Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Mwaka 2013 nikiwa katika shughuli za shirika moja hivi tulienda kikazi wilaya moja hivi, kanda ya ziwa.Kuna kijiji tulikuta nyumba kali lakini hakuna watu wanaoishi na wenyeji walituambia ukimwi ulifanya tamasha kakita familia miaka ile
Duuh
 
Dah Ujumbe wako unahuzunisha sana lakini unatupa funzo. Tunapaswa kua waangalifu sana janga bado lipo na linaondoka na waja taratibu. hakuna aliye salama.

Hiyo kitu imekula sana watu, Kagera, Iringa hasa mafinga, makambako na njombe. Mbeya, tunduma, Rungwe pia wameondoka wengi. Sina hakika lakini kuna ishara kuwa kutofanya tohara, hali ya hewa ya baridi kali, na wadau wa huko kuwa na maumbile manene pamoja ya .... na desire kubwa ya kufanya tendo ni sababu kuu ya maeneo hayo kuathirika zaidi.

Pale dodoma kuna Ukoo ulikuwa unaitwa Masimba: Walikuwa wanafanya ufuska wa kupindukia wa ndugu kwa ndugu, Inasemekana HIV imewaondoa wote kijiji kimebaki maghofu.

Hata Dar nayo ni mwathirika mkubwa. Sample; kuna Bendi maarufu nchini; HIV iliondoka na Wanamuziki wake wote hadi wabeba ngoma. Pia, ukichukua wasanii wakubwa nchini ni wachache sana wameweza vuka miaka 55, wengi uondoka mapema kutokana na hilo janga ingawa huwa atuambiani ukweli.

Siku hizi, HIV inaua kupitia kisukari, kufeli kwa Ini, figo na moya n.k.

Asante kwa kutukumbusha. hakuna aliye salama bila kudra za mungu na kuchukua taadhari hatuwezi
 
Nakumbuka 2001 kuingia 2002 kuna dada tulikuwa tunasali naye kipindi hicho huko nyumbani kanda ya ziwa. Dada alikuwa mzuri sana pisi ya kwenda sema ndo ivo alikuwa hajatulia kudanga kwa sana route kama zote. Ww si akaja kanya waya, nakumbuka bado nilikuwa mdogo but namkumbuka vzuri. Akaanza kuugua mdogo mdogo zinapita week hata 2 haji kanisani siku akija full kulala lala tu mara atoke nje kuota jua wakati joto kali mcha yeye baridi haliishi. Mwisho wa siku habari zikasambaa mtaani kuwa dada kauvagaa. Ikifikia kipindi hawezi kutoka ndani kanisani hatokei tena nikaja kumuona siku moja nahisi ndo ilikuwa siku yake ya mwisho kuja kanisani maana aliletwa kanisani kwny baiskel na kaka yake. Dada kaisha kawa kama mtt mdogo nywele zimenyonyoka nyepesi mdomo kama kapaka unga dalili zote unaziona kabisa hazijifichi.
Tokea hapo sikumuona kuja tena kanisani hata mataani, akawa wa kulala ndani tu kila kitu kitandani hata chooni hawezi kwenda ilikuwa balaa siku tukaenda kumsalimia yaani kitandani huoni mtu mtu unasikia sauti tu halafu kipindi hicho walikuwa wanakuwa wakali balaa. Mwaka 2002 kama sikosei dada wa watu akaumaliza mwendo. Jamani UKIMWI wa miaka ya 2000 ilikuwa ni balaa. Mtu unakonda unabaki kichwa tu nywele zinaisha kichwani, mdomo unapauka, majipu hayakuishi, kuharisha ndo usiseme. Waliopata HIV kipindi hicho waliteseka sana.
#WatchOutHIVisReal.
Kwa miaka hiyo, kama sijakosea nahisi hapa palikuwa Bunda Mtaa uliyopo jirani na Posta barabara inayoshuka stand mpya kama unatoka Musoma.
Mama wa Binti huyo alikuwa Mwalimu.
 
Na hamna watu wako kwenye hatari ya maambukizi Kama watu walio kwenye serious relationship....Maana mnaaminiana,hakuna Tena condom baina yenu,kwa hiyo mmoja akichomoka akaleta kila mmoja anajifanya hajui umetokea wapi...ndio Maana unashangaa wale malaya hawana maambukizi Maana hamna mtu anamuamini kila akipiga nae anavaa protection
Shabgazi umemwaga ukweli mtupu
 
Hizo ndio unapata mawenge. Hapa ni mazoezi maji mengi, kula vizuri na kuendelea kugegeda tuu na kutokuwa n mke. Maana mke anakuletea stress na huu ugonjwa hautakiwi uwe na stress
Piga dawa uongeze umri, kuna binamu yangu nae kagomea kabisa dawa hataki kusikia....cha ajabu hata apetite huwa hana sio mlaji hivo anakomaa tu na zoezi na anapiga chuma ukimuona sio rahisi kujua.

Sasa hapigi dawa ila anakula mizigo tena anapenda mizigo yenye mawowowo
 
UKIMWI ni hatari nilishuhudia kwa macho yangu ndugu yangu akipofuka macho asubuhi wakati dada yake akiwa anajiandaa kumwamsha kumpatia chakula. Daah ilikua Mwaka 2009 aisee sitakaa nisahau alivyokua akilia kwa uchungu kwamba haoni tena na hata kaa aone kipindi kile nilkua bado mdogo hadi machozi yalinitoka R.I.P aunt naweza kusema japo kuna magonjwa mdngine mabaya kma Saratan na Sukar ila UKIMWI upewe maua yake

Pia 2016 na 2017 nikashudia UKIMWI ulivyowapiga vibaya watu wangu wa karibu wakaangamia na kuacha watoto wadogo ambapo mtoto mmoja kati ya hao naishi nae kila siku ananiuliza mama atarudi namwambia atarudi siku moja ndio hivyo ni Simanzi tu.

Lakini na ushahidi na mtu mmoja yuko nao sasa kwa zaidi ya miaka 31 naweza sema vitu vingine ni Imani tu! Maana ni mtu anayemjua Mungu Kwelikweli na anatumia dawa ni mtu mzima sana na amefanikiwa kimaisha hata kaajiri watu wengi kwenye kampuni zake ambayo ni NG'Os ya kusaidia waathirika hyu kwa story nilizosikia kwa wazazi wangu Ngoma aliletewa na marehem mumewe na iliyomuua mume wake ni mkanda wa Jeshi na mme wake ali confess mbele yake na kwa wasimamizi wa ndoa yao ambao ni wazazi wangu siku ya kufa kwake kuwa aliupata baada ya kutoka na Secretary wake.

Tuwe makini Waungwana Ngoma is really aisee!Kimasihara so poa utamenya kimasihara na wewe utamenywa kimasihara.
Ngoma hatari sana.. ila kwa siku hizi sukari hatari sana ×100.. nishiaona inampofua mtu kijana tu mixer mwingine imemkata mguu.. ukijikwaa tu ukapata kidonda kwenye kidole inaweza ikawa mguu ndio ntolee hio..
 
Back
Top Bottom