Somo la mali kwa wanandoa kwa kilichotokea kwa Achraf Hakimi na mkewe

Mama kasema "Kunatatizo Gani ikiwa ni kweli?" Elewa imeisha hiyo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dunia haitomsahau Gabriel Villa, mwanasheria kwa taaluma aliyefanya pia kazi ya uwakala wa usafirishaji.

Bwana huyu mwaka 1994 alikutana na mwanadada mrembo Christina Carta kwenye sherehe

Wawili hawa wakapendana na hatimaye kufunga ndoa licha ya kuwa Gabriel alimzidi mrembo huyo miaka 30.

Tajiri huyo mara tu baada ya kufunga ndoa alimpeleka mkewe nchini Jamhuri ya Dominica kwenye visiwa vya nchi hiyo kula maisha kwa miezi minne.

Na waliporudi waliishi pamoja kwenye ndoa ya furaha kubwa kwa miaka 20.

Baada ya miaka hiyo ishirini ya kuishi pamoja hatimaye wawili hawa waligombana na Mwanamke akaenda kudai talaka kisheria ili wagawane mali.

Lakini baada ya kufuatilia taratibu hizo za kisheria, Wanasheria wa Mwanamke huyo walimjulisha kuwa bwana Gabriel alimtaliki mke wake huyo miaka 20 iliyopita bila yeye kujua hivyo kwa miaka yote hiyo hawakuwa wanaishi kwenye ndoa.

Kumbe bwana, ile fungate bwana Gabriel aliyompeleka mkewe nchini Jamhuri ya Dominican alitumia pia mwanya huo kuandikisha talaka kabisa kwa mkewe bila mwenyewe kujua kwani kwa wakati huo ni nchi ya Jamhuri ya Dominican pekee ndiyo iliyokuwa inaruhusu kisheria talaka kutolewa bila mmoja wapo kujua.

Mwamba huyu alipoulizwa alisema alijua kuwa siku moja Mwanamke huyo angetumia mbinu ya kudai talaka ili kuchukua mali zake hivyo alijiandaa mapema😀

NDUGU YETU HUYU ANAPASWA KUPEWA CHEO GANI😀😅?

👇👇👇
 
Field Marshall. Hivi Ndikumana alitoga talaka kwa Dada la Dada?
 
Huyu
Huyu mwamba ni legend ,
 
Hayo ni maisha yake cha kujiuliza je ww una mali za kufanya ufuatilie stori za wenye pesa au utagawana vijiko na sahani. Cheo hapo mpe uafisa talaka
Mkuu hizo habari Zipo kutufunza maisha na ukisikia ulimwengu unaowafunza walioshindikana Kwa mama zao ndo huwa hivi ukiona haina umuhimu Sana kwako unapita hivi Tu.
Hayo ni maisha yake cha kujiuliza je ww una mali za kufanya ufuatilie stori za wenye pesa au utagawana vijiko na sahani. Cheo hapo mpe uafisa talaka
 
Mimi nilichojifunza mwanamke anatakiwa kuangaliwa kwa jicho la kipekee, sio wanawake wa kibongo tu ndio changamoto bali ni ulimwengu mzima,
Mwanamke anakila zana za kumdumaza mwanaume.

Binafsi nazidi kuwa mbali nao, maisha bila mwanamke yanawezeka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…