Socrates, Plato na Nietzsche: Siyo kila mtu anatakiwa kuwa kiongozi

Hivi@Kiranga Kiranga ulipita hapa
 
Mtoto wa mtu kama Elon Musk au Joseph Stiglitz ana asilimia kubwa ya kuwa na uwezo wa kiakili kama baba yake. Huu ndiyo ukweli.
Kama ambavyo elon musk aliibuka tu na kujipatia umaarufu bila baba yake hivyo tunaamini elon musk ni juhudi zake ndio zimemfikisha na wala sio alirithi kwa baba yake.

HIvyo hivyo hata hao watoto wakiwa na akili sio kwa sababu ya elon musk wamemrithi hapana bali ni kwa sababu ya juhudi zao na malezi ambayo watakulia nayo.
 

Unaongea kama una facts na una uhakika na unachosema kwa kujiamini kabisa, Duh.

Baba yake alikuwa anamiliki migodi ya madini Zambia, Hotels, lodge, biashara nyingi sana pamoja na kuwa engineer, sailor, pilot na Consultant.
 
Unaongea kama una facts na una uhakika na unachosema kwa kujiamini kabisa, Duh.

Baba yake alikuwa anamiliki migodi ya madini Zambia, Hotels, lodge, biashara nyingi sana pamoja na kuwa engineer, sailor, pilot na Consultant.
Imani yangu ni kwamba elon musk umemtolea kama mfano tu lakini hauwezi kulinganisha utajiri wa elon musk na baba yake.

Elon musk ana utajiri mkubwa na amefanya mambo makubwa tofauti na baba yake hivyo sioni urithi hapo bali ni juhudi binafsi na makuzi aliyopitia.

Achilia hilo kuna matajiri wengi tu ambao tumeanza kuona wao wakifanya makubwa na sio baba zao.

Hivyo hata kama ukaikataa hoja ya elon musk na baba yake bado wapo wengine wataprove ukweli wa hilo jambo.

Alafu pia elewa tu mkuu bakhresa usitegemee watoto wake wakawa masikini,watakuwa matajiri sio kwa sababu ya kurithi akili haoana bali kwa sababu wemeshakuta njia walizotengeneza wazazi tayari.

.hivyo suala la kurithi akili ondoa kabisa mkuu wangu
 
Kwani kuwa kiongozi unatakiwa na DNA strands za aina gani?Acha kuwaza na kuamini kwa DNA kama za Mangungo zinafaa kwa UONGOZI
Nadhani unapungukiwa na uwezo wa kiakili.

Fanya utafiti kidogo kuhusu Sultan Mangngu wa Msovero utakuja kushangazwa na matokeo yake.
Sultan Mangungu wa Msovero ni kiongozi aliyeona miaka 100 mbele.Alichokifanya yeye,Leo hii kinafanywa kwa ubaya mara mbili tena ikulu kukiwa na sharehe na tafrija juu.
Mangungu alikuwa genius

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Mwanangu uko vizuri,hata mm binafsi hua siamini ktk democracy na equality,nnaamini fika kabisa kua kuna watu wanauwezo wakufikiri,kiutendaji ,kiubunifu zaidi ya sisi wengi ila hawana nafasi namfumo umewwaweka nje walioshikiria vijiti ni watu wengine wasio nauwezo wowote hata mambo ya kawaida tu kushugulika nayo niahida ,unayohoja ya msingi usikilizwe.
 
Hakika, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Unazungumzia nature vs nurture.
Nasema hivi viongozi wa juu wanahitaji vyote vipaji vya asili vya uongozi na mazingira, elimu, role model sahihi kuongoza taifa kubwa kama Tanzania.

Angalia kiongozi wa sasa wa Tanzania, anajifunza kazi kazini, anabahatisha, hit and miss, angalia teuzi, tenguzi, uwajibikaji na kuwajibisha walio chini yake.

Sera zake ni kutembeza bakuli duniani na sio kujitegemea, rushwa imetamalaki kila sehemu nidhamu imeporomoka. Role model wake ni nani? Unamjua.
Elimu yake ni ipi? ya kuungaunga.
Familia, ukoo wake imetokea wapi? Mume wake anajishughulisha na nini? Misimamo yake toka awali ilikuwaje, inajulikana?

Sidhani kama ana kipaji cha uongozi, lakini nurturing, elimu sahihi ya kiuongozi ingeweza kumsaidia hata kiduchu kujua vipaumbele sahihi vya nchi kama angeandaliwa toka kijana kuja kuchukua nafasi kama hii.
 
Nakubaliana na wewe kwennye mengi uliyoyasema mkuu.
 
Ila jamani, mimi siwaonei, najaribu kusema uhalisia uliopo!


......Hivi Wand kwanini uzi wa siasa mmeuleta huku jukwaa la intelijensia....?
 
Kivipi mkuu? Tufafanulie, sisi wengine kipindi kikwete anaingia madarakani tulikua bado wadogo kuchanganua mambo makubwa
2005 kulikua na Dr Salim Ahmed Salim, Prof Mark Mwandosya, kati ya wengi waliokuwepo!

kiuwezo na kiutendaji Kikwete hawakaribii hata nusu hao wawili niliowataja, lakn kwa sababu alijenga mtandao mkubwa na akawa na timu kubwa nyuma yake, basi chama kikampitisha!

(inasemwa walitoa pressure kubwa sana kwa Mkapa ili jina la jk lisikatwe, walifikia hatua ya kwenda chadema mchana kweupe kutoa taarifa eti 'mgombea wao' akikatwa basi watahama chama timu nzima na wafuasi wao.......)

matokeo ya uongozi wa kikwete hadi leo tunaugulia, madhara yake ndio haya tunalia nayo hata leo
 
Sio kila mtu anatakiwa kuwa kiongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…