Sokomoko la zawadi ya gari ya Rais mstaafu Mwinyi

Sawa....nini mnataka kifanyike
Kuondoa mambo haya

Ova
 
Kwanini wanasiasa wastaaafu wanajipanga marupurupu kama ya wale wa nchi zilizoendelea ila sisi tunaambiwa pesa haitoshi. Juzi juzi mwinyi alikabidhiwa nyumba ya zaidi ya shs bil 7!
 
Kwanini wanasiasa wastaaafu wanajipanga marupurupu kama ya wale wa nchi zilizoendelea ila sisi tunaambiwa pesa haitoshi. Juzi juzi mwinyi alikabidhiwa nyumba ya zaidi ya shs bil 7!
Sijui!

Labda uwaulize wenyewe..
 
Sawa....nini mnataka kifanyike
Kuondoa mambo haya

Ova
Nimesema hapo juu. Badala ya kupewa magari na kujengewa nyumba watengewe fungu ambalo watatumia kujengea mradi wenye faida kwa jamii ambao utakuwa kama ukumbusho wake.

Amandla...
 
Nadhani gari litabakia la serikali lile v8 litabakia nyumbani yeye apande benz ajili fupi ...apande kirahisi
 
MATAGA wanapata tabu sana na mama Samiah Suluhu.MATAGA&Sukuma -Gang ni watu wenye roho mbaya sana!
 
Hata mm nimejiuliza kama ile kubwa ilikuwa ndefu kuipanda ina maana hata mtoto wake alishindwa kumnunulia gari linaloendana na umri wake? Kuna mengi ambayo hamujajui. Bora uzima.yetu macho.
 
Sasa 450 m mbona unaziona si mali kitu wakati 38 m zilikuuma!? Au matumizi ya 38 m yalifanya jambo lisilo na manufaa kwa taifa lakini 450 zimefanya jambo muhimu, zito, la lazima na manufaa kwa taifa!?
Hizo milioni 450 mmezitoa wapi?
 
Kwa maoni yangu zawadi sio jambo la msingi sana kujadiliwa, tunapoteza malengo na makusudio.

nadhani hata yeye mwenyewe Mzee wetu Babu yetu wa Taifa Mzee Ruksa atafarijika zaidi akiona tunajikita kujadili MAUDHUI ya kitabu chake alicho kiandika badala ya kujadili ZAWADI aliyo pewa.
 
Kwa nini unasema Hussein hawezi kushindwa kumnunulia mzee wake hilo Benzi?

Hussein ana hela nyingi sana au kwa sababu yeye ni Rais wa Zanzibar?
 
Ahsante ndugu!

Jamaa kala kona mazima baada ya mimi kuweka ushahidi ambao upo kinyume na uzushi wake.

Ndo maana sasa nimeamini kuwa hata nyumbu wana akili nyingi zaidi kuwashinda hawa watu wa aina ya huyo jamaa uliyemnukuu.
 
Kwa nini unasema Hussein hawezi kushindwa kumnunulia mzee wake hilo Benzi?

Hussein ana hela nyingi sana au kwa sababu yeye ni Rais wa Zanzibar?
Mzee "kibongobongo" baba akienda age vijana wanachukua hatam. Sasa ni zamu ya Hussein kumhudumia mzee wake.
 
Bima!!!? kwani kuna askari anaweza kulikagua hilo gari?? sheria huwa zipo kwenye makaratasi na huwa zinatumika kwa wanyonge sio kwa level hiyo.
 
Ndo maana nikauliza kama kama wamempa au wamembadilishia tu..

Siku zote nimekuwa nikidhani Rais mstaafu hupewa usafiri wa serikali kwa matumizi yake.

Na kwamba huo usafiri ni mali ya serikali na si mali yake binafsi.

Tatizo letu ni uwazi. Haya mambo yangekuwa yako wazi wala watu tusingehoji sana hii leo.

Au labda yapo wazi lakini ni sisi tu ambao hatujui…
 
Binti wa Profesa Yule Simba damu mtaalam wa mifupa anadai Rais kashauriwa vibaya. Kwa maana ya muda wa kuongea na wazee kuwa karibu na kumpa zawadi mzee mwingine.
Kwani Rais yeye hana akili yake mwenyewe ya kuweza kujua kisichofaa na kinachofaa?

Rais akishauriwa ajambe hadharani atakubali tu kwa vile kashauriwa hivyo?
 
Kwani Rais yeye hana akili yake mwenyewe ya kuweza kujua kisichofaa na kinachofaa?

Rais akishauriwa ajambe hadharani atakubali tu kwa vile kashauriwa hivyo?
Milioni 450 inaonekana ni pesa nyingi lakini ni ndogo sana kwa matumizi ya marais linapokuja suala la usafiri wao.

Mama wanamletea zengwe ili mradi tu nafsi za baadhi ya watu ziweze kuridhika.
 
Fundi…umesema kuwa Rais mstaafu huwa anapewa magari mawili na huwa yanabadilishwa kila baada ya miaka 5.

1. Hayo magari mawili huwa ni ya aina gani? Yanayofanana au yasiyofanana?

2. Ina maana Rais Mwinyi sasa kapata gari ya tatu au wamembadilishia tu moja kati ya hayo mawili uliyosema wanapewa?

Narudia tena kusema kuwa huendi tatizo hapa ni timing, optics, word choice, na labda setting…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…