Soko la Machinga Dodoma, tumpe Rais Samia maua yake

Soko la Machinga Dodoma, tumpe Rais Samia maua yake

Hakuna kitu hapo, naumia sana kuona Taifa tuna risishana ujinga, wakati wenzetu wana risishana akili. Unachinga ni vitu ya ku descourage kwa gharama yoyote ile, ila Bongo tuna hamasisha Unachinga si kwa sababu za Kiichumi bali za kisiasa
Shida unasifia kwa kufika.mara moja tena kama reporter tuulize wakazi tulioishi na tunaoendelea hapa tuambie kuhusu MACHINGA COMPLEX ya dar hadi kuanza kuchoma masoko ya mchikichini kazimisha watu wahamie pale
 
Tuna sapoti ujinga badala ya kuja na sera nzuri za Vijana kuwekeza tunawatengenezea nazingira ya wao kuendelea kuwa wajinga, Hao wana siasa kuna ndugu zao ni Machinga?

Nchi tuna risishana ujinga,
Soko lina ujinga gani
 
Soko ni landmark lile.

Serikali ikiwekeza ktk ideas kama hizo tutaondokana na wamachinga kuvamia mabarabara na kutembeza bidhaa kwenye bars.

Mapato yataongezeka
Nchi ina laana hii. Haya mabanda ndiyo rais anasifiwa? Nadhani tuko kwenye hali mbaya sana.
 
Nnia pekee ya kuondokana na Macbibga ni uwekezaji kwenye viwanda, vijana wapate ajira, au uwekezaji mkubwa kwemye kilimo.

Hmachinga ni kutengeneza Taifa ka watu wasio waza wanao waza uchuuzi tu, Wamachinga wanakuza uchumi wa China
Mkuu ungelijua kuwa machinga wanasaidia sana kupunguza makali ya inflation usingekuwa na makasiriko namna hii
 
Nchi ina laana hii. Haya mabanda ndiyo rais anasifiwa? Nadhani tuko kwenye hali mbaya sana.
Hayo mabanda yanawawezesha vijana wajasiriamali kuhudumia familia zao na kuchangia pato la Taifa.

Sometimes we need to be appreciative kwa vichache vinavyoonekana
 
Hayo mabanda yanawawezesha vijana wajasiriamali kuhudumia familia zao na kuchangia pato la Taifa.

Sometimes we need to be appreciative kwa vichache vinavyoonekana
Uko good sana aisee
 
Mkuu, huogopi kukasirisha watu fulani hv?!!!!
Mkuu
Nilishaweka hapo juu wapo watakaoshangazwa.

Ninapoona wananchi ni wanufaika wa moja kwa moja na huduma za serikali hapo lazima nioneshe shukran kwa serikali.

Tunawapambania wananchi na siyo matumbo yetu
 
Ahhahahahha mimi dodoma hapana nitabaki dar
Miafrika ndivyo tulivyo.
Hatutaki kuhangaisha akili zetu. Ndio maana dar imejaa uswazi kwa sababu ya kila mtu kukimbilia dar,. Dodoma ni mji unaojengeka na baada ya miaka 10 ijayo utajuta kusema maneno yako. Kuwa na miji mingi mikubwa kunaifanya dar ipumue na hata kujengeka vizuri zaidi maana influx ya watu kukimbilia huko itapungua kwa sababu ya uwepo wa majiji mengine yenye huduma muhimu zinazolinga au kukaribiana na huduma zinazopatikana dar.
 
Wengi watashangazwa na huu uzi.
Nimekuwa nakosoa tena kwa lugha kali utendaji wa hovyo usiozingatia uhalisia hususani kuanzia awamu hii ya sita.

Tembea uone.
View attachment 2660495
Nilifanikiwa kutembelea soko la Machinga pale mji mkuu Dodoma, nilijihakikishia kuwa plan na ukamilishwaji wa mradi wa soko hilo la Machinga umefanikiwa kwa kiasi kukubwa.

Sijajua kwa undani soko hilo likikamilika linapaswa liweje lakini kwa kila Mtanzania na mgeni anayetembelea atakubaliana nami kuwa soko hilo linaweza kuwa la kisasa kwa afrika mashariki na kati.

View attachment 2660496
Nimekuta wamachinga wamepangwa vizuri, alama za wapi utakuta aija ya bidhaa unazotafuta zinaonekana kwa uwazi. Zimeandikwa kwa lugha yetu tukuka ya kiswahili ambapo ni uamuzi wa dhahabu. Usafi wa soko na hata huduma mbalimbali muhimu kwa machinga na wanunuzi zipo. Nimekuta lipo eneo limetengwa ndani ya soko la wamama kunyonyeshea, kuna ATM, store, vyoo vizuri. Maeneo ya baba na mama lishe yametengwa vizuri hata sehemu za nyama choma nje ya soko zinashawishi kwani meza za wateja ni za marble ambazo zinadumu kuliko mabati na mbao.

View attachment 2660501
Kelele ndani ya soko zimedhibitiwa ambapo wenye vipaza sauti hawaruhusiwi kufungulia sauti kubwa.

Kuhusu usafiri, soko limejengwa pembezoni mwa barabara kuu huku kukiwa na kituo kikubwa cha daladala kuelekea maeneo mengi ya jiji la dodoma. Kimsingi serikali imewatendea haki wamachinga kwani imeamua kuwaweka mahala sahihi ambapo haimlazimishi mteja kwenda umbali mrefu kutafuta petty goods. Nilimuuliza mmachinga mmoja wanalipa kiasi gani kwa siku akasema wanalipa Tshs 1,000 na akaenda mbali zaidi kuwa anaiona ni fair kwa sababu soko halikauki wateja pia alilinganisha na eneo lake la biashara pale Kariakoo aliloamuq kuachana nalo kwa sababu hata hrla wlizokuwa wanatoa kwa jiji hazikuzuia harassments za mgambo na kukithiri kwa uchafu.


Tofauti na majiji mengine kama Dar, wamachinga wanaondolewa maeneo potential kwao na kutupwa nje pembezoni mwa mji ambapo hata miundombinu kama vyoo, umeme , usafiri vinakuwa ni taabu.

Kwa mfano pale Kariakoo wangechukua mfumo wa soko la Machinga Dodoma hakika wangeweza kukidhi takwa la serikali kuwakusanya machinga na hata wakachangia pato la jiji kwa tozo watakazolipa. Serikali inaweza kuongea na NHC wakapanua eneo lile kulifanya liwe efficiency kwa biashara.

Pale Mbagala Zakhiem kuna utopolo umejengwa ambapo wamachinga hawatakuwa na nafasi zaidi ya wafanyabishara wenye msuli wa fedha.

Kwenye hili soko la Machinga Dodoma, tuungane kumpongeza Mama Samia kwa sababu amefanikiwa kuwapatia machinga sehemu stahiki kwa shughuli zao. Pia kama ikipendeza masoko kama haya yajengwe kwenye majiji hapa nchini na kuangalia pale Mbezi Mwisho kujenga soko la Machinga la kisasa ili kuongeza wigo wa nchi jirani kuja kununua bidhaa kama wanavyofanya Kariakoo na Mbagala.


Muwe na weekend njema


CC: Pascal Mayalla ChoiceVariable bubex_jr johnthebaptist emback Ne91cM Mzee Mwanakijiji Dr. Mariposa Dr Matola PhD FaizaFoxy Mohamed Said
Asante kwa kutujuza. Pongezi nyingi kwa waliobuni wazo, ku finance na kusimamia ujenzi. Maendeleo hayana chama.
 
Back
Top Bottom