Haijaisha mpaka iishe!
Waarabu wanafungika, hawana mpira wowote bahati tu imewabeba!
Nabi kachelewesha sana sub. Leo kachemka! Alitakiwa half time irudi timu ingine baada ya kuwa Nyuma kwa goli moja!
Tumemiliki mpira asilimia 60, ila mtu wa kuwaunganisha Mayele na Musonda alikosekana!
Aziz Ki hakuwa makini alikazana kutaka kufunga badala ya kawaida yake kutoa mapande, anao anao sana badala ya kuharakisha kutoa pasi , c Morisson alielewa alichokosea Aziz Ki.
Mayele hakupata usaidizi akawa anacheza pembeni, Ambundo au Denis Nkane wanajua kukimbia na Mayele ,
Kibwana hakupanda inavyotakiwa!
Timu haikukaba kama kawaida yake, waarabu walirelax wakiwa na mpira!
Pengo la Aucho lilionekana timu ilikosa balance!