Sokomoko la zawadi ya gari ya Rais mstaafu Mwinyi

Tatizo hapa ni ufinyu wa taarifa!

Aliyemnunulia Mwinyi hilo gari ni Samia au ni serikali?

Wewe umesema ni Samia. Unaposema ni Samia unamaanisha ni Samia kama Samia au ni Samia kwa niaba ya serikali?
Ufinyu wa taarifa, na ndio maana watu wanajadili. Kungekuwa na taarifa inayojitosheleza huenda mjadala usingefika huku.

Kama ingekuwa SASHA kamnunulia mzee kwa pesa zake hapo hakuna mjadala, kama katumia pesa za serikali basi tujue..
 
Ni mamoja ni mali ya serikali au amepewa binafsi kutoka kwenye hazina ya umma.
Msimamo wa dini ya Kiislamu katika jambo hili ni mkali sana. Huwezi kuchukua mali ya watu ukaitumia upendavyo.
Bwana mmoja aliwahi kwenda kwa Khalifa Omar bin Al Khattab, usiku. ( Omar alikuwa ndiye rais wa Waislamu wote wakati huo waliofikia takriban milioni 4 na mali zilizokadiriwa dola bilioni 7 (kwa sasa) wakitawala mataifa ya Rumi (wazungu) na Waajemi (Iran). Akamkuta anafanya mahesabu ya pesa zilizoletwa kama Zaka kutoka mikoa ya Syria na Yemen. Yule bwana akamwambia, nimekuja kwa mzungumzo nawe. Omar akamwuliza, mazungumzo binafsi au ya masuala ya umma? Akasema, ya binafsi. Omar akachukua ile koroboi ilyokuwa inawaka, akaizima. Akamwita bwana yule asogee, gizani. Yule akauliza, vipi, mbona umezima taa? Omar akasema, ndiyo, mafuta ya taa hii yamenunuliwa kwa mali ya umma, si mali yangu. Na wewe una mazungumzo nami ya haja zako binafsi. Nahofia Mwenyezi Mungu atakwenda niuliza juu ya matumizi haya ya mali ya umma!

Huo ndio Uislamu usiofuatwa!
 
ACHENI KULIALIA NA KULALAMIKA
NYIE PAMBANENI NA HALI ZETU,
TAFUTENI MALI KIVYENU!
HAO MNAOWAONEA GERE WAKO KWENYE
MFUMO WAO NA FAMILIA ZAOOOOO

ova
 
Urais ni ajira usisahau hilo bwashee!
 
Hata mm nimejiuliza kama ile kubwa ilikuwa ndefu kuipanda ina maana hata mtoto wake alishindwa kumnunulia gari linaloendana na umri wake? Kuna mengi ambayo hamujajui. Bora uzima.yetu macho.
Isije kuwa baba ntu kapewa zawadi ya hepi bethi dei, vijimaneno navyo huwa haviishi huku kitaa...
 
Hakuna hata moja iliyoniuma.
 
Kabla ya kuandika hili bandiko reeefu... ungeangalia kwanza aina ya hao wanaolipigia kelele hilo "benz la chini" wana akili za aina gani? Je ni walewale walioshangilia wakati mwendazake akiwagawa "wale ndege wa ikulu" apendavyo kana kwamba ni mali yake binafsi au ni wale waliokaa kimya?
Nadhani sasa midhali mitandao imefunguliwa ingelikuwa vema tujadili vitu vyenye afya kwa Taifa...
 
That’s what I thought too…
Serikali haigawi zawadi mali ya umma, bali serikali inagawa stahiki zilizopo kwa mujibu wa sheria.

Mwinyi kapewa zawadi siyo stahiki.
Stahiki zimeorodheshwa, zinajulikana na zina utaratibu wake.

Wapi na ni lini mzee ruksa kaomba serikali impe Benz?.

Ni daktari gani wa Mzee ruksa aliyerecommend Benz?.

Samia kajuaje kuwa Benz ndo inayomfaa mzee ruksa na siyo gari nyingine?.

Lile gari ambalo mzee ruksa analo sasa, litarudi serikalini au nalo lunakuwa lake binafsi?
 
Unayo majibu ya hayo maswali yako?
 
Unayo majibu ya hayo maswali yako?
Ni rhetoric questions ambazo tukio la jana linaonyesha mzee kapewa surprise tu ya "Birthday gift"

Ingekuwa imefata official Channel ya mzee kuomba gari serikalini kama sehemu ya package ya stahiki zake basi lisingetolewa kama Zawadi, kuvalishwa gift ribbon, maana ingekuwa siyo gift bali ni haki ya mtu!

Kiufupi kwa maelezo ya Samia, Samia mwenyewe kaona mzee anapata tabu ya kupanda gari na kushuka basi akaamua ampe "Zawadi" ya benz
.
Sasa angempa kwa fedha zake za mfukoni hatuna shida, lakini kutwaa mali ya umma na kumpa (nje ya package ya stahiki za mzee), sisi tunaona ukakasi
 
Unajuaje kuwa hajampa kwa fedha zake [Samia] za mfukoni?

Au unasadiki hajampa kwa fedha zake toka mfukoni?
 
Mkuu Nyani Ngabu heshima kwako. Bandiko lako limenifanya "Nitabesamu" kidogo na kunifanya niwaze kidogo " Nje ya Box". Hongera sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…