Tatizo lenu mnashindwa kutofautisha akili, Elimu na Kwenda shule.
Akili mtu anazaliwa nayo. Hata asipopata fursa ya kwenda shule bado atajifunza vitu vya msingi katika maisha kulingana na mazingira aliyokuwa nayo na maisha yatasonga.
Elimu ni ufahamu juu ya jambo au nyanja fulani. Hii hupatikana kwa kufundishwa na kujifunza. Kupata elimu si lazima uende shule. Mtu yeyote mwenye akili na basic education: darasa la saba anaweza kujiendeleza ki elimu hata nje ya mfumo rasmi na akawa mtu makini sana.
Kwenda shule ni kupata fursa ya kujielimisha kupitia mfumo rasmi. Kutegemea na akili ya mtu, shule hadi degree, zina zalisha watu wa aina tatu
1. Watu wenye kukarili mambo. Hawa mara nyingi hawajui kitu kingine zaidi ya kukarili walichofundishwa. Watu hawa huwa na ufaulu wa kati na mara nyingi hata kazini ni watu wa kusubiri kuelekezwa kitu cha kufanya. Huweza kazi za routine zisizo hitaji kufikiri. Hawa watu ndo mara nyingi hupenda kujivunia vyeti (kwenda shule) ili kuficha udhaifu wao.
2. Watu wanao karili na kuelewa kidogo. Watu hawa huwa na ufaulu wa wastani. Huelewa mambo ya shule na kidogo mambo ya nje ya shule. Watu hawa wanaweza kufanya kazi za routine na zile zisizo za routine ila kwa usimamizi na maelekezo ya kila mara.
3. Kundi la mwisho ni watu wenye elimu. Hawa ni watu wenye akili na wamepata fursa za kula vidato. Huelewa mambo mengi maana hupenda kujisomea. Kazini huwa ma think tank..kupanga mikakati, mbinu na kuboresha utendaji. Hupenda na huweza kufanya kazi za akili na siyo routine. Wanaitwa knowledge workers.
Nadhani mtoa mada ni mtu kundi la kwanza. Hata namna alivyo wasilisha hoja yake inaonekana kabisa amekarili tu mambo fulani na kujiona ana elimu.
Uandishi wowote wa mtu aliye elimika huzingatia kanuni ya 4W1H. 4-W's ni What, Who, Why, When na H Moja ni How.
Siku zote unapoandika kwa kuzingatia kanuni hii...msomaji ataelewa na kuridhika na andiko lako bila kubaki na maswali mengi. Nawasilisha