Hamna kitu hapo na kwa hali hii jeshi letu kukaa kimya Kwa uoga wakati wanasilaha sishauri mtu kuandamana hiyo tarehe 29 sababu watu watakufa ovyo sababu hao waganda hawana huruma na mtanzania ndio maana huyo bibi amepanga kuwatumia na hakuna kitu kitakachobadilika itakua kazi bure tu
Unataka jeshi liingie kati wewe umekaa ndani unakunywa chai?
Ni jukumu lako kuipambania nchi yako, nani kakuambia wanajeshi pekee ndio jukumu lao kuipambania hii nchi?
Kingine hao walioingia hawajaingia wao kama wao, wanapewa support na wanajeshi wengine na wakiwemo wanajeshi wakubwa wenye vyeo, si suala la kukurupuka hovyo. Mambo ya kiusalama hayaendi hivyo.
Usifikiri wanajeshi wana miili ya chuma, na wao wana familia, wana watoto na watu wanaowategemea, wanafanya mambo kwa tahadhari. Na jeshini sio wote wapo upande wa wananchi, mapandikizi ya uvccm yapo, ndugu za mafisadi wakubwa wapo, wanufaika wapo...
Huwezi kurupuka hovyo kama mlevi kuanza kushambulia hao askari kutoka UG, japo inajulikana wanakuja kuzuia maandamano lakini huwezi jua wametumia sababu zipi na sheria ipi kuwaingiza, maana ccm inajulikana kwa kutumia sheria mbovu walizotunga wao kukandamiza demokrasia.
Tuseme unawashambulia, halafu wanakuja kutoa documents wanasema waliingia nchini kisheria kwa ajili ya kupata mafunzo kutoka JWTZ, hapo mahakamani utajibu nini ? wewe waache hadi siku waingie barabarani ndipo itajulikana..
Wewe kama unakaa ndani kaa ndani, kuna wengine watatoka, suala la kutupia jeshi lawama halitosadia ni jukumu ako kama mwananchi kuipambania nchi yako. Hata kama jeshi litakaa upande wa serikali.