Sitaki kuzini: Sijawahi kuona kama ana dalili za kuoa na sitaki kumwambia unioe

Sitaki kuzini: Sijawahi kuona kama ana dalili za kuoa na sitaki kumwambia unioe

Aisee pole Sana . Mbona mwenzetu shetani anakutesea sehem muhimu hivo..... Au ulisha wahi shiriki madhabau za kichawi na kujiwekea nadhiri juu ya papuchi yako.....? Mbona wengine wanapukuchuana na hakuna tatizo .


Ushauri wangu Anza kuanza kujua kwa nini wewe upo hivo na hayo mavitu uliyatoa wapi uyarudishe uendelee kuchakatwa Kama wengine
Acha kumpotosha mwenzako wewe. Iko hivi :
Ukiona wewe unatenda dhambi na hupati misuko suko na mwwnzako akitenda dhambi hiyo hiyo anapata misukosuko, basi fahamu kwamba Mungu kamchagua yeye na wewe kakuacha.
Imeandikwa kuwa wale watu ambao MUNGU anawapenda basi huwaadhibu pale wanapokosea kama vile baba avyowaadhibu watoto wake wakikosea. Soma MITHALI 3:11-12
 
Habari za mida hii ndugu zangu

Nmekuja nipate ushauri maana naona kila ninalotaka kuliweka mezani napangua.

Nimekuwa na mahusiano na kijana mmoja kama miezi miwili hivi au mitatu. Alinikuta sina mtu na tukaanzisha uhusiano (Huyu mtu ananijua na tunajuana maana tumetoka sehemu moja na tumesoma wote primary na alikuwa ananipenda toka primary na baadae huku ukubwani, ila imetokea tumedate mwaka huu.

Mimi ninasali na mwenzangu sio kiivo japo hajawahi kunipa changamoto za mimi kumtafuta Mungu. Nilipoanza nae mahusiano ghafla nkaona kama narudi nyuma kiroho (nimepitia mengi mpaka kujiconnect zaid na Mungu na ndio ilikuwa pona yangu)

Nilirudi nyuma kiroho nikawa namiss mambo mengi ya kanisani japo hakuwahi nizuia. Niseme tu nilirudi nyuma na vita nilivyokuwa napitia mwanzo vilirudi kwa kasi. Nikamuomba anipe space maana nilishindwa kubalance Mungu na mapenzi(alikuja moto maana kunipata aliona kama nini sijui).

Tukaaa week akaniomba kuwa nimpe nafasi atajitaidi kuweka chachu ya mimi kusali, nikarudi tena. Ikaenda nikawa napitia mambo mengi kiroho na kila siku kanisani naombewa na nikaambiwa mlango unaowapa nafasi Adui ni Uzinzi. Nikaletewa ndoto kuhusu uzinzi unavonilostisha(wanaojua mambo ya kiroho wanaelewa) nikaamua kusikiliza na kuacha uzinzi.

Nilichojia hapa ni kuwa niongee vipi na mwenzangu aelewe kuwa sipo tayari kuzini, maana mtu asiyesali ataona kama nachekesha. Asiwaze namuacha kwa sababu nyingine ila sina sababu zaidi ya hiyo.

Ningeweza kusema labda aamue kama ananioa au vipi ila katika story sijawahi kuona kama ana dalili za kuoa na sitaki kumforce wala kumwambia unioe lakini sitaki kuzini. Naombeni ushauri niongee nae vipi.

Ukiona huna ushauri pita tu, Kuna watu wajuaji sana HUMU.
Kama kweli unasali na kumtii MUNGU basi endelea kumwamini MUNGU, mkabidhi njia zako zote na yeye atakuongoza.
Ukimtumaini MUNGU atakuunganisha na Mume anayekufaa na siyo Mume unayemtaka wewe.
Kama huyo jamaa ni chaguo la MUNGU kwa ajili yako basi Yeye MUNGU atakufungulia njia na jamaa atakuoa. Wala huna haja ya kuhangaika kumshawishi akuoe, wewe tulia, mwamini MUNGU.
Lakini kumbuka, imani pasipo matendo ni bure. Imani yako kwa MUNGU ni lazima iambatane na "utiifu" na "sala".
 
Kuruka kiunzi cha uzinzi kwenye hii dunia ya sasa ni sawa na mtu kuponyoka adhabu ya kifo kwenye guillotine... Wale wote ambao wana Misheni ya kuacha uzinzi Mungu awatie nguvu sana kwa kweli.

MÊmENtO HoMO
 
Baki na msimamo wako.
Mwambie ukweli.

Mungu ni wa thamani kuliko kitu kingine chochote..kuwa na Yesu ni bora kuliko vyote.
Kuna vitu lazima uvipoteze kwa ajili ya Mungu.

Wakati mwingine kabla hujaingia kwenye mahusiano muulize kwanza Roho mtakatifu.
Tulia sikia sauti yake.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Asante Mama mchungaji.
 
Sasa si umwambie tu hutaki kudinywa steaight forward...

Kitendo cha kuweka uzi ni kama una mashaka na uamuzi uliokwisha ufanya moyoni, wataka kuipa nafasi akili nayo iamue...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom