Soko la Hisa la Dar es Salaam na orodha ya makampuni yaliyosajiliwa

Soko la Hisa la Dar es Salaam na orodha ya makampuni yaliyosajiliwa

kk achana na hiyo issue kama huna mtaji wa kutosha, wanaofaidika n wale waliowekeza pesa nyingi kwa hyo issue sasa kama ww una ka milion moja chako usijaribu utaumia vibaya mno.

Tambua vle vle sio faida tu bali company ikipata hasara na ww inakuusu, share pia zikishuka bei ni majanga

kwa Tanzania hii biashara ya hisa bado ni changa sana uki compare na kenya. kenya kuna watu wanaishi kutokana na hii kazi kwa tanzania makampuni yenye share kwenye Dar es salam stock exchange ni haya apa TCC CRDB NMB TWIGA CEMENT PRECION AIR na mengineyo, hayazid 12

nakushaur nunua share za TCC, crdb ni majanga. wanauza share bei rahisi ila hazina faida yyte:flypig::flypig::flypig:
 
Habar wadau, nmejarbu kufwatilia kuhusu soko la hisa linavyoendeshwa na kwa jinsi gan mtu unaweza ukajihusisha na soko hilo yan kununua hisa ili kutengeneza faida baadae ila sijafanikiwa kupata details za kueleweka.

Ningependa kuelimishwa kuhusu hili soko kabla sijafanya maamuzi ya mwisho kutumbukiza kapesa kangu nilichodunduliza. Nafaham kuna makampuni mbalimbali yanauza hisa zake ila sifaham vgezo vp vya kuzingatia wakat nataka kununua hisa za kampuni flan, vlevle napenda kujua hii biashara kama ina hasara, je hasara yake inakuja kivip?

Je kuna dhamana yoyote kwa mtu aliyenunua hisa za kampuni flan halaf kampuni ikafa/ikafilisika?
Naomben mchango wenu wadau..
 
As of Today hizi ndio stock Updates
[h=3]Stock Updates[/h] [TABLE="width: 100%"]
[TR="bgcolor: #1869B4"]
[TD="width: 75%"]STOCK[/TD]
[TD="width: 24%"]PRICE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]ABG[/TD]
[TD]7,030[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CRDB[/TD]
[TD]310[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]DCB[/TD]
[TD]490[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]EABL[/TD]
[TD]4,920[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]JHL[/TD]
[TD]5,900[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]KA[/TD]
[TD]240[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]KCB[/TD]
[TD]870[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]MBP[/TD]
[TD]600[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]NMB[/TD]
[TD]2,700[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]NMG[/TD]
[TD]5,790[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]PAL[/TD]
[TD]470[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]SIMBA[/TD]
[TD]2,480[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]SWISSPORT[/TD]
[TD]2,700[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]TATEPA[/TD]
[TD]650[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]TBL[/TD]
[TD]8,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]TCC[/TD]
[TD]10,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]TOL[/TD]
[TD]310[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]TWIGA[/TD]
[TD]2,460[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Inategemea wewe na mahitaji yako katika ushiriki,

1.unataka kushiriki kama kampuni ili uuze baadhi ya hisa za kampuni yako kwa umma au

2, unataka kushiriki kama mtu binafsi unaetaka kununua hisa za makampuni yaliyoorodheshwa katika soko la hisa?.

Kama ad 1, unatakiwa kuuza hisa kama kampuni, uwasiliane na mamlaka ya soko la mitaji na hisa hapa Dar. kama ad 2, unataka kushiriki kama mtu binafsi ukiwa hapa Dar nenda kwa mawakala wa masoko ya mitaji na pesa yako uweke order ya kununua hisa ya kampuni zilizoorodheshwa, watakuelekeza tu. kama uko mikoani nenda benki ya CRDB au NMB watakuunganisha na soko la mitaji bila shaka. mafanikio mema.
 
thanx GwaB, nimekupata, ila bado kuna utata katika bei za hisa, coz nahitaj kama mtu binafsi na si company, hawana huduma za moja kwa moja kwa kutumia simu?
 
thanx GwaB, nimekupata, ila bado kuna utata katika bei za hisa, coz nahitaj kama mtu binafsi na si company, hawana huduma za moja kwa moja kwa kutumia simu?
Bei za hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye Soko (DSE) zinachapishwa kwenye baadhi ya magazeti kwa ajili ya kutoa taarifa na kuwa kiongozi kwa watu kama wewe.

Ila hizo bei ni kwa siku zilizopita si kwa siku hiyo au baadae. Pia baadhi ya vipindi vya television, hasa baada ya taarifa ya habari, hutoa taarifa za bei katika Soko la Hisa. Ukitembelea kwenye tovuti za Soko (DSE) au Mamlaka ya Masoko na Mitaji (CMSA) utapata taarifa za Mawakala wa Soko la Hisa na kuweza kuwasiliana nao moja kwa moja.

Taarifa kama hizo unaweza kuzipata kwenye matawi ya CRDB nchi nzima.
 
Tatizo DSE wamelala sana, nina uhakika kama wangekuwa wanatoa mwamko kwa wananchi basi leo tungeongea mengine.

Watanzania hatuna elimu ya hii mambo na wengi wana excess pesa kwenye account zao na hawajui nini cha kufanyia.

Mfano, mtu anakuja ana 10000000 anaomba ushauri wa biashara gani ya kufanya lakini angekuwa na taarifa ya DSE angewekeza huko.
 
Soko la hisa linafaa kwa mtu yeyote ilimradi uwe na uwezo wa kununua kiwango cha chini cha hisa kinachotakiwa kwenye Soko la Hisa (DSE). Nadhani kwa sasa ni hisa 100.

Hakuna dalali atakayekutafutia/kuuzia hisa chini ya hapo. Kuhusu faida inategemea unazinunua hisa kwa lengo gani. Kama ni kupata kipato cha kutosha unapaswa uwe nazo nyingi ili hata faida (gawio) utakalopata liweze kuwa la kutosha. Kwa mfano, ukiwa na hisa 100 za kampuni X na mwisho wa mwaka ikatangaza gawio la Shs. 200 kwa kila hisa ina maana utapata Sh. 20,000. Mwenye hisa 1,000 atapata Sh.200,000.

Mwenye hisa 10,000 atapata Shs.2,000,000. Wengine wananunua hisa kwa ajili ya kukuza mtaji. Kwa mfano wakati unanunua bei ya hisa ilikuwa Sh. 500. Labda baada ya miaka miwili unataka kuuza na bei ya kila hisa kwenye soko imepanda mpaka Sh.1,200. Utakuwa umekuza mtaji kwa Sh. 700 (1,200-500) kwa kila hisa. Lakini vile vile wakati wote ulipokuwa unazimiliki hizo hisa ulikuwa unapata gawio la faida.

Kwa maneno mengine soko la hisa ni kama biashara nyingine. Ukiwekeza mtaji mkubwa na faida unayopata ni kubwa (kama biashara imeenda vizuri).
 
Brokers wanasaidia sana kwenye ushauri, usifuate trend ya online utakimbia
 
Ndugu wana JF, napenda kufahamu zaidi kuhusu jinsi ya kuwekeza kwenye soko la hisa katika mambo yafuatayo:-

1.Kujua hisa zenye faida
2.Mtaji unatakiwa kuweza kupata faida hasa kwa mtu mwenye kipato cha kati
3.Ni hisa za kampuni gani zenye faida katka uwekezeji.

Ntapenda kujifunza kutoka kwenu ukizingatia mie ni mfanyakazi napata muda mchache sana kusimamia bihashara nyingine.
 
Kuhusu ni Hisa gani uwekeze inabidi mwenyewe ufanye due diligence ya kuchunguza kampuni na kuangalia ni Kampuni ipi ina uwezekano wa kuendelea kwa kuangalia historia ya kampuni, products zake na management yake (hakuna guarantee kwamba kampuni itaendelea milele) hata kina KODAK walifirisika, ingawa kina Coca Cola huenda ikawa vigumu kufirisika kuliko labda industry za ushindani kama Technology n.k. anyway kuhusu hisa ni nini na jinsi ya kuwekeza angalia hapa...

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-biashara-na-uchumi/638786-soko-la-hisa.html
 
Kununua hisa, minimum ni hisa mia hivyo kuhusu faida utapiga hesabu wewe.
Nakupa mfano mdogo: Hisa za kampuni ya Swala zilipoingia sokoni miezi michache iliyopita zilikuwa zikiuzwa kwa sh. 600 na leo hii ni sh. 1840. Kwa mantiki hiyo, mtu aliyenunua hisa 1000 kwa wakati ule ilimgharimu sh. laki sita na akiziuza leo hii atapata sh. milion moja na laki nane, yaani ni mara tatu ya ile pesa ya awali.

Binafsi, nakushauri ununue hisa za CRDB. CRDB ana perform vizuri sana sokoni kwasasa na hisa zake ni sh. 345 (bei ya leo) ukinunua hisa elfu kumi itakugharimu 3,450,000 au hisa elfu moja ni sh. laki tatu na arobaini na tano. Miezi michache ijayo hisa za CRDB lazima zitapanda sana.

Pia kampuni za cement ni nzuri na hauna dini au dini yako haikubani, nunua hisa za TBL au TCC.

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)
 
Last edited by a moderator:
Kuwekeza kwenye masoko ya hisa kuna faida kubwa lakini vilevile kuna riski kubwa, na hiyo ni theory ya kibiashara high return always associated with high risk.

Hizi stock zipo za aina kuu mbili , kuna common stock na preffered stock. kama kampuni inafirisika wenye preffered mnakuwa wa kwanza kulipwa na wenye common mnakuwa wa mwisho. na hizo common stock zipo za aina mbili , nyingine traded katika IPOs.

Si razima ununue hisa , unaweza ukanunua bonds katika bond market market na ukapata faida kubwa kwa muda mfupi. zipo bonds za miezi mitatu , mwaka , hadi miaka kumi.

Kabla hujanunua hisa kwenye co yoyote inabidi inabidi ufanye speculation , kwa sababu co ikipata hasara na wewe utakuwa umepata loss. Ni pm nikuelekeze jinsi ya ununuaji wa hisa na makampuni ambayo utatengeneza faida, siwezi kuyataja hapa itakuwa nafanya promo.
 
Kuna mtu anaweza kutujuza juu ya uwekezaji kwenye Treasury Bills?
 
Aisee walionunua hisa za swala kwenye IPO sasa wanachekelea...
 
Ukinunua hisa zinakaa mda gani kupata gawio lako
 
Ndugu wana JF, napenda kufahamu zaidi kuhusu jinsi ya kuwekeza kwenye soko la hisa katika mambo yafuatayo:-
1.Kujua hisa zenye faida
2.Mtaji unatakiwa kuweza kupata faida hasa kwa mtu mwenye kipato cha kati
3.Ni hisa za kampuni gani zenye faida katka uwekezeji.

Ntapenda kujifunza kutoka kwenu ukizingatia mie ni mfanyakazi napata muda mchache sana kusimamia bihashara nyingine.

Afu pia mjue kuna makampuni yana zero dividend policy kwa kumaanisha wao hawatoi dividend ila faida yote wanaifanyia retained earnings,so the only profit utakayopata ni kwny capital gains yan kama ulinunua hisa sh.2000 per hisa then ukija ukauza may be sh. 4000 per hisa then sh. 2000 ndo capital gains
 
Back
Top Bottom