Sitosahau mara yangu ya kwanza kuingia Barbershop

Sitosahau mara yangu ya kwanza kuingia Barbershop

Nina visa kuhusu bei huwa nacheka sana nikivikumbuka.

Kuna siku nimeenda dar, 2016 nadhani. Sasa kuna mpwa wangu alikuwa UD pale, ilikuwa nionane naye. Ukienda mjini, mwanachuo lazima umtoe chochote. nikamwambia niko "kagame hotel, kwa kuwa wewe ni mwenyeji, njoo maeneo haya, then twende saloon ya jirani mandevu yamekua na kesho kuna watu naonana nao siwezi enda hivi".
"Poa bro, nami nataka nikanyoe"

Tumefika barbershop, dogo kaanza, baadae nikafata kwa kinyozi wa pili mimi. Sasa dogo akawahi maliza. Nikamuuliza jamaa mnanyolea sh. Akaniambia 5k. Kichwani nikajua 10 wote. Mfukoni nina kama 70 tu. Lengo dogo nimtoe 50. Nimeingia kule chemba, nikamwambia yule dada naosha tu.

Pembeni dogo, nasikia scrub ya steam sijui, mara massage ya kichwa, mara mba.. Nikajua hapa shughuli ipo.

Bill kuja 40. Nikuuliza kivipi, kale kadada, kunyoa 10, steamer 15, massage ya kichwa 10, mba 5. Ntafanyaje sasa nikalipa. Ila nilichukia vibaya sana.

Dogo nikampa twenty, nikamwambia rudi chuo kesho tutaonana.
 
Digo unaingia Barbershop na buku,unataka wakuoe?,[emoji23]
 
Khahahahah!
Kuna siku nikawa nimedaka kamkwanja flani hivi kadoogodogo.

Nikajisemea,kabla hakajaisha,ngoja na Mimi nikaoshe nyota.

Nikatungua kadent & katshet kamtoko
Mimi huyo🏃 Barbashop haiwezikani napita tu.

Nikazama ndichi,ebhanae kidogo kidogo nirudi nyuma nikajikaza kiume,maana nilikuta Sura kadhaa nzuri kinouma.
Nywele zangu Kama kawaida hazina mlolongo mzuri.

Karibisha yenyewe nikasema,ewaaaaaa hapahapa.

Mademu waliokuwa wawili vinyozi wawili,wateja Kama watatu.so more ndani kukawa c haba.

Store nyingi,na wakawa vinyoz wanawatania wale mademu mpaka nikasema,day Kuna watu wanafanya kazi mazingira mazuri,FURU rsha.

Zamu ikafika YANGU,mashine za kunyolea haziumiz hata kidogo,tofauti na kile pa siku zote unakutana na mashine utafikiri imetolewa JIKONI
,Nikamaliza,sikuwa na wasiwasi,nikaulizwa mekapu ipi nahitaji,nikasema iliyo quarity.
Sasa ebhanaeeeee!demu mkali ndo slikuwa anafanya hayo yote.
Si nilisema quarity,hee acha aanze kufinya uso wangu.

Aibu ya mwaka,uso wangu ulikuw unatoa vitu vyeupe Kama MAFINYO loh3!
Nikashtuka,in maana nimeoza au!.
Mbona sielewi elewi,kucheki watu mle ndani wanafatilia show inayoendelea kwangu.
Naiman vilivyotoka usoni kwangu vingejaa mfuniko wa chupa ya maji Kilimanjaro.

Nikapelekwa room ingine,kule hudma Kama kawa ya viwango,room ile ilikuwa kubwa kinyama.
Baadae ile pisi mautani Kama you're,kumbe bhana MDA wote msemaji was RUVU SHOOTING slikuwa amesimama Dede kwa ajili ya mahojiano.
Kulingana na Dada yule alivyokuwa akinishikashika,akaniambia,Kuna huduma extral Kama ntahitaji lakini.maana nilifanyiwa mpaka massage ya nusu mwili.

Alikuwa akifika karibu na kwa msemaji was Ruvushooting anakuwa Kama amejisahau anagusa kiutaalam.

Nikamwambia fresh,akasema day ni elfu 20000. Huduma ya extral.nikasema fresh.

Maana nilitaka nipewe huduma zote za pale.

Daaaaaaaah,duniani Raha Sana bhana.
Nikapiga bori Kama feisal shot la nje ya 18.
Wow.
Nilivotoka mule ndani,nikajisemea mmepata hell YANGU kubwa,Ila nami nimeinjoi.
Baada ya hapo,nilala njaa Kama siku 3 mpaka 4.
hapo kwenye kulala njaa uliyataka mwenyewe ndugu😹😹😂🤣
 
Khahahahah!
Kuna siku nikawa nimedaka kamkwanja flani hivi kadoogodogo.

Nikajisemea,kabla hakajaisha,ngoja na Mimi nikaoshe nyota.

Nikatungua kadent & katshet kamtoko
Mimi huyo[emoji125] Barbashop haiwezikani napita tu.

Nikazama ndichi,ebhanae kidogo kidogo nirudi nyuma nikajikaza kiume,maana nilikuta Sura kadhaa nzuri kinouma.
Nywele zangu Kama kawaida hazina mlolongo mzuri.

Karibisha yenyewe nikasema,ewaaaaaa hapahapa.

Mademu waliokuwa wawili vinyozi wawili,wateja Kama watatu.so more ndani kukawa c haba.

Store nyingi,na wakawa vinyoz wanawatania wale mademu mpaka nikasema,day Kuna watu wanafanya kazi mazingira mazuri,FURU rsha.

Zamu ikafika YANGU,mashine za kunyolea haziumiz hata kidogo,tofauti na kile pa siku zote unakutana na mashine utafikiri imetolewa JIKONI
,Nikamaliza,sikuwa na wasiwasi,nikaulizwa mekapu ipi nahitaji,nikasema iliyo quarity.
Sasa ebhanaeeeee!demu mkali ndo slikuwa anafanya hayo yote.
Si nilisema quarity,hee acha aanze kufinya uso wangu.

Aibu ya mwaka,uso wangu ulikuw unatoa vitu vyeupe Kama MAFINYO loh3!
Nikashtuka,in maana nimeoza au!.
Mbona sielewi elewi,kucheki watu mle ndani wanafatilia show inayoendelea kwangu.
Naiman vilivyotoka usoni kwangu vingejaa mfuniko wa chupa ya maji Kilimanjaro.

Nikapelekwa room ingine,kule hudma Kama kawa ya viwango,room ile ilikuwa kubwa kinyama.
Baadae ile pisi mautani Kama you're,kumbe bhana MDA wote msemaji was RUVU SHOOTING slikuwa amesimama Dede kwa ajili ya mahojiano.
Kulingana na Dada yule alivyokuwa akinishikashika,akaniambia,Kuna huduma extral Kama ntahitaji lakini.maana nilifanyiwa mpaka massage ya nusu mwili.

Alikuwa akifika karibu na kwa msemaji was Ruvushooting anakuwa Kama amejisahau anagusa kiutaalam.

Nikamwambia fresh,akasema day ni elfu 20000. Huduma ya extral.nikasema fresh.

Maana nilitaka nipewe huduma zote za pale.

Daaaaaaaah,duniani Raha Sana bhana.
Nikapiga bori Kama feisal shot la nje ya 18.
Wow.
Nilivotoka mule ndani,nikajisemea mmepata hell YANGU kubwa,Ila nami nimeinjoi.
Baada ya hapo,nilala njaa Kama siku 3 mpaka 4.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Pole sana Mkuu Atalanta 😂😂😂
Na Mimi nina kisa tofauti kidogo lakini hapo kwenye ishu ya bei ndio ninapo taka kupazungumzia. Kuna siku mwaka fulani nilikuwa nipo Zanzibar kikazi. Siku hiyo asubuhi mida ya saa 5 asubuhi nikawa nimefanya kazi ya haraka na nikaingiza kama 120k ni pale kwenye duka la sourvenir MEMORIES OF ZANZIBAR. Opposite ya hilo duka kuna mgahawa unaitwa Tanzanite nikazama mule ndani chap chap nikaisoma MENU nikaagiza Msosi hata siujui 😂😂😂ilikuwa ni BUTTERNAN something like that. Sasa kwa mawazo yangu nikadhani itakuwa ni kama Cheese / Bread au kitu chochote kinacho fanania kumbe hiyo BUTTERNAN ni Chapati kavu kabisa haina mafuta wala Chumvi yaani kama unakula Sacrament ya Kanisani ile. Hiyo BUTTERNAN ilivyoletwa nikaletewa na Kibirika cha Chai ya Karafuu imechanganywa Mdalasani na kikopo cha asali ili kuiunga hiyo Chai. Sasa ishu imekuja kwenye Bill yaani ilinitoka 30,000 kizembe sana hasa ile Chapati isiyokuwa na Chumvi wala haijachomwa kwa mafuta yaani roho iliniuma sana... 🤣🤣🤣
Lakini siku zote kosa sio kosa lakini kurudia same mistake ndio mistake.
😅😅😅
Butternan ni kavu sana tena ukitaka ujue ukavu wake acha ipoe kabisa inakauka ile Kauka kiasi unaweza kumpiga nayo mtu akazimia.
Huwa wanakuja nayo hawa waarabu wa dpw nawaambia rudi nayo tu sili.
Waambie garlic butter nan next time,
Hiyo hatakuangusha,wakitoa jikoni lazima waipake siagi ya kitunguu swaumu inakua lainii mda wote na taste yake balaa.
Ule ikiwa moto.
 
Pole sana Mkuu Atalanta 😂😂😂
Na Mimi nina kisa tofauti kidogo lakini hapo kwenye ishu ya bei ndio ninapo taka kupazungumzia. Kuna siku mwaka fulani nilikuwa nipo Zanzibar kikazi. Siku hiyo asubuhi mida ya saa 5 asubuhi nikawa nimefanya kazi ya haraka na nikaingiza kama 120k ni pale kwenye duka la sourvenir MEMORIES OF ZANZIBAR. Opposite ya hilo duka kuna mgahawa unaitwa Tanzanite nikazama mule ndani chap chap nikaisoma MENU nikaagiza Msosi hata siujui 😂😂😂ilikuwa ni BUTTERNAN something like that. Sasa kwa mawazo yangu nikadhani itakuwa ni kama Cheese / Bread au kitu chochote kinacho fanania kumbe hiyo BUTTERNAN ni Chapati kavu kabisa haina mafuta wala Chumvi yaani kama unakula Sacrament ya Kanisani ile. Hiyo BUTTERNAN ilivyoletwa nikaletewa na Kibirika cha Chai ya Karafuu imechanganywa Mdalasani na kikopo cha asali ili kuiunga hiyo Chai. Sasa ishu imekuja kwenye Bill yaani ilinitoka 30,000 kizembe sana hasa ile Chapati isiyokuwa na Chumvi wala haijachomwa kwa mafuta yaani roho iliniuma sana... 🤣🤣🤣
Lakini siku zote kosa sio kosa lakini kurudia same mistake ndio mistake.
Hiyo kitu Wana penda kula wahindi na waarabu baadhi 🤣😃.
👉Iko expensive Kutokana na sehemu🤣😃, pimbi wewe Manyanza
 
MUENDELEZO
yule mdada Asha akakiminya wapi sijui kile kiti kikawa kinalala Basi kinarudi nyuma taratiiibu "Yaani Kama kina lala hivi" Mara baada ya muda kidogo kikakaa sawa Ila kwa dizain ya kulala hivohivo. Wakati nikiwa bado nipo kwenye kile kiti nikaona Asha akafungua koki ya maji pale pale pembeni kulikua na Kama ka sink hivi kadogo alipofungua Ile koki ya kwanza nikahisi Yale maji yaliyotoka yalikua ni ya motomto nilihisi hivyo kwasababu alijiosha mikono yake afu wakati wa kujifuta ndio yakanirukia kidogo baada ya hapo akafungua koki nyingine tenah hapo yakatoka ya baridi nayo pia niliyahisi kwa stail Ile Ile akafungua tenah koki ya tatu hapo sikuona kilichotoka sababu mawazo yangu yakarudi tenah kufikiria bei tu Yaani kichwa kikawa kinawaka Moto kwa kuwaza bei ya pale Sasa ukijumlisha na Asha alipokua akafungua zile koki Yaani ndio akawa ananitoa kwenye reli kabisa.

Baada ya muda Asha akaniuliza kua natumia Sabuni au rosheni gani..?? aah mtihani mwingine huuu kwangu me home nishazoea Sabuni ninayotumia Ni TAKASA "kipindi kile zilikuwepo sijui Kam bado zipo Hadi saiz" Tena na yenyewe sio kwamba hiyo Ni spesho kwa kuogea aah hapana Kama nataka kwenda kuoga nabeba ntakayoiona unakuta Sabuni hiyo hiyo Ni yakuogea tena hiyo hiyo ya kuoshea vyombo Sasa hapa eti naulizwa unatumia Sabuni gani nijibu nini Sasa.Nikamwambia em tuone Sabuni ulizonazo hapa Basi nikaangalia sikuona hata TAKASA yangu Wala inayoendana na TAKASA haikuwepo pale, ilibaki kidogo nimuulize kua Kama anasabuni ya magadi nikaona mmh hapa ntaonekana mshamba Zaidi. Ikabidi nimwambie we nipake yoyote Ile ambayo haitoi vipele. Akachukua Sabuni gani sijui Ile me siifaham akanza kunipaka aisee yule mdada anamikono milaini nyieee sijapata ona Basi na ushamba wangu huu naoshwa usoni na kichwani lakini chaajabu kichwa chini kikawa kinahangaika Yaani sikuile ilikua ni tabu tupu. Jamani jamani Kuna wadada wanajua kuongea yule mdada "Asha" alikua anaongea taratiiibu Ila kadri ninavyoisikia sauti yake nilikua nazidi kusisimka daah nyie acheni tu, Chaajabu Sasa ukiniuliza alikua anaongea nini sikumbukk hata kimoja Ila napenda tu kusikia vyenye alivyokua anaongea. Akawa anachukua sijui vitu gani Mara ajipake mkononi afu anipake usoni Mara anifute na kitambaa lain, akawa ananipaka hiki ananisafisha. Kusema ukweli sikutamani nitoke kwenye kile chumba kwa wakati huu nilikua najiona Kama nipo kwenye ulimwengu mwingine kabisa yaan nilikua nasikia raha tu kua na yule mdada mule ndani.

Baada ya muda kidogo nikaona ngoja nimuulize Asha bei ya kunyoa hapa Ni shingapi. samahani sister hivi bei ya kunyoa hapa Ni shilingi ngapi kwani..?? Yule mdada akawa Kama ananishangaa hivi baada ya kunijibu akaniambia kwani hawajakwambia bro ni shingapi. Nikamwambia hapana hawajaniambia akasema usijar bei ya hapa Ni ya kawaida sana. Sasa nikawa nimechoshwa na majibu yao Yale nikawa nimetulia tu.Nikawa nimemaliza kunyolewa Sasa nikaanza kujifikiria kuhusu bei akili ikawa inaniambia kabisa kua hapa piga ua garagaza hapawezi kua pa buku. Nikamfata kinyozi mmoja "Emma" sababu niliona kidogo yeye ndio Kama nimezoeana nae kwa muda ule mfupi. Yule broo Emma alivyoniona tu nimetoka kunyoa akaniulize dogo umeonaje huduma. Nikamjibu huduma ni nzuri tu brooh, wakati naongea nae hapo pia alikua anamnyoa mtu mwingine yule Big alikua kwenye kiti kingine akinyolewa na yule jamaa mwingine. Nikaona hapa ili kujua bei nisiulize kwa sauti kubwa nisije haribu Basi nikamsogelea yule brooh Emma karibu afu nikamuulize sorry brooh gharama yake ni kiasi gani. Emma akanijibu dogo gharama yake siyo kubwa Ni teni tu. aisee nilitoa macho achaa Nikamuuliza Tena taratibu "umesema shingapi broo" safari hii hakujibu yeye akajibu yule big "dogo si umeshaambiwa ten au hujui kiingereza okay bei yake ni Elfu kumi nimekufafanulia Sasa". Nikashangaa huyu Big vipi nae me naongea na Emma afu yeye ananijibu. Nikaona isiwe kesi nikamwambia Emma "brooh naomba tuongee maramoja tafadhari" yule Big akajibu tena muongee nini dogo we TOA hela Kama huna acha viatu hivyo aisee nilijuta kwenda pale mbona. Nikabaki najiwazia moyoni Sasa hapa hata Kama nikaomba anipunguzie bei kutoka elfu kumi Hadi buku hivi atanielewa kweli..??. Nikaona hapa lazima niache kitu hapa usikute atasema niache viatu kweli Ila daah na Mimi kwanini niliingia hapa Sasa.

Ninachoshukuru Mungu yule Emma alikua anaonekana ni mcheshi Sana afu alikua akitabasamu tu muda wote wakati naongea nae Sasa nikaona hapahapa ndio pa kujichukulia point. Nikamwambia Tena taratibu "broo samahani naomba nipunguzie bei bas" akanigeukia afu akaniambia dogo bei ya kunyoa ndio hiyo hiyo hua hatupunguzi ndio maana tukaamua kuweka bei ndogo hivyo. Moyoni nikawa najisemea elfu kumi ni bei ndogo kweli..?? Yaani hela ambayo Mimi natumia kwenye msos siku tatu kwa bajeti yangu afu wao wanasema eti ni ndogo, Nikasema daah bora ningenyoa na wembe tu Hostel . Emma akaniuliza kwani wewe unashingapi nikaganda nafikiria maana nilikua naogopa hata kutaja hela niliyonayo nikabaki namuangalia tu kwa sura ya huruma. Dogo usitie huruma mjini hapa hakuna wa kumdekea aliongea Big, alikua ananiona kupitia kioo Cha mbele Cha mle saloon. Emma Akasema Basi subiri hapo nimmalizie kumtoa huyu afu tutaongea nikaona hapa saloon inaonekana kunakuwaga na watu wengi hapa unaweza kuta katoka huyu akaja mwingine nikaona Bora niwe muwazi tu. Nikamwambia samahani brooh Mimi ninahela ndogo nilikua sijui bei yake kweli tena. akaniambia usijari dogo hela ndogo Ni shilingi ngapi hiyo kwani elfu Tano au, daah nikabaki namkodolea mimacho tu afu nikatikisa kichwa kukataa hiyo hela aliyoitaja yeye. akasema Sasa una kiasigani dogo nikamwambia nina buku. Buku !!! aisee yule Big alishangaa nyieee akasema Emma huyu dogo anakufanyia masihara bhana haiwezekani afu we dogo kwani Ni wa wapi wew nikamwambia me natokea morogoro akasema morogoro mbona wajanja afu we inaonekana mshamba mshamba wewe Ni wa morogoro kweli wewe.

Nikajisemea tena moyoni eeh Mungu nisaidie nisionekane tapeli tu me nitoke salama hapa. Hamna broo sema me natokea ndani ndani kidogo nikaamua kumjibu hivyo. Ndani ndani wapi huko nae akaniuliza nikamwambia natokea Euga akasema duuh huko nako ni morogoro nikamjibu ndio. Emma malizana na mtu wako bhana akasema yule Big. Me nikajua ananilipia alivyokua ananiuliza maswali vile Sasa et nae anamwambia tenah Emma amalizane na Mimi daah . Naomba nisaidie brooh nikaamua kuanzisha Tena mazungumzo Sasa Mimi nakusaidijae hapo mdogo wangu labda angalau Kama ungekua na elfu Tano Mimi ningekuelewa Sasa wewe dogo una buku hata Kama wewe ungekua Mimi ungefanyaje hapo eeh afu kingine dogo humu siko peke yangu nipo na wenzangu nao pia tunagawana pesa Sasa vipi Kama Mimi nilichukua hiyo buku yako wao watanielewa ?

Nikaona kweli kabisa jamaa kaongea sawa lakini na Mimi hiyo 10k Sina nikafikiria nikamgeukia yule Big nikamwambia broo naomba nisaidie samahani Mimi nilikua sijui bei ya hapa Ila Kama ningekua naijua nisinge hata Sogea. Yule Big akanikata jicho afu akaniambia dogo mbona msumbufu wewe afu mbeya umekuja kwa Nani yako kwanza tuanzie hapo nikamjibu nimekuja chuo kusoma. Yaani mitoto mwingine Ni mipumbafu kabisa Sasa wewe msomi mzima ulifikiri bei ya kunyoa hapa Ni buku ivi kweli !! wewe lipa tu ili sikunyingine ujifunze nikamwambia samahani brooh nimejifunza tayar nilikua siifaham kweli Tena yule Big akaniangalia afu akasema sikunyingine usirudie tena utatolewa kizuri Mbeya imebadilika sikuhizi sawa, nikamwambia sawa shukrani brooh nashukuru sana. Sasa unashukuru Nini akaniambia yule big nikamjibu nashukuru unanilipia akasema haaa wew dogo Nani kasema nakulipia dogo vipi wewe. Nikaona Sasa hapa naumbuka mtu mzima nikarudi kukaa kwenye sofa pale safari hii sikuona hata Kama lile sofa Ni laini niliona hakauna tofauti yoyote Kati ya sofa na benchi la kawaida na hii Ni sababu ya mawazo niliyonayo .

wakati nimekaa pale nafikilia nikaona yule Big akaniambia dogo nenda kasome ntakulipia Daah Kama sikusikia vizuri nikamuangalia Tena yule big. Unashangaa Nini dogo wewe nenda me ntakulipia aisee nilimshukuru Sana yule Big siku hiyo.

Tangu siku hiyo sijawah kurudi Tena pale saloon Kuna kipindi nilitaka niende hata niwape hai hasa hasa yule kinyozi Emma lakini sikufanya hivyo.
Kali sana, BONGE MOJA LA COMEDY
 
Umenifurahisha.Umenikumbusha mara ya kwanza kutumia tea bag tena hotelini .Kata kamba kwenye kikombe nikakatoboa na meno nikamimina kwenye kikombe.Wenyeji wangu wakabaki wamepigwa na butwaa.Ushamba mzigo.
Nimecheka kwa sauti aisee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
IMG_0992.jpg
 
Back
Top Bottom