Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Kijijini kwetu ulifyeka kijiji kizima, wamebaki watu wachache sana, nyumba ni nyingi kuliko watu.
Vijana kutoka mikoa mingine wanajikalia bure kwenye nyumba zilizoachwa
Mnatakiwa information km hizi ziwekwe kwa uwazi na kutaja mtaa au Kijiji husika unaweza kuongeza awareness wengi hudhani taarifa zisizokuwa detailed ni chai humu

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Nina Aunt yangu anaishi nao huu ugonjwa sasa akismbiwa aende Hospital akapate ARV's hataki eti kaokoka na nabii wao kawaaminisha kuwa ukimwi hauwezi muua saivi kakonda balaa.
Huwa hawataki kutumia dawa. Usihangaike na counseling tumia nguvu za mwili. Kamata weka ktk gari peleka hospital. Iko hivyo.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Umekaa mitaa choka sana sisi tulifikia mtaa unaitwa pipeline ndo kulikuwa uzunguni nyumba zina angalizika kwa mbali mwaka 96 nyumba nzuri kidogo na vihela kiukweli vilikuwepo tulitoka navyo dar vya uamisho wa maza tukapanga pipeline

baadae ndo tukamia huo mtaa wa mikosi wenye jina la herufi tu 2003...... mtaa wa kishua sana miaka hiyo ndo majanga yalipo anzia ... na kwanini nilijua majirani zetu wanakufa kwa ukimwi mama angu alikuwa nurse so alikuwa anapiga story tunasikiliza pia alikuwa anawauguza wakiwa hoi pale mafinga hospital...

pamoja na u unurse wake ukimwi ulikuja kum bamiza RIP my mumy...sitosahau ulivyoniangalia those dying eyes my god niliumia mara mwisho na kuniambia napenda harufu(perfume nilipaka) yako mwanangu nikasema bye ukajibu bye ndo maongezi yetu ya mwisho i will always love you ...leo naandika haya tribute yako pia kuwaasa wengine.... nikapanda basi la abc kurudi dar nikijua sito kuona tena ..kweli baada week tatu kaka angu alinipigia simu kusema mama is no more....

Tulificha kifo cha kusema kafa tu kwa presha ila ilikuwa AIDS .... hata wanangu nitakuja kuwasilimua hii story ya ule mtaa na hakuna hata sehemu.nimedanganya wala kusingizia maana maza alikuwa nurse so alijua hali za watu wengi wakilazwa

Mbaya zaidi mwaka 99 waliweka hodi maalumu la watu wa HIV so ukiwa huna hela afu una ukimwi unasekwa huko nadhani ile hodi walikuja kuivunja kuondoa unyanyapaaa ilikuwa chini kabisa kule

Nimesimulia story asilimia 5% tano tu ya majanga nilishuhudia mafinga why niliyajua mengi nilikuwa mtoto wa nurse tena mtoto pendwa.....

Asanteni wadau uzi wangu umesomwa na watu wengi naamini umetoa elimu kubwa kuhusu hili gonjwa ..

Wengine wanasema bora ukimwi kuliko kansa...ni hivi ukiwa na ukimwi hata kansa unapata kiu rahisi mno yaani ukimwi ni kama boss la magonjwa yote linapiga simu moja kansa njoo mara moja inakuja....likiamua kumwite chawa wake TB fasta tu.... bado kijana wake mkanda jeshi

Ukimwi ni boss wa magonjwa ukiamua inaweza sema basi tumvuruge awe kichaa unakuwa kichaa madaktar wanajua hili yaani ninaposema UKIMWI ni boss la magonjwa yote namaanisha linaweza sema tuletee vidonda tu utapata hadi ufe

Hizo kansa kwa watu wenye ukimwi ndo nyumbani maana boss wao ukimwi si anakuwepo ndani utashangaa unapata kidonda hakiponi then kansa

AIDS SIO MCHEZO
Kwanini unaficha huo huo mtaa? Kila saa unaandika herufi moja herufi moja! Weka wazi nani anakujua hapa? Na hata akikujua yadhuru nini? Hapa unaweza kuongeza awareness just tu kuutaja na huo mtaa.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Wewe umeongea kitu cha msingi ambacho watu wengi hawakielewi.

Wanadhani eti virusi vinapitia ktk michubuko ya uume kwa nje tu. Wakati kumbe virusi vinapita kwenye ngozi laini ya ndani ya tundu la uume (Epithelium cells). Hizo cells ndo zina receptors nyingi za wadudu wa HIV kuliko hata lingozi la nje
Hii elimu ya hii issue watu wengi hatuna. Nafkiri Kuna haja ya kutoa elimu kama hii ki usahihi. Nafkiri semina za ukimwi nyingi zinafanywa na watu ambao siyo medical practioners. Kwa mfano pamoja na kuhudhuria au kusikia elimu ya ukimwi lakini sikuwahi kusikia hili.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Mwanangu natetemeka hapa, naogopa mzee maana nami nishauguza na kuzika ndugu si chini ya wanne kwa huu ugonjwa...
Nikikumbuka zamani nilikua makini saana hata nikaamua kuoa mapema na kua muamifu ila ndoa ilipovunjika nimeingiwa na roho ya uhuni balaa tena mbaya zaidi siwezi kutumia mpira....
Naogopa kesho yangu namuomba Mungu anasaidie hii roho ya umalaya initoke maana nikijikaza wiki mpaka natetemeka nahisi homa na akili inavurugika sijui n nini hata... enhh Mola nisaidie....😥😥😥😥
Okoka ndugu, hiyo ndio pona yako ilipo.
 
Sijasema mimi kwamba wameletwa kwa ajili ya kusambaza ,mimi nachojua kwamba kuna "WATOTO WA MAMA SALMA" vyuoni wamejaa TELE na hata ROMA alishawahi kuimba na kuwahasa wanafunzi wawe makini na "WATOTO WA MAMA SALMA" ,UDSM nakumbuka kulikuwa na FUSP na pia kuna tetesi jamaa mmoja alikuwa anasema kwamba kuna Demu ana ngoma na yeye alikuwa FUSP.(Female Undergraduate Scholarship Program).
Kwa waliosoma vyuo vikuu wanaelewa rate ya maambukizi ilivyo kulingana na mahusiano holela ya vyuoni. Ukitaka story ya rate ya maambukizi vyuoni jenga urafiki na wauguzi wa kike wa hospital za vyuo. Huwa hawana kuficha ficha wanakwambia hali halisi ilivyo. Wewe ndo uamue mwenyewe.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Ila kuna kitu kimefichwa kwenye AIDS ikitokea kwenye familia mmoja akaupata trust me lazima na wenzie aidha Wawili Au watatu watapata,ni kitu kama laana hivi but anyway naendelea na tafiti
I think ni no mawazo yako tuu. Ukimwi siyo ugonjwa wa vizalia. Uambukizeaji wake haufati mtiriko wa familia unless wewe ujichanganye mwenyewe.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Kwa waliosoma vyuo vikuu wanaelewa rate ya maambukizi ilivyo kulingana na mahusiano holela ya vyuoni. Ukitaka story ya rate ya maambukizi vyuoni jenga urafiki na wauguzi wa kike wa hospital za vyuo. Huwa hawana kuficha ficha wanakwambia hali halisi ilivyo. Wewe ndo uamue mwenyewe.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app

Mavyuoni ni hatari ,ndiyo wapo moto kila kitu wanataka kujaribu hivyo wanaungua sana.
 
Kwa mujibu wa baiolojia ya kidato cha pili che; virusi (vikiwemo vya UKIMWI) vina sifa zote za viumbe hai na visivyo hai.

Kwahiyo; kinapokuwa nje ya seli hai kinakuwa inactive (dormant) punde tu kinapopata access ya kuwa kwenye seli hai kinaanza kuishi.

Haya mambo magumu sana kuyaelewa! [emoji16]
Lakini nafkiri virus ana limitations ktk kusurvive kwake akiwa nje ya mazingira fulani hasa ya damu au majimaji fulani. Nikifikiria vifaa vya saluni jinsi vinavyotunzwa. Halafu kuna ile bandika bandua ya kutumia mashine moja ya saluni nahisi wanaume wengi tungekuwa waathirika.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Mavyuoni ni hatari ,ndiyo wapo moto kila kitu wanataka kujaribu hivyo wanaungua sana.
Nimeona jamaa anabisha concept ya watoto wa mama Salma. Lakini hiyo issue tulisikia sana miaka ya 2010s. Labda hiyo program ilishaisha lakini hicho kitu kilikuwepo.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Umekaa mitaa choka sana sisi tulifikia mtaa unaitwa pipeline ndo kulikuwa uzunguni nyumba zina angalizika kwa mbali mwaka 96 nyumba nzuri kidogo na vihela kiukweli vilikuwepo tulitoka navyo dar vya uamisho wa maza tukapanga pipeline

baadae ndo tukamia huo mtaa wa mikosi wenye jina la herufi tu 2003...... mtaa wa kishua sana miaka hiyo ndo majanga yalipo anzia ... na kwanini nilijua majirani zetu wanakufa kwa ukimwi mama angu alikuwa nurse so alikuwa anapiga story tunasikiliza pia alikuwa anawauguza wakiwa hoi pale mafinga hospital...

pamoja na u unurse wake ukimwi ulikuja kum bamiza RIP my mumy...sitosahau ulivyoniangalia those dying eyes my god niliumia mara mwisho na kuniambia napenda harufu(perfume nilipaka) yako mwanangu nikasema bye ukajibu bye ndo maongezi yetu ya mwisho i will always love you ...leo naandika haya tribute yako pia kuwaasa wengine.... nikapanda basi la abc kurudi dar nikijua sito kuona tena ..kweli baada week tatu kaka angu alinipigia simu kusema mama is no more....

Tulificha kifo cha kusema kafa tu kwa presha ila ilikuwa AIDS .... hata wanangu nitakuja kuwasilimua hii story ya ule mtaa na hakuna hata sehemu.nimedanganya wala kusingizia maana maza alikuwa nurse so alijua hali za watu wengi wakilazwa

Mbaya zaidi mwaka 99 waliweka hodi maalumu la watu wa HIV so ukiwa huna hela afu una ukimwi unasekwa huko nadhani ile hodi walikuja kuivunja kuondoa unyanyapaaa ilikuwa chini kabisa kule

Nimesimulia story asilimia 5% tano tu ya majanga nilishuhudia mafinga why niliyajua mengi nilikuwa mtoto wa nurse tena mtoto pendwa.....

Asanteni wadau uzi wangu umesomwa na watu wengi naamini umetoa elimu kubwa kuhusu hili gonjwa ..

Wengine wanasema bora ukimwi kuliko kansa...ni hivi ukiwa na ukimwi hata kansa unapata kiu rahisi mno yaani ukimwi ni kama boss la magonjwa yote linapiga simu moja kansa njoo mara moja inakuja....likiamua kumwite chawa wake TB fasta tu.... bado kijana wake mkanda jeshi

Ukimwi ni boss wa magonjwa ukiamua inaweza sema basi tumvuruge awe kichaa unakuwa kichaa madaktar wanajua hili yaani ninaposema UKIMWI ni boss la magonjwa yote namaanisha linaweza sema tuletee vidonda tu utapata hadi ufe

Hizo kansa kwa watu wenye ukimwi ndo nyumbani maana boss wao ukimwi si anakuwepo ndani utashangaa unapata kidonda hakiponi then kansa

AIDS SIO MCHEZO
Hii ni kweli kabisaaa,..Nimeona watu wengi wakisemekana wanasumbuliwa na figo, kansa mara kifua au presha,... lakini chini ya kapeti wengi wao ni Waathirika......
 
Sio mafinga tu HIV vijijini mkoa wa mara pia napo ipo ya kutosha

Nilienda huko kwa kazi ya mkataba hii miradi ya wadau wanao support wanaoishi na HIV aisee

Nimekoma kwenda huko katu sirudii

Binafsi nimetumia pep mara 2 pia nimezika wengi tu na kushuhudia vijana wadogo sna wakiteseka na hilo gonjwa
Bila kusahau migodini,...nimeshuhudia mengi sana Chunya,...baadhi ya vijiji, huitaji kuwa mtaalamu kujua hiki kijiji kimewaka....
 
Chifu ukimwi hauna mfanano. Huu ugonjwa acha kabisa. Ugonjwa ambao mume anakula arv mkewe hajui au mke anakula arv mumewe hajui na hapo unakuta wanaendelea kuzaa!Wazazi wanakula arv watoto hawajui.

Kwenye mazishi cv ya ugonjwa wa marehem inabadilishwa. Ukitaka kujua jiulize hapa kuna comment 400+ kuna wachangiaji wangapi wamekiri kuwa na shida hii na ujiulize je ni kweli hamna mwenye shida hiyo? acha kabisa Ukimwi baba lao aisee.
Kila mmoja anasema Hana....😞😞🥲
 
Upande wa mama walizaliwa kumi.Wakike 6,wakiume wanne.wajomba wote wako hai
Ila huu ugonjwa ukawabeba
Mama×
Mama mdogo×
Mama mdogo×
Mama mdogo×
Mama mdogo×
Mama mdogo×
Baba nae akaenda wakatuacha wadogo sn.Huu ugonjwa hadi leo umetuathiri sn kisaikolojia.ila MUNGU ni mwema tunapambana
 
Back
Top Bottom