It's a law of nature. Mwenye nacho huongezewa. Asiyekuwa nacho, basi anaweza kunyang'anywa hata kidogo alichobahatika kuwa nacho ili achukue mwenye nacho kingi tayari...
Mwinyi anapewa zawadi ya gari aina ya Germany Technology Mercedes Benz na serikali na siyo Mama Samia Suluhu Hassani...
Inashangaza kidogo kwa sababu kiongozi mstaafu kama Mwinyi mwenye privileges na marupu rupu kibao na mwenye familia nzuri yenye watoto wenye nyadhifa kubwakubwa na uwezo Mkubwa wa kiuchumi ktk jamii, anashindwaje kujinunulia yeye mwenyewe gari atakalo kwa mahitaji yake kwa gharama zake toka ktk fedha nyingi anazolipwa na serikali wakati wote...?
It doesn't make any sense, right...?
Mama Samia Suluhu Hassani, Rais wa JMT umeanza kuboronga mapema sana. Unaanza kulewa madaraka mapema sana. Unaanza kuanza kuyatumia madaraka yako ya Urais vibaya mapema sana...!
I am afraid to say that, this is very dangerous to your presidency...
Nakuhakkikishia kuwa, unaweza kuishia kuwa Rais wa hovyo sana pengine kuliko hata Mwendazake Pombe Magufuli...!!
LABDA UNASAHAU HARAKA SANA....
Kumbuka, ni wiki jana tu umetoka Mwanza kwenye sherehe za Mei Mosi. Wafanyakazi waliitaka serikali yako ingalau iongeze mshahara hata Shilingi 50,000 tu kwa kila mfanyakazi. Ulijitetea vizuri, tukakuelewa na tukasema tutakuvumilia sawasawa na ombi na maneno yako...
Aidha kumbuka jana tu pia ulikusanya "wazee wa Dar". Wakaiomba serikali unayoingoza ifanye vitu vidogo kadhaa...
Ukajitetea wewe " Malkia wa maneno matamu" huku ukisingizia hali mbaya ya uchumi wa nchi...
Ukawaomba upewe muda. Wazee wale kwa nilivyotazama nyuso zao, wakakuelewa na kukupa " benefit of doubt "..
Lakini leo katika hali ya kushangaza unaamua kumzawadia fedha za wazee na wafanyakazi hawahawa wa nchi hii Mzee Ally H. Mwinyi kiasi cha fedha za kitanzania kati ya 900,000,000 hadi 6,900,000,000 (bilioni 6.9) kama zawadi ya birthday yake....!!
Are you really serious Madam President..?
Labda hujui na wewe na watu wako mnadhani Watanzania hawajui gharama za magari hayo iwapo ni mapya. Ngoja tukueleze...
Binafsi nilipopata tu unachotaka kufanya, haraka haraka nimetembelea soko la aina hii ya magari mapya mtandaoni, nimeshangaa kwa sababu bei yake ni kubwa sana..
Mercedes Benzi ya bei ndogo kabisa kwa kuzingatia muundo na toleo ni USD 400,000 sawa na Tshs. 920,000,000...!!
Ya bei ya juu kabisa ni USD 3,000,000 sawa na Tshs 6, 900,000,000 (bilioni 6.9..!!!)
Hapa chini ni baadhi ya picha ya magari haya..
View attachment 1779132View attachment 1779134
Hivi unadhani kuna sababu gani ya Watanzania kuendelea kuamini kuwa wewe mama kama kiongozi wa nchi hii unakwenda kufanya tofauti na aliyekutangulia nawe kwa bahati tu umejikuta ni Rais wa nchi hii...?
It's a wrong decision at a wrong time...
Achana na hii kitu. Hizo fedha unazoziona hapo siyo zako. Ni fedha za Watanzania zaidi ya 60,000,000. Tafadhali usuanze kupagawa mapema hivi, utaharibikiwa. Tumia busara na hekima kuzitumia fedha hizo ili kila Mtanzania aone impact yake..
Unapata wapi ujasiri wa kumzawadia mtu mmoja Tshs. 900,000,000 (huku tayari akiwa fedha zake nyingi tu) kati kati ya kundi kubwa la wananchi unaowaongoza ambao zaidi 30% wanaishi katikati ya umasikini uliotopea...??
View attachment 1779135
View attachment 1779136
View attachment 1779137