Somo la mali kwa wanandoa kwa kilichotokea kwa Achraf Hakimi na mkewe

Somo la mali kwa wanandoa kwa kilichotokea kwa Achraf Hakimi na mkewe

Nadhani wanaume tunatakiwa tujifunze kutoka kwa Hakimi.Jamaa alikuwa sawa kbsa katika Hilo alilofanya.

Hata mtume Paulo ametuusia sisi wanaume kwamba wanawake tuishi nao kwa akili.

Kudos[emoji2935] Hakimi
 
Habari za matajiri we waulize masikini wanazo zoote!!
 
Ww jamaa mbona siku hizi una andika chenga.
Yaani nimpende mke ambaye tumekutana ukubwani na ambaye kesho ataniacha na kwenda kwa mwanaume mwingine kuliko mama yangu aliye nizaa ,kunishomesha na kunipa maarifa?

Mke na mama kila mtu atapedwa kwa nafasi yake lakini mama ana nafasi zaidi ya mara kumi mbele mke wangu.

Katika ulimwengu huu hakuna kitu chenye thamani kama mama na baba yako chochote utakacho kifanya hilo unatakiwa kulitambua.
Wazazi wana thamani kuliko hata watoto wako.
... naam; na hata sio wawili tena bali wamekuwa mwili mmoja! Hiyo ndoa tafsiri sahihi ya ndoa! Kama unaweza kuwa mwili mmoja na mama yako hayo yenu sasa!
 
Niish na tajir miaka 20 akiniacha sitahitaj anigawie chochote coz nitahakikisha nakua tajir kuliko yeye
 
Binafsi nadhani kesi hii imejaa porojo mitandaoni kuliko UHALISIA wa kisheria

Hata mimi binafsi sheria hii ya kugawana mali pasu kwa pasu baada ya talaka bila kuangalia mchango wa kila muhusika inanikwaza sana

Lakini watu tunapaswa kujua kwamba hili ni TAKWA la kisheria na sio maamuzi au utashi wa mtu..... na takwa hili haliwezi kukwepwa kijanja janja

Kisheria mali zote zinazo chumwa ndani ya ndoa na wanandoa ni zenu wote
Sasa swala la kuchukua mali za wote na kuanza kumpa mama yako kinyemela lina ukakasi kisheria..... na sisitiza KISHERIA na sio kiutashi

Sidhani kama sheria zinaweza kuacha loops za kijinga kiasi hicho cha kumilikisha mali za pamoja kwa mtu mwingine bila ridhaa yenu wote

Ninachojua mimi hii bado ni hadithi za kusadikika kwasababu kisheria hapo mahakama itaamuru hesabu ya mapato yenu itatoa matumizi na kiasi kilichobaki kitatakiwa kugawanywa
Sasa kama ulimpa nani sijui hiyo utajua wewe
Utatakiwa kutoa hilo gawio
 
Hii habari umeifanya katika tunduizi provocative unless uwe feminist otherwise umeiandika katika angle yq uchokozi wa kimtizamo tu, mke awaye yeyote anahama kwao na anahamia familia ya mume na akiachika anarudi kama alivyokuja kwa maana anakuwa ameasi. Iko hivo yaani traditional perspective ya ndoa
 
Heri katika Mungu iwe nanyi!

kipekee na kwa dhati sana kwa niaba ya wapinga ndoa wote ndani ya jukwaa, Tanzania, Africa na Dunia, nampomgeza ndugu yetu kwa kutuheshimisha na kututia moyo na hamasa ya dhati kabisa sisi wadau teule tulioona mbali ya kwamba ndoa ni ubatili, unafiki, uhuni na ushetani.

Na hoja hii inahuishwa na mantiki ndoa na wanandoa wenye hila za kutaka mgao wa mali au urithi wa mali pasipo upendo wa kudumu, wenye kuingia kwenye ndoa nje na makusudi ya Mungu.

Sisi ambao kwa dhati kabisa tumekataa na upinga unafiki na kuamua kukataa ndoa tuheshimiwe na ibaki muktadha wa kukubali kutokukubaliana katika hilo.

kipekee mola ampe maisha marefu ndugu Hakimi

Inshallah Hakimi ni zawadi ya Eid.

Shukrani

Wadiz
 
Moderators tafadhari msifute hii thread hakuna lugha mbaya zaidi ya ujumbe uzi uheshimiwe
 
Binafsi nadhani kesi hii imejaa porojo mitandaoni kuliko UHALISIA wa kisheria

Hata mimi binafsi sheria hii ya kugawana mali pasu kwa pasu baada ya talaka bila kuangalia mchango wa kila muhusika inanikwaza sana

Lakini watu tunapaswa kujua kwamba hili ni TAKWA la kisheria na sio maamuzi au utashi wa mtu..... na takwa hili haliwezi kukwepwa kijanja janja

Kisheria mali zote zinazo chumwa ndani ya ndoa na wanandoa ni zenu wote
Sasa swala la kuchukua mali za wote na kuanza kumpa mama yako kinyemela lina ukakasi kisheria..... na sisitiza KISHERIA na sio kiutashi

Sidhani kama sheria zinaweza kuacha loops za kijinga kiasi hicho cha kumilikisha mali za pamoja kwa mtu mwingine bila ridhaa yenu wote

Ninachojua mimi hii bado ni hadithi za kusadikika kwasababu kisheria hapo mahakama itaamuru hesabu ya mapato yenu itatoa matumizi na kiasi kilichobaki kitatakiwa kugawanywa
Sasa kama ulimpa nani sijui hiyo utajua wewe
Utatakiwa kutoa hilo gawio
Mkuu mbona unachekesha hakuna Sheria yeyote inayo mpangia mtu ni vipi atumie pesa yake na ndio maana ww tangu umezaliwa na kujua kutafuta pesa serikali haijawahi kukufuata na kukuuliza ni vipi unatumia pesa yako kunufaisha familia yako.
Sheria inacho kihitaji ni nyaraka za kisheria zinazo dhibitisha umiliki wa mali hizo basi hayo masuala ya sijui pesa zote za mshahara anazipeleka wapi sio kazi serikali wala mahakama.
 
Asante mwamba, umeeleza vizuri sana na kwa utulivu mkubwa. Nimeelewa vizuri sana na nimejua nochague upande upi
 
  • Wakili, umezungumzia Kuhusu kuandikisha Mali Kwa majina ya wengine eg Mama Ake Hakimi, na kusema kuwa Hana Mali yoyote (Hakimi), hiyo mahakama iliyoamua Hilo shauri ilitakiwa ijiulize inawezekana vipi mtu mwenye kipato Cha zaidi ya Bilioni 2 asiwe na Mali yoyote? Tuseme alikuwa anatumia zote? Mahakama ilitakiwa ijiulize Mama Hakimi ameweza vipi kumiliki ukwasi wa kutisha i.e hizo Mali kama Nyumba? , Mama Hakimi analipwa Bilioni ngapi , Hadi aweze kumiliki hizo Mali?, Mahakama ilitakiwa itoe amri kwa Hakimi atoe matunzo Kwa mke wake
  • Hapo Hakimi ametumia false pretense.
Kuna mahala hujaelewa mkuu, rudi usome tena. Jamaa kaeleza kuwa "ni ngumu kugawa mali zilizoandikwa jina la mtu mwingine" neno ni ngumu ndio lina uzito hapa. Yaana mahakama inakosa ushahidi wa moja kwa moja kuwa hii mali ni ya wana ndoa.
 
Kwann atoe matunzo Kwa mtalaka??

Hivi Kama mke WA hakimi ana Mali je wanaruhusiwa kugawana na mumewe baada ya taraka

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili mbona lilishaamuliwa na mahakama kuwa, kwakua Hakimi hana kitu, basi bibie anawajibika kulipa gharama zote za mahakama na baadae mahakama itaangalia kqma sheria itaruhusu kugawa mali za bibie
 
Back
Top Bottom