Soko la Mbeya liliungua miaka zaidi ya kumi na halijajengwa, ila la Kariakoo limeungua juzi tu limetengewa bilioni 34

Soko kuu ni matola mpaka leo lipo alijawahi ungua wewe unazungumzia Uhindini pale panatakiwa kujengwa Supermarket sio soko kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo
Pale ndipo lilikuwa soko kuu. Soko Matola halijawahi kuwa soko kuu. Na fahamu kuwa hata supermarket ni soko. Super-market.
 
Dah nasikitika kuona kuna baadhi Wameshindwa kujibu na kuweka utofauti wa kisiasa wao tunasafari ndefu sana, anyway kwa sasa dar ndio inapewa kipaumbe kikubwa sana kutokana na mapato yake pia population ni kubwa na uhitaji ni mkubwa pia ila kuna haja ya kupanga upya tena ili kupunguza na kutanua wigo mbeya ingefanya vizur kama ingepangiliwa vizur sababu ina nafasi ya kuhudumia nchi za majirani ila tatizo viongozi hawafikilii nje ya box.
 
Ni tatizo. Mikoa yote ya mipakani kama Kagera, Kigoma, Songwe, Mbeya nk ingeweza kujengwa masoko ya kimataifa. Kungekuwa hakuna sababu ya watu wa kutoka nchi jirani kwenda mpaka Dar kufanya manunuzi ya jumla.
 
Dah, basi tuna viongozi wa ajabu sana. Wanaona bora miaka kumi ipite hivihivi! Ndiyo maana watu huhusisha kuungua kwa masoko na hujuma.
Kama unaishi Mbeya unalionaje hilo eneo lililozungurukwa na mitaa minne na lipo uhindini katikati ya jiji, ungekuwa na madaraka ungeliachia?
 
Mtoa uzi anazungumzia soko la uhindini mbeya ambalo lipo katikati ya jiji mkabala na NMB Mbalizi road . karibu na ofisi nyeti.

Kwa sasa lina tumika kama car parking.. ila nmeona building plan yake..
litajengwa kubwa kuliko hata hilo la dar.. kuna video na attach hapa.

Ingawa tetesi ni Kuwa Chief Ha--nga-- Yaaa... hapatani kabisa na mbunge Betina.. ndiyo maana Mbeya imelala hoii kwa sasa
Ugomvi wao unatokana na nini?

Walikuwa wanagombea mwanaume ?
 
Kama unaishi Mbeya unalionaje hilo eneo lililozungurukwa na mitaa minne na lipo uhindini katikati ya jiji, ungekuwa na madaraka ungeliachia?
Nafikiri ndiyo piece ya ardhi yenye thamani zaidi mjini au niseme mkoani Mbeya kwa sasa. Lazima livutie ufisadi. Hata hivyo ni mali ya umma. Itumike/ningeitumia kwa maslahi ya umma.
 
Halafu malizia KARIAKOO SOKO LA TAIFA, hilo la Mbeya bado kunahela tunaisikilizia
 
Dah nasikitika kuona kuna baadhi Wameshindwa kujibu na kuweka utofauti wa kisiasa wao tunasafari ndefu sana, anyway kwa sasa dar ndio inapewa kipaumbe kikubwa sana kutokana na mapato yake pia population ni kubwa na uhitaji ni mkubwa pia ila kuna haja ya kupanga upya tena ili kupunguza na kutanua wigo mbeya ingefanya vizur kama ingepangiliwa vizur sababu ina nafasi ya kuhudumia nchi za majirani ila tatizo viongozi hawafikilii nje ya box.
kwahiyo we ndio unaona umeandika point?
 
Hii imakaaje. Ni kwamba serikali inafanya miradi yake kwa upendeleo?
Linganisha potentiality ya masoko hayo. Angalia mapato serikali inayopata kwenye masoko hayo, wanufaika ( yaani wafanyabiashara na wanunuzi kwa idadi yao), sehemu soko lilipo (hadhi ya eneo), umri wa soko na historia yake kitaifa.

Ukiondoa ushabiki, utakuja kuona usahihi wa maamuzi hayo ya serikali kulipa hicho kipaumbele
 
Ni ngumu kulinganisha kwa sasa kwa sababu soko hili limeungua zaidi ya 10 yrs. Kumbuka kuwa hili ndilo lilikuwa soko kuu la Mbeya. So hata kama halifikii umuhimu wa soko la Kariakoo ila ni moja ya masoko muhimu Tanzania. Kihistoria hili soko lilikuwa linahudumia mikoa ya nyanda za juu kusini, hivyo hata kihistoria ni muhimu. Hili siyo soko la mtaani. Lilikuwa ni soko kuu la mkoa wa tatu kwa kuchangia pato la taifa.
 
Back
Top Bottom