Sometimes Huhitaji Ushauri Wala Pesa… Unahitaji Tu Mtu Mmoja Akukumbatie na Kukuambia: Everything Will Be Okay

Sometimes Huhitaji Ushauri Wala Pesa… Unahitaji Tu Mtu Mmoja Akukumbatie na Kukuambia: Everything Will Be Okay

Kuna wakati maisha yanakupeleka sehemu mpaka unatamani usingezaliwa kwenye hiyo familia uliyopo.

Au unajikuta unajuta kuishi, imefikia hatua mpaka mtu unatamani kujiua tu ili uepukane na madhila ya dunia.

Naandika hii thread huku nikiwa natetemeka na kukata tamaa. Natamani mtu aniambie tu nitakuwa sawa. Najiskia vibaya sana na nina uchungu mkubwa sana ndani yangu.🙏
Pole sana, upo wapi nikufate?
 
Sema na mimi maneno haya "oh jesus,fanya muujiza maana nipo kwenye giza na ukija mwanga unaniumiza!!! Baba please kama unaniskiza naijongea altare nambie neno moja na mimi ntabaki pale"....
Hilo jaribu lako ni dogo na utalishinda njoo ufanyiwe maombi,wenye tatizo kama lako wengi wameshafunguliwa
 
Kuna wakati maisha yanakupeleka sehemu mpaka unatamani usingezaliwa kwenye hiyo familia uliyopo.

Au unajikuta unajuta kuishi, imefikia hatua mpaka mtu unatamani kujiua tu ili uepukane na madhila ya dunia.

Naandika hii thread huku nikiwa natetemeka na kukata tamaa. Natamani mtu aniambie tu nitakuwa sawa. Najiskia vibaya sana na nina uchungu mkubwa sana ndani yangu.🙏
Mama P pole kwa unayopitia.

Usiumie sana, jipe moyo. Tambua kwamba giza likiwa nene, kunakaribia kupambazùka.
Usikate tamaa, kesho njema na ya furaha iko mbele yako.

Mungu akutie nguvu.
 
Hisia hiyo ina nguvu kubwa sana. Wakati mwingine maneno mengi au suluhisho la kifedha haliondoi ule uchovu wa ndani ya roho.
Unachohitaji ni ubinadamu tu—kuhisi upendo, usalama, na uwepo wa mtu anayejali bila kukuhukumu.
Kumbatio na maneno hayo rahisi hubeba ujumbe mzito kwamba hauko peke yako katika mapambano yako
 
Kuna wakati maisha yanakupeleka sehemu mpaka unatamani usingezaliwa kwenye hiyo familia uliyopo.

Au unajikuta unajuta kuishi, imefikia hatua mpaka mtu unatamani kujiua tu ili uepukane na madhila ya dunia.

Naandika hii thread huku nikiwa natetemeka na kukata tamaa. Natamani mtu aniambie tu nitakuwa sawa. Najiskia vibaya sana na nina uchungu mkubwa sana ndani yangu.🙏
Mama pretty, wewe ni wa thamani sana! Tena sana...! Nakufahamu kama rafiki mwema na mtu wa maana Sana!
Tafadhali simama hapo ulipo na usitishe fikrq za kutoa uhai wako amq kujidhuru kwa nqmnq yoyote ile...! mawazo haya ya giza na ya kutaka kujidhuru ni uongo mkubwa unaoletwa na uchovu mwingi na uchungu wa sasa,
lakini haukufafanui wewe wala thamani ya maisha yako, . Maumivu unayoyapitia yana nguvu kwa muda mfupi tu, lakini kesho yako inaahidi mambo mazuri, makubwa na ya kuvutia ambayo bado hujayashuhudia
 
Pole sana Mama Pretty, kuna wakati shida za familia au changamoto za dunia zinatuelemea mpaka tunajiona hatuna thamani ya kuishi tena. Nataka ujue kwamba hisia zako ni valid kabisa, na ni sawa kabisa kulia na kuishiwa nguvu wakati mwingine.

Hata hivyo, naomba usiruhusu hayo mawazo ya kukata tamaa yashinde hii vita, wewe ni mtu wa thamani sana, na kuna watu wengi wanaokupenda na wanaohitaji uwepo wako hapa duniani, shusha presha yako sasa hivi, usijihukumu kwa unavyojisikia, na uweke akilini kwamba you are stronger than you think. Hii hali ngumu unayopitia ni ya mpito tu na itapita, nina uhakika utakuwa sawa kabisa, please don't lose hope kabisa.
Nashkuru sana, najitahidi🙏
 
Nakuelewa sana,kipindi ulichopo usijidhuru na kujiona sio chochote haupo pekeako kwenye Hilo. yawezekana hutupo nawe kimwili kimaana pamoja lakini tupo nawe kiroho nafeel hiyo hali yako,kama kuna mtu wa karibu unamuamini jaribu kumshirikisha unayopitia kwa sasa yawezekana akawa msaada mkubwa kukuondoa katika hali uliyopo.Mimi ni mhanga wa hiyo hali yako naelewa vizuri sana namna unavojisikia.
Ni kweli kabisa, ila nimekosa mtu wa kumwambia ndio maana nimekuja huku kutemea sumu yangu. Asante
 
Back
Top Bottom