Sitaki kuzini: Sijawahi kuona kama ana dalili za kuoa na sitaki kumwambia unioe

Sitaki kuzini: Sijawahi kuona kama ana dalili za kuoa na sitaki kumwambia unioe

Habari za mida hii ndugu zangu

Nmekuja nipate ushauri maana naona kila ninalotaka kuliweka mezani napangua.

Nimekuwa na mahusiano na kijana mmoja kama miezi miwili hivi au mitatu. Alinikuta sina mtu na tukaanzisha uhusiano (Huyu mtu ananijua na tunajuana maana tumetoka sehemu moja na tumesoma wote primary na alikuwa ananipenda toka primary na baadae huku ukubwani, ila imetokea tumedate mwaka huu.

Mimi ninasali na mwenzangu sio kiivo japo hajawahi kunipa changamoto za mimi kumtafuta Mungu. Nilipoanza nae mahusiano ghafla nkaona kama narudi nyuma kiroho (nimepitia mengi mpaka kujiconnect zaid na Mungu na ndio ilikuwa pona yangu)

Nilirudi nyuma kiroho nikawa namiss mambo mengi ya kanisani japo hakuwahi nizuia. Niseme tu nilirudi nyuma na vita nilivyokuwa napitia mwanzo vilirudi kwa kasi. Nikamuomba anipe space maana nilishindwa kubalance Mungu na mapenzi(alikuja moto maana kunipata aliona kama nini sijui).

Tukaaa week akaniomba kuwa nimpe nafasi atajitaidi kuweka chachu ya mimi kusali, nikarudi tena. Ikaenda nikawa napitia mambo mengi kiroho na kila siku kanisani naombewa na nikaambiwa mlango unaowapa nafasi Adui ni Uzinzi. Nikaletewa ndoto kuhusu uzinzi unavonilostisha(wanaojua mambo ya kiroho wanaelewa) nikaamua kusikiliza na kuacha uzinzi.

Nilichojia hapa ni kuwa niongee vipi na mwenzangu aelewe kuwa sipo tayari kuzini, maana mtu asiyesali ataona kama nachekesha. Asiwaze namuacha kwa sababu nyingine ila sina sababu zaidi ya hiyo.

Ningeweza kusema labda aamue kama ananioa au vipi ila katika story sijawahi kuona kama ana dalili za kuoa na sitaki kumforce wala kumwambia unioe lakini sitaki kuzini. Naombeni ushauri niongee nae vipi.

Ukiona huna ushauri pita tu, Kuna watu wajuaji sana HUMU.

IMG-20210505-WA0174.jpg
 
Mkuu mambo mengine ni utoto unajiita mlokole umezin kabla ya ndoa saiz eti unasema hutak kuzin tena nina hasira nao hawa kuna manzi mmoja nilimsotea kinoma kama miez sita mm nikajua kikombe mm ndio takivunja alikua ananiambia hawez kufanya bila ndoa siku moja akaachia kuweka mpini ukazama nilishangaa sana
Huwezi kujua mtu amepitia yapi mpaka akafikia hatua ya kuokoa,elewa kuwa sikuwahi kuokoa,Kwaiyo nlishazini before.Saiv ndio nmeamua kuishi maisha mapya,Mungu akusaidie uwe mwepesi wa kuelewa kabla ya kucoment kitu kwa mtu.
 
Vitu gani ambavyo huwezi kuvivumilia kwenye maumbile?
Umevijuaje?

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Mimi sio mbaguzi ila let say mke wangu amefanyiwa FGM na mimi siwezi kuishi na mwanamke aliyefanyiwa FGM,lakini mimi sikugundua hilo maana hatukuwahi kuvuliana nguo..huoni hili litapunguza upendo na ndoa itakuwa hatarini kwani tayari mimi mume nitakuwa sifurahii tendo?.

N.b
Walaaniwe wale wote wanaowafanyia FGM watoto wa kike bila concern yao.
 
Mpenzi (mtaje kwa jina lake),

Kuna jambo linanitatiza sana. Na kwa hili naomba nikueleze yanayonisibu.

Kwanza, tambua ya kuwa nakupenda na hakika nakupenda mno. Hilo halina shaka yeyote na wewe walifahamu vema. Naamini ya kuwa hata wewe unanipenda.

Pili, naamini ya kuwa misuko suko ya hapa na pale hayatahitimisha mapenzi yetu kama kweli yanatoka miyoyoni mwetu. Tumeshajenga msingi, kinachofuata ni ukuta imara wa kutukinga.

Tatu, najua fika ya kuwa mapenzi (kulalana) ni nguzo moja imara katika kuimarisha mahusiano. Na tumeshafanya hivyo mara kadhaa. Unanijua nje ndani.

Lakini, hivi karibuni nimeanza kupitia misukosuko fulani (itaje). Na nimeoteshwa pia ndoto juu ya misukosuko hii (mhadithie ilivyokuwa). Na katika kutafuta suluhisho la changamoto hii, nimeelezwa kuwa usinzi ndiyo mlango unapotokea. Na nikijaribu kufikiri naona kama kweli kwa kuwa kabla ya hapo haikuwa hivi.

Kwa hiyo, ikikupendeza naomba tuendelee kuwa wapenzi bila ya kushiriki tendo la ndoa mpaka pale ambapo tutafunga ndoa. Narudia nia yangu siyo kukunyima tendo kwa sababu ni kwa manufaa yetu sote. Na ingekuwa hivyo nisingekubali tangu hapo mwanzo.

.......

Kaa tulia mpe akujibu. Mtapata muafaka na utaendelea na maisha.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Pole dada kwa changamoto unayopitia
Mimi kwa ushauri ni kuwa;
Ukianzisha mahusiano lazima uyapime uone ni ya Ngono tu au yanakupelekea kwenye Ndoa?
Ukianzisha mahusiano na mtu, kwa muda mfupi akaanza kutaka papuchi jua hayo mara nyingi sio muoaji
Muoaji haweki papuchi kipaumbele kwani anajua mipango ikikaa sawa atakuwa mmiliki hivyo hana haraka

Mimi ninachofikiri;
Endelea na mahusiano ILA usimpe tena papuchi kwani inaonekana wewe huna uzoefu na hayo mambo, LAKINI muhimu zaidi, utakapo mnyima ndio utaona uelekeo wake kama ni muoaji au anataka kujitimizia; Na kama ni muoaji na wewe upo tayari AKAJITAMBULISHE KWENU
Akingangania au Kuzira; Piga chini kwani sio muoaji

Mwisho; hukusema unarudije Nyuma huko kanisani:
Hupati muda wa kuhudhuria kwa kuwa unakuwa busy?
Vioi shuhuli zako za kimaisha zinakwendaje? au ni huko kanisani pekee?
Asante kwa ushauri Mparee2,nmekuelewa sana sana.
 
Yaani kidume nisipime quality ya papuchi niuziwe mbuzi kwenye gunia?..Hivi vitu kwa dunia ya sasa ni rarely possible.
Me too....i chase to bash but quality ones i struggle to keep. Sasa ilitokea wife materials kashanielewa kila kitu na guest/geto anakuingia ila ataki tutumie mpaka eti niende kwao... whaaat im not that nut. 3 incidents wananielewa ila no testing dah kidume siezi kubali mbuzi kwenye gunia lazma nitest kwanza is it alive? Is it healthy?
 
kwa mfano wewe mwanamke ulishatembea na mwanamme wako tuseme miaka hata 5 halafu mkaachana, umeanza mahusiano mengine yana mwaka mmoja. Halafu unafosi huyu jamaa mpya akuoe do you think that's fair
Ni sawa tu.
Mwanamke kufanya dhambi wakati uliopita,haimpi uhalali wa kuendelea kuitenda eti kwa sababu tu nyuma alishatenda.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Habari za mida hii ndugu zangu

Nmekuja nipate ushauri maana naona kila ninalotaka kuliweka mezani napangua.

Nimekuwa na mahusiano na kijana mmoja kama miezi miwili hivi au mitatu. Alinikuta sina mtu na tukaanzisha uhusiano (Huyu mtu ananijua na tunajuana maana tumetoka sehemu moja na tumesoma wote primary na alikuwa ananipenda toka primary na baadae huku ukubwani, ila imetokea tumedate mwaka huu.

Mimi ninasali na mwenzangu sio kiivo japo hajawahi kunipa changamoto za mimi kumtafuta Mungu. Nilipoanza nae mahusiano ghafla nkaona kama narudi nyuma kiroho (nimepitia mengi mpaka kujiconnect zaid na Mungu na ndio ilikuwa pona yangu)

Nilirudi nyuma kiroho nikawa namiss mambo mengi ya kanisani japo hakuwahi nizuia. Niseme tu nilirudi nyuma na vita nilivyokuwa napitia mwanzo vilirudi kwa kasi. Nikamuomba anipe space maana nilishindwa kubalance Mungu na mapenzi(alikuja moto maana kunipata aliona kama nini sijui).

Tukaaa week akaniomba kuwa nimpe nafasi atajitaidi kuweka chachu ya mimi kusali, nikarudi tena. Ikaenda nikawa napitia mambo mengi kiroho na kila siku kanisani naombewa na nikaambiwa mlango unaowapa nafasi Adui ni Uzinzi. Nikaletewa ndoto kuhusu uzinzi unavonilostisha(wanaojua mambo ya kiroho wanaelewa) nikaamua kusikiliza na kuacha uzinzi.

Nilichojia hapa ni kuwa niongee vipi na mwenzangu aelewe kuwa sipo tayari kuzini, maana mtu asiyesali ataona kama nachekesha. Asiwaze namuacha kwa sababu nyingine ila sina sababu zaidi ya hiyo.

Ningeweza kusema labda aamue kama ananioa au vipi ila katika story sijawahi kuona kama ana dalili za kuoa na sitaki kumforce wala kumwambia unioe lakini sitaki kuzini. Naombeni ushauri niongee nae vipi.

Ukiona huna ushauri pita tu, Kuna watu wajuaji sana HUMU.
Wajuaji tupo ili kuwaondolea ujinga mnaoukumbatia hapa! Hivi unaelewa kwamba huyo Nabii wenu anatembea na waumini wenzio humo humo kanisani licha ya vitisho vyake kwenu?

Swala jingine ni kuwa ukipenda ua penda na boga lake! Ukitaka mchumba ukubali na kugongwa kama hutaki kugongwa tafuta kaka wa kiroho muendele kusindikizana kwenye misa za week nzima!
 
Mimi sio mbaguzi ila let say mke wangu amefanyiwa FGM na mimi siwezi kuishi na mwanamke aliyefanyiwa FGM,lakini mimi sikugundua hilo maana hatukuwahi kuvuliana nguo..huoni hili litapunguza upendo na ndoa itakuwa hatarini kwani tayari mimi mume nitakuwa sifurahii tendo?.

N.b
Walaaniwe wale wote wanaowafanyia FGM watoto wa kike bila concern yao.
Kumbe ni FGM tu inayokupa wasiwasi,hakuna lingine?
Hayo mambo unatakiwa uulize kabla hamjafunga ndoa.
NB:Uulize,siyo ujaribu.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Hii ishu iko kiroho zaidi wengi hawawezi kukuelewa, mwambie kwa uwazi tafuta sababu yoyote yenye mantiki atakayoelewa then achana nae, ama punguza mawasiliano nae,

Wengine tukizini tunapitia mateso sana kwenye maisha unafulia mpk unakoma nafsi inatukutika tu muda wote, kwahiyo nakuelewa Sana tu unachopitia
 
  • Thanks
Reactions: ABJ
Ndo akae single mpaka pale atakapopata wake ambae atakubali kuvumilia mpaka watakapofungua ndoa, au adate na mtu wa kanisani kwake ili iwe rahisi maana ni imani moja wataelewana
Nasali Kkkt dia...sisali yale makanisa ya watu private ila tu kutokana na changamoto zangu,ilikuwa rahisi kuwa karibu na viongozi wa dini pale kanisani.
 
Baki na msimamo wako.
Mwambie ukweli.

Mungu ni wa thamani kuliko kitu kingine chochote..kuwa na Yesu ni bora kuliko vyote.
Kuna vitu lazima uvipoteze kwa ajili ya Mungu.

Wakati mwingine kabla hujaingia kwenye mahusiano muulize kwanza Roho mtakatifu.
Tulia sikia sauti yake.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Nashukuru sana,Kweli Mungu ni zaidi ya mtu na kitu.
 
Back
Top Bottom