Soko la Machinga Dodoma, tumpe Rais Samia maua yake

Mkuu nakubaliana nawe kabisa, lile soko ni mzuri na limejengwa sehemu sahihi na ndio maana huduma muhimu zipo bila matatizo. Aidha kwa Mbezi, panafaa sana kujenga soko kama lile maana sehemu za kujenga zipo. Nadhani lile eneo la wazi katikati ya barabara kuu ya njia 8 na barabara ya service road ambapo daraja la juu la watembea kwa miguu wanao vuka barabara kutoka Mbezi Bus Stand na kutokezea Mbezi Stand ya daladala na mwendokasi. Eneo hilo linatosha kabisa kuwaweka wamachinga wote wa Mbezi. Eneo lina anzia upande wa Magharibi mwa stand ya daladala hadi kwa Yusufu (round-about) Eneo linakidhi kwa soko.
 
Umeongwa kitaalam sana
Wapangaji mipango wa Dar waandae mkakati huo
 
Mkuu Ujamaa, nakubaliana nawe juu ya namna ya ongezeko la hawa wamachinga; ni kweli kabisa kwamba pamoja na sababu zingine zinazopelekea ongezeko la wamachinga lakini hizi ulizozitaja ndizo zinazo zalisha watu hawa. Aidha sikubaliani nawe katika kutatua tatizo la uzalishaji wa hawa wamachinga. Hili la baadhi lawanachinga kutembeza bidhaa zao na la kuwapatia baadhi ya barabara kuendesha biashara zao naona kama tutarudi tulikotoka. Nadhani njia sahihi ni hii ya kuwajengea masoko kwa kadri ya idadi yao; maeneo yapo.
 
hilo soko nani alieanza kujenga nani...??.mda mwingine uwe unakua na akili...
 
Sikuwahi kufikiri kwamba unaweza kuwa chawa.
 
Utajenga Kila Kila sikuuu?? Maana wanazalishwa Kila sikuuu. Maana yake tuwe tunapanga bajeti Kila siku ya majengo ya kifahariii kama hayooo?? Kiwanda Cha machinga nikila sekunde wanazalishwa utawezaaa?? Ni Vyema tutafute namna nzuriii ya kitatua
 
Hayo mabanda yanawawezesha vijana wajasiriamali kuhudumia familia zao na kuchangia pato la Taifa.

Sometimes we need to be appreciative kwa vichache vinavyoonekana
Hili siyo jambo la kusifu. Ni jambo lililochewa na lina-reflect mamtatizo yetu. Sitakaa nisifie dalili za matatizo.
 
Huku kwetu mvua zimenyesha za kutosha, pongezi sana kwa mheshimiwa rais mama dokta Samia.
 
Asante mama na mtaka kwa kazi njema. Kanyaga twende mama piga kazi tumecheleweshwa mnooo kama taifa zaidi ya 7 miaka
 
Mkuu, huogopi kukasirisha watu fulani hv?!!!!
Siku zote mawazo ya mtu ndio uondoa ujinga elimu hii haikutokea Kwa mwingine Bali Ni JPM alisema lazima unapotaka kuwaondoa machinga barabarani uwawekee mazingira mazuri hivyo Hakuna anayeumia.
 
Wakati anavoingia madarakani,akatoa agizo la kuwapanga machinga...wakuu wa mikoa mingi kama kawaida wakawanunulia migambo virungu vipya tayari kuingia kazini,maeneo mengi machinga walipigwa na kufukuzwa katikati ya miji..

Watu wote ikiwemo wabunge walikaa kimya kwa vipigo vile vya machinga,isipokua H. Polepole aliyejitokeza kuwatetea.

Ni mkuu wa mkoa wa Dodoma pekee kipindi kile Mtaka aliyekuwa na approach tofauti. Anasema kwa maneno yake mwenyewe akifanyiwa mahojiano " Tuliamua tuwe na mtizamo tofauti,nikaongea na mheshimiwa atupe muda tusiwafukuze machinga mjini,bali tuwajengee soko hapa hapa mjini ili wafanye shughuli zao,nae akanikubalia"

Kumbe unaweza ukaona mtizamo wa aliyeombwa machinga wasifukuzwe mjini Dodoma ulikuaje,hasa ukitizama hakuingilia kati vipigo kwa machinga wa majiji mengine. Sifa na utukufu ni kwake yeye
 
Mama anaupiga mwingi sana. Tuachane na akina Mbowe na CHADEMA yao wanakumbatia ukabila na udini na kusahau uungwana wa mama yetu.
 
Walinda ligacy na Chadomo watatukana 😂😂
 
Siku zote mawazo ya mtu ndio uondoa ujinga elimu hii haikutokea Kwa mwingine Bali Ni JPM alisema lazima unapotaka kuwaondoa machinga barabarani uwawekee mazingira mazuri hivyo Hakuna anayeumia.
Okaaaay, kumbe. Nashukuru kwa taarifa. Wakitokea watu wakiuliza vipi kuhusu Machinga complex ya Dar iliyoanza kipindi cha jk haikuwa mwanzo wa yote haya, nitawaambia ''KOMENI! TENA MKOME SANA!''
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…