Sisi Wakristo masikini tunanufaika vipi na shule za Kanisa?

Sa si ugome kuchanga? Umeshikiwa bunduki? Binafsi sichangi mchango wowote wa kanisa zaidi ya sadaka.
Nimevimbiwa nimetoka kula ugali na mbaazii
Juzi Kati kuna katekista aliniuliza Kuhusu bahasha fulani wanatoaga za mwisho wa mwaka.

Kwanza nilishangaa nikasema Muulize mama fulani,kumbe mimi nilishakataa kitambo kuchangia kwa hiyo nikamwambia mwanamke akomae mwenyewe atafute pesa mimi sina.

Sitakagi ujinga mimi,mahospital yao yote gharama kubwa,mashule ndio hivyo na hakuna kitu wanatoa hata kuwashukuru waumini.
 
Mi ni KKKT nilishaachaga kutoa sadaka ya mambo ya mfuko wa elimu sijui benk mara hospital maana vikiisha hata siwezi kuvimudu hata mwanangu sitaweza kumsomesha hapo. Hizo ni business na wanaofaidika ni hao waliojuu wanaondesha V8. Na siku ukinyoosha kidole kuuliza Haya mambo watakuparura kila kona maana unawaingilia maakuli yao. We makanisa yana kila ruzuku kutoka serikali ie hawana wakodi kama sekta binafsi but still wanafamya biz kabisa. Huku zikiwa zimejengwa BURE kabisa na waumini Masikini.... Ni WIZI.
Now Kanisa ni Business entity sio tena kueneza Injili na ndio maana mahubiri yao 90% ni pesa... 5% mafanikio 5% ndio injili ya Yeshua.
 
Nilitegemea waumini wao waliokidhi vigezo vya utumishi wa Kanisa ulioyukuka angalau kupewa upendeleo fulani na pia waumini wao wawe Wana bima ya nafuu kwenye huduma za jamii maana hizo taasisi zinaendeshwa.kibiashara na Kwa sadaka zao.

Pia lengo liwe huduma sio biashara.
 
Halafu hizi shule zunapokea misaada kutoka Roma na huku wanacharge ada kubwa
 
Muumini maskini anachangia ujenzi wa shule ya kanisa, shule ikikamiliza Ada inakuwa kikwazo kwa mtoto wa maskini kusogelea shule hiyo.
 
Unachosemaa ni kwamba kanisa lianzishe Social Protection schemes!
 
Muumini maskini anachangia ujenzi wa shule ya kanisa, shule ikikamiliza Ada inakuwa kikwazo kwa mtoto wa maskini kusogelea shule hiyo.
Inaumiza sana ...ninlazima tusimame kidete kupinga
 
Michango yenu inatumika kujenga shule za gharama kwa ajili ya watoto wa ma don nyie mnaochanga muwapeleke watoto wenu Saint Nyangema
 
Toa sadaka kwa wingi ili ujiwekee hazina mbinguni ambako wevi hawataiba, ya dunia yanapita.
Bwana asifiwe!
 
Ndugu yangu Tafuta fedha vinginevyo umasikini sio mzuri!!...Shule za Misikiti nazo Ada zao zikoje?!!....
 
Tupe na Islamic schools!!
 
Unakuta mmachangishwa mjenge kanisa,mnachanga weee miaka 10 kanisa linaisha..mnahamia.Mnaanza tena kuchangishwa eti ujenzi wa Kitega uchumi cha kanisa na vitisho kibao vya maandiko...bila hiyana mnachanga mnajenga hicho kitega uchumi,kikimalizika mapato yote wanakula wao.

Dadaadeki sitoi zaidi ya buku 3 kwa wiki kanisani hizo zinawatosha.
 
Hii ndiyo Prof Chachage aliita Collective Imbelization....!
Ambayo Kanisa na CCM wanaitumia sana kuwachezesha Sindimba!
Halafu CCM watoto wao ndiyo wanasoma kwenye hizo shule.Kanisa linawapenda kwa sababu huwa hawasumbui kulipa ada.
 
Kanisa ndo limekusababishia umaskini wako?

Hao wanaopeleka watoto hizo shule wanawezaje?

Pambana na hali yako it's everyman for himself dunia ya leo usipende vya bure.
 
Umaskini sio sifa
 
Hili si tatizo la kkt tu, ni madhehebu yote ya kikristu pamoja Sda pia, wakati wa ujenzi mnatangaziwa kuchangia, unajitutumua kuchangia. Lakini inapofikia mtoto wako kusoma kwenye hizo shule zao sarakasi ziaanza, kwanza interview na kama mtoto hajapata wastani walio weka hata kama una hela na mshiriki uiyeichangia shule mtoto hasomi.
Pengine mtoto amefikisha wastani na unaamua kukijitutumua na viela vyako vya mawazo unamlipia ili asome siku ukikwama tu kidogo anarudishwa kama kawaida.
Hitimisho mimi nilishaamua sichangii shule wa chuo nitaenda kulipia huduma wakishajenga Shule zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…