Sokomoko la zawadi ya gari ya Rais mstaafu Mwinyi

Hiyo ni zawadi ngodo sana, hata dimondi huwa anagawa magari ya kifahari kwa ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi na mahawala wake🤣

 
Kwa hili bi mkubwa kachemka.
Unless kama katoa pesa yake mfukoni lakini kama pesa ni ya serikali mama ajitafakari, kwa yale maneo aliyoongea mama lile gari sasahivi ni mali ya ali hassan mwinyi kwahiyo hata akided halirudi serikalini
 
Ngabu, mimi katika kuwajua wazungu na namna wanavyoendesha mambo yao, wapo strict sana kwenye matumizi ya pesa za umma. Nilishanga kujua kwamba kama rais wa marekani amealika wageni wake binafsi white house, gharama za entertainment ya wageni wake atatumia pesa zake binafsi. Miaka ya karibuni spika wa bunge la australia alilazimika kujiuzulu baada ya kukodi helkopita kwenda kwenye kikao cha chama, ukaibuliwa mjadala kwa nini asitumie gari la ofisi ambalo linagharamiwa na pesa ya walipa kodi kama kweli alihudhuria kikao cha kikazi? kwa hiyo trend ninayoona kwa nchi za kiafrika hususan Tanzania ni kwamba ukishakuwa rais wa nchi au kigogo mkubwa upo entitled kutumia pesa za serikali kadri ya utashi wako au utashi wa wale wanaoidhinisha matumizi ya pesa za umma. Rais mstaafu analipwa pensheni, ulinzi na usafiri. Sioni mantiki serikali kuendelea kutumia pesa za walipa kodi kumpa zawadi za birthday za magari ya gharama huku ikendelea kumlipa pesheni na kugharamia usafiri wake na ulinzi wake....
 
Nimeeleza siyo zawadi. Ni stahili yake.
Tatizo la watanzania kuhoji.You nailed it bro. Rais Mwinyi alipopewa nyumba na Hayati Rais Magufuli kulikuwa na kelele?Just curious!!!
 
akili yangu iko kamili niamini ndo maana niko mbali kiuchumi kisiasa!

hiyo kila ukinunua una changia ni huduma unazopewana sirikali za kawaida za kila siku.

Ni utamaduni wa Dunia nzima. Tangu enzi za Yesu.
Hakuna Serikali ambayo haina wajibu wa matumizi ya pesa za wachangiaji ndio maana kuna bajeti na maelekezo ya matumizi mtu mmoja au wachache haifai wajiamulie matumizi ya pesa ya jamii

Huduma gani za kijamii zimeteteleka ajili ya manunuzi hayo?
Km nchi itateteleka ajili ya kibenz cha mstaaf ife au iuzwe tu.
Issue sio kama iliyotoka ni ndogo au nyingi issue ni matumizi kama hayafuati utaratibu na kufanya urahisi wa kila kiongozi kujiamulia kutoa pesa utamaduni huu unaweza ukajenga kufuja pesa..., hatukatazi kutoa zawadi hata wewe ukitaka toa chochote ila maamuzi yasiwe yako binafsi alafu utumie pesa za wote

Pesa za Serikali ndio pesa za wananchi usidhani wanafyatua pesa sehemu, kwavile natua pesa nipate huduma za barabara ulinzi na mahakama zipo ndio nisiseme au kuuliza kuhusu pesa za wananchi ?, Unaongelea Kodi yangu, sio kodi yangu kodi zetu.., Serikali inaendeshwa kwa kodi kama hujui ndio leo nikwambie

Ina biashara nyingi sana km hujui.

Ina misaada ile misaada haiji hivihivi kuna watu wanapitisha kopo kimatonya.Ili ule bado unalindwa na familia yako bure usionewe na wanyarwanda.
Kweli akili yako inahitaji nyongeza, Serikali ina biashara nyingi sana (hizo bishara ni za nani kama sio wananchi kwa ujumla), inavyopata pesa kwenye utalii na maliasili kama sio mali ya wananchi ni ya nani (viongozi ?), Misaada wanatoa misaada kwa niaba ya aliyeomba kama yake au anaomba kwa niaba ya wananchi ?, na unadhani wanapokopa ni nani atakayelipa kama sio wewe mpaka vizazi vijavyo ?


Boda boda ililetwa bure au imenunuliwa kutokana na biashara ambayo fedha zetu za kigeni zinatumika, au madini tunayouza n.k., na tunapopewa mikopo nani atalipa ? (na misaada inayokuja na masharti ya kutubana (ni nani analipa kama sio mwananchi) unaweza kumuona mkulima mlima pamba ni mpuuzi ila bila yeye kulima hio pamba au mkulima kulima mahindi unadhani hata huyo Rais angekuwa na cha kukiongoza ? Sio lazima kuwe na made in Tanzania ndio ujue nguvu ya mwananchi unadhani madini yanayouzwa au swala ambao badala ya kuwala tunawaacha ili watalii waje sio sacrifice ?

Acha kuangalia mambo kwa upeo sawa na urefu wa pua yako....
 
Tupe majibu Professor ipi inauma matumizi ya benzi ama kuokoa mtu asifungwe!?
Mzee ukiangalia kwa mtazamo huo unakosea. Nchi hii nimewapa mfano mdogo tu unaonaendelea hivi sasa wale covid 19 pale mjengoni wanatafuna kwa mwezi zaidi ya milioni 250 isivyo kihalali kwa ujinga tu wa spika na chama chake CCM je hiyo pesa ingeweza kujenga madarasa mangapi? Huu ni mfano tuu wa matumizi mengi ya hovyo nchi hii. Hilo la kupewa zawadi ya Benz ni suala dogo sana lisitupe presha.
 
Hakujenga pekee yake, yeye anakila kitu wakati waliomsaidia wengi wao hawana kitu. Tuache kuwatukuza hawa viongozi!!! This thinking hautifikishi kokote inaturudisha nyuma sana
Hufahamu maana ya leadership!! Hata muwe na resources nyingi bila right leadership ni sawa na ZERO. If you can't capture this it's unfortunate then
 
Kwani hilo gari kimenunuliwa akapewa AHMwinyi?

Hilo ni moja ya magari 20 yaliyotolewa na Mfalme wa Morocco King Hassan VI kama zawadi kwa Tanzania. Ila Mwendazake alikuwa amekauka kama vile ni magari yake binafsi.
 
Maskini wataendelea kufa na vinono vitaliwa na matajiri na wanasiasa milele na milele. 🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂
 
La juu haliwezi, wamempa la chini, well and good.

Hatutaki aibu ya kusikia rais Mwinyi kaumia au hata kibaya zaidi kimetokea kwa sababu kajikwaa akipanda gari refu ambalo limekuwa likimpa shida kupanda, tutaonekana wajinga dunia nzima kwa kushindwa kuhudumia wazee wetu.

Lakini je, wamempa la chini, hilo la juu wamelichukua kwa sababu linampa shida?

Au ndiyo kiendacho kwa mganga hakirudi?

Kwa sababu kama wamelichukua hilo la juu, hapo wamembadilishia tu.

Na kama hawajalichukua, kwa nini wameliacha gari lenye matatizo hivyo?
 
Binti wa Profesa Yule Simba damu mtaalam wa mifupa anadai Rais kashauriwa vibaya. Kwa maana ya muda wa kuongea na wazee kuwa karibu na kumpa zawadi mzee mwingine.
 
kujipendekeza ndio imezidi haswa kwa watanzania, yaaani unakuta mtu anajipendekeza kisa anataka madaraka!! huu ni upuuzi mtupu, unacho takiwa ni kujiheshimu na kuheshimu watu wengine.

kujipendekeza na hadaa.

mbaya zaidi kuna viongozi wengine hawapendi hata watu wajue/wafahamu ukweli wa maisha ya kiongozi mfano hata haya maisha tuliyo yajua kupitia kitabu chake wapo wapumbavu wachache watanuna kwa sababu zile zile za unafiki na chuki.
 
Binti wa Profesa Yule Simba damu mtaalam wa mifupa anadai Rais kashauriwa vibaya. Kwa maana ya muda wa kuongea na wazee kuwa karibu na kumpa zawadi mzee mwingine.
Leo Jumapili, nasoma Biblia.

Matayo 25:29


29 Kwa maana kila mtu mwenye kitu ataongezewa, naye atakuwa navyo kwa wingi. Lakini kwa yule asiye na kitu, hata kidogo alicho nacho atanyang’anywa.
 
Na mimi nitagombea uraisi,makamu wangu atakuwa Mzee Rungwe Sipunda,safari hii hatutagwa wali bali tutagawa biriani, tena biriani kutoka pale Mchambawima. Kwa marupurupu haya sikubali lazima ngombee uraisi.
 
Leo Jumapili, nasoma Biblia.

Matayo 25:29


29 Kwa maana kila mtu mwenye kitu ataongezewa, naye atakuwa navyo kwa wingi. Lakini kwa yule asiye na kitu, hata kidogo alicho nacho atanyang’anywa.
Ndiyo maana kuna baadhi wanatilia sha "New Testament", kwamba ipo kimkakati.
Hii haimaanishi naunga mkono imani yako na akina Ayan Rand ( R.I.P)
 
Mimi naona huku ni kudhalilishana kweli. Hawa ni watu walioomba wenyewe hiyo kazi, hawakutufanyia favour kwamba alikuwa mahali tukamuomba aje atusaidie. Huyu aliwatumikia raia wa nchi hiyo kwa utashi wake. Sasa haya ya shukrani zilizopitiliza zinatoka wapi?

Hakuna Rais mstaafu ambae hakuna nyumba yake binafsi ( wengine zaidi ya moja). Hamna Rais mstaafu asie na uwezo wa kujinunulia gari anayoitaka kutokana tu na posho yake ambayo ni asilimia 80 ya mshahara wa Rais aliyekuwepo. Rais mstaafu anapewa magari mawili na yanabadilishwa kila baada ya miaka mitano. Analipiwa mpaka dobi. Yote hayo bado tunaona ana shida sana kiasi cha kutaka waboreshewe mafao yao! Kusema leo tunamjengea nyumba Rais mstaafu na kumnunulia gari ni kumdhalilisha kuwa ni maskini kiasi hicho.

Kwa wenzetu Marekani Rais mstaafu anajinunulia nyumba. Sijasikia waziri mkuu wa uingereza au India wakipewa nyumba au magari baada ya kustaafu. Wao kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma wanatarajiwa kuwa wamejipanga kwa ajili ya maisha ya ustaafu.

Mimi ningeunga serikali kama ingetenga fungu ( milioni 500) ambazo mstaafu ataweza kutumia kujenga kitu chenye faida kwa jamii kama kumbukumbu yake, vitu kama maktaba, sehemu ya utafiti n.k.

Haya ya nyumba na magari ni kuwafedhehesha tu. Aidha, itaonekana kama Rais aliyepo anayapigia debe kwa vile anajua yeye pia atanufaika.

Amandla....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…