Leo matokeo ya Mitihani ya Darasa la nne na Form Four yametoka!
Kama kawaida shule zinazoongoza nyingi ni zile zenye Uhusiano na Kanisa, iwe kwa umiliki au kwa njia nyingine! Hii bila shaka inatoka na misingi Bora iliyowekwa!
Pamoja na mafanikio haya, Shule nyingi za Kanisa gharama zake za masomo ni ghali sana! Pengine kuliko hata shule za watu binafsi!
Hali hii huwafanya Wakristo wengi masikini wasinufaike na hizi shule! Kwangu mimi nafikiri hiki ni kinyume na misingi ya Ukristo na hata ubinadamu!. Ilitarajiwa basi wenye shule nao wanufaike!
Wote ni mashahidi Kwa mfano, upande wa KKKT kumekuwa na michango ya kuchangia Seminary kadhaa hapa nchini! Lakini ni vipi hawa masikini Wananufaika ambao ndio wanaochanga kuku na mbuzi wao na wengine huchangia kwa maombi ilhali ada za shule hizi ni sawa na kipato Cha familia masikini kwa mwaka mzima!
Je, hao hawana haki ya hii Elimu Bora!
Je, Kanisa linaona hii hali!?
Hali haipo tofauti pia ktk Hospitali za Kanisa,Waumini wengi hawana ubavu wa kuingia hospitali kadhaa za ambazo ni ghali.
Ni vipi Msharika Maskini wa Loita Dayasisi ya Meru anaweza kupata huduma Bora za afya ktk Hospitali ya Selian aliyaoichangia kwa miaka mingi!
Nafikiri kuna kitu hakipo SAWA! Ndani ya Kanisa na Sisi Waumini pia!
Tutafakari!