Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Nimeepuka sana kutembeza rungu kwa Ke wa vyuo zaidi ya vitatu.

Wake za Watu na wanafunzi sijawahi kabisa kujamiiana nao.

Namshukuru Mungu kwa neema hii maana si kwa ujanja wangu, Mungu naomba anisaidie niendelee kutembea na biti hili hili maisha yangu yote, Amina.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Wachina wanatibu kisukari nimeshuhudia Rafiki yangu aliyeugua kisukari kwa zaidi ya miaka miwili bila tiba ila aliporejeshwa kwenye hospital ya Wachina Dar alipona mazima na haumwi tena kisukari.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
una maanisha wenye ukimwi ni wale waliomdhihaki Mungu
Mungu huwa ni mlinzi wa watakatifu Wake, so ukiwa unamcha Mungu huku we ni Mnafki wa ndoa kwa kuendekeza uzinzi na uasherati ilihali mwenzi wako yu mwaminifu katika ndoa Mungu atakuadhibu wewe mwenyewe na hilo janga wala si mwenzi wako.

Zaburi 34:7.

Malaika wa BWANA hufanya kituo,
Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.

Zaburi 127:1.

BWANA asipoijenga nyumba
Waijengao wafanya kazi bure.
BWANA asipoulinda mji
Yeye aulindaye akesha bure.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Uzi mzuri sana. Ninae ndugu mmoja tunamuuguza. Naona the effect of cheap sex. Anaumwa sana, anahuzunisha mno. Mbaya zaidi hana stability kiuchumi, kimaisha. Naweza sema 'alidanga' bila faida. Leo mambo mengi aliyofanya in the past, yanamback fire. Enzi zake alikuaga pisi kali haswa. Alikula starehe za kila namna. Lakin kweli mchuma janga hula na nduguze. Leo tunakoma kwa janga lililochumwa na huyu mtu.

Anyways, it is what it is. Kwetu wake kwa waume, yes sex is addictive, enjoyable and unexplainable..lakini kupitia wewe mume ama mke, unaweza ukaiangamiza familia. Be careful of the choices you make. Kuwa responsible kwa familia uliyokubali kwa ridhaa yako kuianzisha. Ukiumwa atakayeuguza, atakaeteseka ni your spouse. Mbaya sana mwenzako katulia na wewe ndo unakuwa ticket ya kumuangamiza ama kumuua. Kazi kwetu tuliobaki hapa duniani.
 
Katika vitu ambavyo nimejiandaa kisaikolojia kuvipokea basi ni ukimwi.
Maana wife ana trip nyingi sana kikazi mikoani yaani hapo kuchepuka ni akili yake tu atumie condom au laah.
Nimejikuta nakuonea huruma sana mkuu.Kitendo cha mkeo kuwa na trip daily ina leta confussion sana.Mara nying hata stability ya family huwa inakua at jeopardy sana
 
Kuna Mwalimu mmoja pale UD kwenye kota za Walimu alikuwa anakula kuku na mayai yake.

Alibahatika kupata Mabinti mapacha na walipoanza kupevuka tu aliwatenganisha kila mmoja kulala kwenye chumba chake, kumbe Lizee lilikuwa linakula zamu kwa zamu kwa hao Mabinti zake mbali na Mkewe.

"Mficha maradhi kifo humuumbua" hatimaye Doto alipata mimba, Mama Mzazi alipoona tu dalili zote ilibidi ambane Bintiye kwa maswali mengi kutaka majibu ya aliyemsababishia ujauzito, ingawa Binti alijitahidi sana kuficha ila mwishowe ilibidi amtaje Baba yake Mzazi ndiye mwenye ujauzito huo.

Mama akapandwa na presha ya ghafla ila alipomwambia Mumewe alikataa kata kata, Doto alianza kliniki na ndipo ilipobainika ana umeme alipokuwa anakaribia kujifungua, Kulwa naye ilibidi akapime baada ya kujua Mdogo wake Doto ana umeme halikadhalika naye alikutwa kaukwaa umeme. Mama Mzazi aliposikia hizo habari za umeme kwa Binti zake alipandwa na presha kubwa hadi kuzidiwa hatimaye Baba ilibidi atoroke kabisa home kujitenga na maswahibu hayo.

Mama Mzazi alifariki kwa presha, Baba Mzazi alichanganyikiwa naye hakukaa zaidi ya miaka miwili akavuta, Watoto mapacha walibaki Yatima wakiendelea kuishi kwa matumaini.

Dunia hadaa walimwengu Shujaa [emoji25]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Hii issue nikikua early 90s hasa hasa hii miaka miwili 1998/2000 nakumbuka kusikiliza kwenye taarifa ya habari RTD (TBC ya sasa) kwamba moja ya wilaya za Tanzania kuzungushiwa utepe mwekundu kutokana na kuongoza kwa vifo vilivyotokana na HIV/AIDS,nahisi ni hii hii Mafinga.

Pole sana hauko peke yako,hakuna Tanzania hii aliyekwepa hili zimwi iwe ni kwa wajomba,shangazi,baba wadogo etc mimi niliwahi zika mpaka babu yangu mdogo 2007 na mwanae alizikwa 1997 kisababishi kikiwa huu huu  UKIMWI na mzee alikuwa na jeuri yule aliambiwa atumie ARVs akakataa akasema kama alivyokuwa anafurahia utamu anataka kuuona uchungu nao unafananaje,alikufa mzee aged 70.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…