Social Media: Usijikute Unabishana na Mtu Mwenye Low IQ Bila Kujua!

Social Media: Usijikute Unabishana na Mtu Mwenye Low IQ Bila Kujua!

Mitaa ya IG, Twitter (X), JF, na kwingine ni kama jungle ukikosa Emotional Quotient (EQ) ya kutosha, unaweza kuingia kwenye mabishano makali, ukijitoa ufahamu, kumbe mwenzako ni mwanafunzi wa kidato cha tatu! au mwingine kavurugwa/low IQ.

Wengine ni vichalii vinavyoishi kwa waume za dada zao, lakini wakishika simu, wanakuwa mabosi wa mitandaoni.

Hii mitaa inakuhitaji uwe mbunifu, ujue tofauti ya mabishano ya maana na kelele za watoto wa shule na watu wenye IQ ndogo. Usijichoshe bure ujanja ni akili, si hasira!
Mda huo unatumia nguvu nying mpaka fuvu linafuka mosh, kumbe unahangaika na kitoto kimetoka kula ugari wa dada.
Ndo maana mtu akija na hasira me sionyesh hasira
 
Wapi nilisema una amini maneno ya huku kumbe ? Humu matajiri wapo na hawana kelele kama sie , kwasababu utajiri na kelele ni kama paka na panya.
Mbona kama unanipigia mfano😂
 
Mda huo unatumia nguvu nying mpaka fuvu linafuka mosh, kumbe unahangaika na kitoto kimetoka kula ugari wa dada.
Ndo maana mtu akija na hasira me sionyesh hasira
Aise, pia watu wengine una interact nao humu wanakuvuruga bure, hawana hata direction ya maisha. Unajaribu kuleta mada zenye umuhimu kwako na wadau wenye IQ kubwa lakini unakutana na watatu wanne wanaojaza tu "shit posting."(JARIBU KUANGALIA REPLIES ZA WATU FULANI HAPO JUU WALIVYOKUWA WAKIJIFARIJI NA KUSUPPORT UJINGA) yaani Ni kama kujaribu kumwaga maji kwenye gunia la makengeza.

Mdau mwenye busara haangaiki na vichwa visivyo na maarifa, maana anajua upepo hauwezi kuelekeza meli isiyo na dira.
 
Kabisa bro binafsi nikinywa naona akili inataka kupasuka kwa madini yaliyopo😄
Kuna jamaa nili enda sehemu nimetulia akaja jamaa akaomba akae kalewa mpaka anasahau anacho ongea..

Anaongea vitu havieleweki kabisa yaani anaongea mambo yasiyo eleweka.

Sipendi upuuzi nikaondoka zangu maana Kuna watu ni mental case.
 
Kipindi cha nyuma hapo jf na Twitter (x) ilikua ni mitandao iliyoonekana kama ya watu wa hadhi fulani,
Hata unapoingia jukwaani kwa mara ya kwanza unakagua comment yako kama ina sifa ya kuwepo jukwaani,
Ila kwa sasa mambo yamebadilika facebook wamehamia huku, anaweza mtu kuomba msaada ila ukisoma comment unapata mashaka na wanaochangia,
Sijui nini kitairudishia sifa jf iliyokuwapo awali
 
Back
Top Bottom