa kujenga mashule na mahospitali yao na waislam wakapate huduma huko..

Kesho na keshokutwa, misikiti na makanisa yaanze kujenga hoteli zao, kuwa na mabasi yao, ndege zao nk huduma nyinginezo na watu wadini hizo wazifuate huduma huko...
Uzuri ni kuwa ukiachana na seminary za kuandaa mapadre shule na hospitali za kikiristo zilihudumia na zinaendelea kuhudumia watu wa jamii yeyote bila kujali rangi wala dini ya mtu
 
HINDU wajenge shule zao wasome huko na biashara wafanye wenyewe kwa wenyewe.
BOHORA nao wajenge mashule yao wasome huko na biashara wafanye wenyewe kwa wenyewe.
ISLAM wajenge shule zao wasome huko na biashara wafanye wenyewe kwa wenyewe.
CHRISTIAN wajenge shule zao wasome huko ma biashara wafanye wenyewe kwa wenyewe..

tumekuwa tukizilalamikia jamii za kihindi na kiarabu kwa ubianafsi wai juu ya biashara za wao kwa wao pamoja na kujitenga na kuishi wenyewe wenyewe katika nchi yetu ikiwa pamoja na kuoa na kuoleana wenyewe...

Leo hii tunashangilia uwepo wa shule na hospitali za Kikristo na Kiislam katika nchi yenye watanzania weusi ambao walipaswa kuujenga mfumo wao wenyewe kwa kuwa na shule bora za umma, mahospitali bora ya umma na huduma bora za kijamii za umma...baadala yake watu hawa wanachangia michango na kujenga mashule bora, mahospitali bora ya makanisa na misikiti..
 
Kwani wana CCM masikini wananufaika nini na viwanja vya mpira ambavyo kwa wakati mmoja watanzania wote walichangia kuvijenga na sasa umiliki uko CCM?
Shule nyingi zilizoongoza na zinazomilikiwa hasa na kanisa katoliki si zao la moja kwa moja la michango ya waumini Bali kanisa limejenga kwa vyanjo vyake lenyewe.
Ukiangalia historia ya nchi hii elimu ililetwa na kanisa na shule nyingi zilikuwa zakanisa zikifundisha wanachi wote bure.....Wakati wa azimio la Arusha shule hizi zilitaifishwa na serekali ikaanza kuziendesha
Kanisa lilianza tena jenga shule zingine na mojawapo ni hizo zinazoongoza sasa...so kanisa katoliki limesaidia sana watanzania maskini kielimu na afya sidhani kama wanastahili lawama yeyote kwa status ya shule zao sasa.
Mkuu ,Mimi waakati St Augustine inajengwa nilikuwa Mwanza na kulikuwa na michango ya kufa Kwa waumini wote!
Hoja hapa ni kuwa Maskini wanaochangia kanisa wananufaika vipi na Biashara hizo zikikamilika?
Hivi unajua kina shule za Kanisa wanatoza ada 4m!
 
Uzuri ni kuwa ukiachana na seminary za kuandaa mapadre shule na hospitali za kikiristo zilihudumia na zinaendelea kuhudumia watu wa jamii yeyote bila kujali rangi wala dini ya mtu
...kipato je?!
 
Back
Top Bottom