Songwe: Polisi wakamata walioanzisha kiwanda feki cha Sukari

#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Songwe limekamata kiwanda feki cha kutengeneza sukari katika eneo la Mlowo lililopo wilayani Mbozi, mkoani Songwe, pamoja na watuhumiwa 5 wakiwa na kilo 440 za sukari pamoja na vifungashio ambavyo vinadaiwa kutengenezwa nje ya nchi.

#ITVUpdatesView attachment 2439057

Hao jamaa hawatengenezi sukari ila ni wakwepa kodi,wanaingiza sukari kima gendo then wanatoa kwenye package yake na kuweka package inayopatikana tanzania.utakua na kiwanda bila shamba la miwa!?
 
Kabla ya kumtetea lazima tujue hiyo sukari inafaa kwa matumizi ya binadamu? Maana inakwenda kuingia mwilini isije kwenda kuharibu figo za watu. Watu wamevurugwa hawajali tena afya za wengine wanaangalia pesa tu. Kwanini asichukue vibali tbs /tfda kama hiyo sukari yake ni safe na haina madhara kwa binadamu
tfda ilishajifia zamani mkuu
 
Kabuni kiwanda cha sukari kakamatwa hii serikali ni ya hovyo sana Polisi mjitafakari
#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Songwe limekamata kiwanda feki cha kutengeneza sukari katika eneo la Mlowo lililopo wilayani Mbozi, mkoani Songwe, pamoja na watuhumiwa 5 wakiwa na kilo 440 za sukari pamoja na vifungashio ambavyo vinadaiwa kutengenezwa nje ya nchi.

#ITVUpdatesView attachment 2439064
Hapo angepewa hata incentive Ni sawa na mzee mmoja alibuni umeme wake na akasupply Kijiji kizima ilikua no masuala ya umeme kukata no mita za luku ila ukiamua unampa ata kiasi kwaajili ya uendeshaji

Tanesco wakamkamata kwamba anahujumu mapato yao, wakati hawajapeleka umeme area zile Yule mzee na meneja wa tanesco waliitwa ikulu na mwendazake na alipewa 20m Kama fidia ya usumbufu
 
#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Songwe limekamata kiwanda feki cha kutengeneza sukari katika eneo la Mlowo lililopo wilayani Mbozi, mkoani Songwe, pamoja na watuhumiwa 5 wakiwa na kilo 440 za sukari pamoja na vifungashio ambavyo vinadaiwa kutengenezwa nje ya nchi.

#ITVUpdatesView attachment 2439057
Labda kwasababu anatumia chapa ya watu Bwana Sukari.
Ukikutana na sukari yenye chapa ya bwana sukari mbovu mbovu dukani lawama zitaenda kwa wazalishaji wa Bwana Sukari.
Mkuu hiki ni kiwanda au anafanya kununua sukari gunia na kupack kwenye packet ndogo ndogo za Bwana Sukari.
Ila TZ wangeweka mazingira watu tuwe na viwanda vidogo vidogo tu home yani kama ambavyo kila baada ya nyumba kuna msanii basi kila baada ya nyumba kuna kiwanda home tunafyatua hata fekero za gucci
 
Yule mzee wa tabata aliyetengeneza mtambo wa kufua umeme bila maji wa la mafuta wala kelele aliishia wapi.
Mzre alijifanya mzalendo watu wanataka awauzie tech eti ye ooh nataka ifaidishe nchi yangu, hapa hakuna nayejali.
 
Ilibidi apige ela aondoke
 
Sasa mtu aibuke tu aanze kuzalisha bidhaa bila utaratibu aachwe kweli. Hii ni nchi ina taratibu zinatotakiwa kufatwa unapotaka kufanya jambo. Tena ukizingatia kitu kama sukari ni kitu kinachoenda kuingia miilini mwa watu, tuna uhakika gani kama hiyo sukari ina viwango bora kwa ajili ya matumizi ya binadamu?!! Jaribu kufkiria. Nchi ina watu wengi sana, kama kila mtu akisema afanye chake bila utaratibu, hapata kalika
 
Kabla ya kumtetea lazima tujue hiyo sukari inafaa kwa matumizi ya binadamu? Maana inakwenda kuingia mwilini isije kwenda kuharibu figo za watu. Watu wamevurugwa hawajali tena afya za wengine wanaangalia pesa tu. Kwanini asichukue vibali tbs /tfda kama hiyo sukari yake ni safe na haina madhara kwa binadamu
Ndiyo serikali imsaidie. Haga huko Ulaya bunifu zak zimechukua muda kiwa refined.

Kama kila ubinifu unapigwa vita. Mtakuwa lini na vitu vyenu mlivyobuni?
Mtu akitengeneza gobole anakamatwa...lini sasa mtakuwa na lockheed martin yenu? Hawa watu wasaidie na kuelekezwa kufuata tafatibu siyo kukamatwa na kufilisiwa au kufungwa
 
#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Songwe limekamata kiwanda feki cha kutengeneza sukari katika eneo la Mlowo lililopo wilayani Mbozi, mkoani Songwe, pamoja na watuhumiwa 5 wakiwa na kilo 440 za sukari pamoja na vifungashio ambavyo vinadaiwa kutengenezwa nje ya nchi.

#ITVUpdatesView attachment 2439057
wapigwe faini halafu wapime sukari kama haina madhara wafate taratibu wasajiliwe .
 
Huyu ananunua Sukari ya Zambia kwa magendo kisha anaiweka kwenye vifungashio vya Sukari ya Tanzania kwa hiyo huyu ni mlanguzi
Apo mlowo wanalima miwa sana ko sizani kama ni hivyo ingekua ivo angejenga tunduma uko
 
Polisi na mleta uzi wote mapoyoyo kuchukua sukari aina flani na kuiweka katika kifungashio cha Kilombero Sugar ni feki? mnatakiwa mjiongeze huyo kachukua sukari huko aliko itoa kaweka kifungashio ambacho sio cha sukari husioka saasa kama ingekuwa sukari feki tungeambiwa labda haitokani na miwa labda inazalishwa na katani etc etc kikubwa hapo ni kukiuka taratibu na kukwepa kodi, labda kama ingethibitika bila shaka kuwa sukari hiyo ni ya wanyama ama ya kutengenezea sabuni. POLISI ni wapuuzi wanahangaikaga na wapinzani tu hakuna wanachojua, kuna kamanda mmoja sijui wa mkoa gani anatoaga taarifa kwa waandishi wa habari kama anatangaza mpira, yani sijui darasa la ngapi yule mtu
 
Serikali ituambie vipaji kama hivi vinaendelezwaje?
Vipaji vya kutengeneza vyakula vya watu?? Unajua anatumia ingredient gani kutengeneza sukari?? Anatumia vifaa gani?? Na je packaging yake anatumia brand gani,isije kuwa anazalisha sukari halafu anaweka package ya viwanda vys wenzake kama bwana sukari au azam hilo ni kosa pia,kama anatumia brand yake amefuata taratibu?? Dunia nzima njia pekwe ya kuzalisha sukari ni kupitia miwa,yy kama hana shamba la miwa atuambie sukaro yskw anaizalishaje asilishe watu vitu vya ajabu!!
 
Labda kwasababu anatumia chapa ya watu Bwana Sukari.
Ukikutana na sukari yenye chapa ya bwana sukari mbovu mbovu dukani lawama zitaenda kwa wazalishaji wa Bwana Sukari.
Mkuu hiki ni kiwanda au anafanya kununua sukari gunia na kupack kwenye packet ndogo ndogo za Bwana Sukari.
Ila TZ wangeweka mazingira watu tuwe na viwanda vidogo vidogo tu home yani kama ambavyo kila baada ya nyumba kuna msanii basi kila baada ya nyumba kuna kiwanda home tunafyatua hata fekero za gucci
Sukari huzalishqa kutoka kwnye miwa,wazalishaji wote wa sukari wana mashamba ya miwa,ndo maana bakhresa amelima shamba lake miaka 3 bagamoyo ndo ameanza uzalishaji,huyo bwana shqmba lake lipo wapi??
 
Kabla ya kumtetea lazima tujue hiyo sukari inafaa kwa matumizi ya binadamu? Maana inakwenda kuingia mwilini isije kwenda kuharibu figo za watu. Watu wamevurugwa hawajali tena afya za wengine wanaangalia pesa tu. Kwanini asichukue vibali tbs /tfda kama hiyo sukari yake ni safe na haina madhara kwa binadamu
Waliowatuma wakamataji, ndo hao hao wanaotakiwa kusema kama inafaa kwa matumizi ya binadamu au la.!!
Lisu alishawahi kukataa kupimwa mkojo, unajua sababu?
 
Sasa umeshakiita feki, kwanini asikamatwe, muwapumzishege Tanpol wawatu.
 
Back
Top Bottom