Siwezi kusahau haya manyanyaso ya mama wa kambo

Amen 🙏
 
'Siyo mwandishi mzuri' ...huku unamwaga madini tena vizuri kabisa!

Ndiyo nyie mnachanganyaga watu kusema: 'Sina'ela' huku unaporomosha bonge ka jumba!

Kwenye mada yako umetoa kama darasa.

Wanawake(binadamu) ni wanyama kama walivyo wanyama wengine, tofauti ya binadamu ni kwamba tumepewa utashi.

Kama ushafuga kuku, unaonaje majike yakitotoa vifaranga namna yanavyobehave?

Koo huyu, hataki kuoviona ama kusogelewa na vifaranga vya mwenzake na vikimsogelea anaviadhibu kwa uchungu bila sababu.

Hisia za chuki za namna hiyo hata kwa binadamu tumeumbiwa, ila kwa sababu sisi tumepewa akili ya kujitambua na kutafakari mambo, yatupasa kuchambua na kuvidhibiti vitendo vyetu vya ovyo na kufuata njia iliyosahihi kutendea wengine.

Mama yako huyo wa kambo ana tatizo la kiakili na hawezi kujidhibiti hisia zake ovu.

Hapo wa kulaumiwa ni babako mzazi ambaye ni guardian wa familia kushindwa kuingilia na kukomesha uonevu huo mapema kabisa kabla haujaota mizizi.

Wasichoelewa kina mama wa kambo walio wengi ni kwamba malezi ya mtoto huwa ni ya muda mfupi na baadaye huishia kujitegemea na kufuata maisha yake.

Kama ulimlea vizuri, lazima mtoto huyo atarudisha upendo na fadhila kama zile ambazo angelizitoa kwa mamake mzazi.
 
Pole sana Binti Sayuni03 ila mpaka mwaka uishe nitakuwa nakujua na kukufahamu kila kitu isipokuwa hapo kati ,fanya mpango na hapo nipaone ili mambo mengine yaendelee
 
Nilicho jifunza kupitia haya niliyopitia ni kuishi vizuri na watu maisha yanabadilika muda wowote unaweza kumfanyia roho mbaya mtu kesho ndiyo akawa msaada wako, kama wao walipo sasa mimi ndiyo wananisumbua wakiumwa au wakikwama hela ya chakula ninawapa ninapojisikia, wangekuwa walinjtendea vizuri nadhani ningekuwa na ratiba nzuri kabisa ya kuhakikisha kila baada ya muda flani nahakikisha wanapata matumizi, sifanyi hivyo na sitaweza ninafanya kwa kiasi kidogo tu kwasababu ni wazazi
 
Alikuwa anasema akimuacha ikitokea kaumwa nani atakuwa anamuogesha, ndiyo maana akabaki kumg'ang'ania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…