Somo kwa wanawake: Usikubali kuishi na mwanaume kwa zaidi ya miaka 5 bila kufunga ndoa

Right Marker

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
194
Reaction score
625
Acha kupumbazwa na ahadi lukuki zisizokuwa na kichwa wala miguu. Ukiona sehemu haina mwelekeo ondoka.

Eti ooh!
~ "Subiri nijipange; kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri tujenge; kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri nipate hela ya kupanga vyumba viwili; Kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri nimalize chuo; kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri nipo chooni nakunya; nikitoka tutafunga ndoa".

Kila mwaka unasubiri. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, mwaka wa tatu, mwaka wa nne, mwaka wa tano, mwaka wa sita bado unasubiri huku unazalishwa. Mwaka wa saba, nane, tisa, kumi bado unamsubiri mwanaume ajipange, ajipange nini?

Unasubiri mpaka sura inaanza kukunjama (kusinyaa) ndipo unagundua kuwa mwanaume unayemsubiri ajipange tayari amefunga ndoa ya Kikristo na mwanamke mwingine aliyezaa nae mtoto mmoja. Na wewe ameshakuzalisha watoto watatu.

RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM
 
Kwa hiyo mnatusema "sisi" wenye uchumba sugu?Lakini, mkumbuke tuna watoto watatu,nyumba mbili,kipando(kinafanana na gari)kimoja na shamba hekari nne achilia mbali kipato cha kula milo kamili mitatu kila siku na uhakika wa tiba.
 
Eti ooh!
~ "Subiri nijipange; kisha tutafunga ndoa".

~ "Subiri tujenge; kisha tutafunga ndoa".

~ "Subiri nipate hela ya kupanga vyumba viwili; Kisha tutafunga ndoa".

~ "Subiri nimalize chuo; kisha tutafunga ndoa".

~ "Subiri nipo chooni nakunya; nikitoka tutafunga ndoa".
Duh aisee!

~ "Subiri nicomment; nitamuoa mchumba wangu!"
 
Mmh! Inategemea kwanini uko katika hayo mahusiano, kama ni kwa ajili ya ndoa, basi hakikisha ushauri wa mtoa mada unauzingatia haswa.. Ila kama ni kwa kwasababu zingine usiogope Kikubwa unajua unachokofanya
 
kwamba unaamua uishi na mwanaume ukitimiza yote ya ndoa ila uko na mpango mwingine?
 
Hawasikiagi wako kama kenge mpaka damu ziwatoke, anashangaa siku ya siku anatimuliwa na amezalishwa anaanza kuwalaani wanaume wote dunia nzima kumbe ni upumbavu wake, wengine wanaingia kichwa kichwa mwanaume hafahamiki hata kwao wala hajatoa hata kishika uchumba halafu utasikia anakuwa mkali utasikia "wewe unatembea na mume wangu" siku anapigwa chini akili ndo zinamrudi.

Na wanakuwaga wabishi hao hawataki kusikia ushauri wanajifanya wao ndo wanajua kupenda
 
kwamba unaamua uishi na mwanaume ukitimiza yote ya ndoa ila uko na mpango mwingine?
Kabisa, Kila mtu anasababu zake. Sio wanaume tu ndio wakuogopa vifungo visivyo vya lazima. Kikubwa ubongo na moyo vifanyekazi kwa kujitegemea katika majukumu yake.
 
Kila mwaka unasubiri. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, mwaka wa tatu, mwaka wa nne, mwaka wa tano, mwaka wa sita bado unasubiri huku unazalishwa. Mwaka wa saba, nane, tisa, kumi bado unamsubiri mwanaume ajipange, ajipange nini?
Hivi mtu ambae umeshasubiri miaka yote hiyo, na kuzalishwa watoto wote hao, hata ukisema unaondoka, unaenda wapi hasa..? Kuna muda ukishakaa na mtu, huyo anakua wakwako hakuna pa kwenda tena, kuwe na ndoa kusiwe na ndoa.
 
Samahani mkuu....
Unasemea wanawake hawa ambao wakiamka asubuhi wanawasha data badala ya kiwasha moto...🤔
Ni hatari sana kuwa kwenye mahusiano tu eti kisa huna pa kwenda ukiachwa maana umezalishwa, au kutegemea kuja kugawana mali mkiachana sijui.. Kuna ujinga mwingi hapo hata kufurahia maisha inakuwa kwa mbinde. Kama mahusiano yakibiashara yanaweza kuvunjika na Kila mmoja akaendelea kivyake kwanini isiwe mahusiano haya?!!!
 
Miaka 5 unaishi vipi na mwanaume bila kutambulika rasmi na kufuata taratibu?
 
Acha kupumbazwa na ahadi lukuki zisizokuwa na kichwa wala miguu. Ukiona sehemu haina mwelekeo ondoka.

Eti ooh!
~ "Subiri nijipange; kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri tujenge; kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri nipate hela ya kupanga vyumba viwili; Kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri nimalize chuo; kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri nipo chooni nakunya; nikitoka tutafunga ndoa".

Kila mwaka unasubiri. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, mwaka wa tatu, mwaka wa nne, mwaka wa tano, mwaka wa sita bado unasubiri huku unazalishwa. Mwaka wa saba, nane, tisa, kumi bado unamsubiri mwanaume ajipange, ajipange nini?

Unasubiri mpaka sura inaanza kukunjama (kusinyaa) ndipo unagundua kuwa mwanaume unayemsubiri ajipange tayari amefunga ndoa ya Kikristo na mwanamke mwingine aliyezaa nae mtoto mmoja. Na wewe ameshakuzalisha watoto watatu.

RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM

Ndoa ni Nini? Ukikaa na mtu miaka 5 hata kama Baba yake haukujui na mna watoto ni ndoa tayari, kama unaishi na mwanamke hata miaka 2 haijaisha, hajaenda kwenu na huna mtoto wewe ni Mpumbavu!

Kama unaishi maisha ya u GF na mwanaume na kwenu hajaenda miaka mitano, wewe ni zuzu wa kutupa, Kuna siku ataoa mtu mwingine bia Kukupa taarifa yeyote!
 
Back
Top Bottom