Gobole Lenye Risasi
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 11,519
- 23,693
Acha kupumbazwa na ahadi lukuki zisizokuwa na kichwa wala miguu. Ukiona sehemu haina mwelekeo ondoka.
Eti ooh!
~ "Subiri nijipange; kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri tujenge; kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri nipate hela ya kupanga vyumba viwili; Kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri nimalize chuo; kisha tutafunga ndoa".
~ "Subiri nipo chooni nakunya; nikitoka tutafunga ndoa".
Kila mwaka unasubiri. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, mwaka wa tatu, mwaka wa nne, mwaka wa tano, mwaka wa sita bado unasubiri huku unazalishwa. Mwaka wa saba, nane, tisa, kumi bado unamsubiri mwanaume ajipange, ajipange nini?
Unasubiri mpaka sura inaanza kukunjama (kusinyaa) ndipo unagundua kuwa mwanaume unayemsubiri ajipange tayari amefunga ndoa ya Kikristo na mwanamke mwingine aliyezaa nae mtoto mmoja. Na wewe ameshakuzalisha watoto watatu.
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM
Mwandiko wa kike au una element za ***** mwanaume hawezi andika huo uchafu mwingine. Wanawake mnadanganyana sana.