Sitausahau usiku wa Ngwasuma nikiwa na pisi kali kutoka Arusha

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Nilipata demu nikiwa kijana kijana, tukatoka kwenda naye Ngwasuma, 2007 hiyo Ngwasuma wanapiga Makumbusho Village. Ukumbi ulikuwa unajaza sana, Ngwasuma walikuwa wanapendwa sana.

Watu walikuwa wakitoka Tunduma, Mwanza, Kahama etc kuja kuwaona Ngwasuma, hivyo ni lazima uingie ukumbini mapema ukitaka ukae.

Saa 1⅞ jioni niko na huyu binti Ngwasuma, nikaitisha mbuzi portions mbili na yeye chips na robo kuku, nikamwambia agiza nusu kuku akikushinda nitakusaidia.

Mezani nimelaza maji na konyagi kubwa, zamani ilikuwa ya chupa ya round, sio hili jibapa. Binti aliagiza Coca-Cola nne, ndani ya muda mfupi akawa amezifuta na kaagiza nyingine.

Hadi tunatoka mziki demu kazinywa koka na soda nyingine mchanganyiko zaidi ya 19, kisa hanywi pombe.
 
Itaendelea au imeisha?
 
Afya ya akili ni muhimu kwenye maisha
 
Sasa Buji hivi 2007 hadi mwaka huu si wa 5 na kasoro ya miezi kuwa miaka 6.


Hiyo Konyagi ya mviringo ilikuwaje mkuu...sababu bapa kwa ninavojua ni kitambo sana.


Mbula isyanaloli ndikulonda ubhutungulu nkulumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…