Songwe: Polisi wakamata walioanzisha kiwanda feki cha Sukari

Huyu mimi namwita mjasilimali mwenye kutumia nembo au jina la company yake ndogo. Akitegemea baadae awe na kampuni kubwa
miwa ananunua wapi, acheni kubuni atakuwa naingiza kutoka nje kimagendo. Kuzalisha sukari ni jambo rahisi kihivyo
 
Sasa mtu aibuke tu aanze kuzalisha bidhaa bila utaratibu aachwe kweli. Hii ni nchi ina taratibu zinatotakiwa kufatwa unapotaka kufanya jambo. Tena ukizingatia kitu kama sukari ni kitu kinachoenda kuingia miilini mwa watu, tuna uhakika gani kama hiyo sukari ina viwango bora kwa ajili ya matumizi ya binadamu?!! Jaribu kufkiria. Nchi ina watu wengi sana, kama kila mtu akisema afanye chake bila utaratibu, hapata kalika
Ni kweli kabisa, ni viongozi tu wa serikali ndio wanaoruhusiwa kufanya vitu bila utaratibu, sio kila mtu
 
Kabla ya kumtetea lazima tujue hiyo sukari inafaa kwa matumizi ya binadamu? Maana inakwenda kuingia mwilini isije kwenda kuharibu figo za watu. Watu wamevurugwa hawajali tena afya za wengine wanaangalia pesa tu. Kwanini asichukue vibali tbs /tfda kama hiyo sukari yake ni safe na haina madhara kwa binadamu
Hii sukari hatengenezi yeye isipokuwa anajumua Zambia then anakuja kuipaki kwenye vifungashio vya Tanzania ili auze maana akiacha na vifungashio vya Zambia anakamatwa
 
Kiwanda. Feki ndio kiwanda gani?? Sema kiwanda kisochofata taratibu za kisheria kuzalisha na kutoa huduma.
Ndio serikali inataka kodi inataka tozo inataka uthibiti na udhibiti, yeye kakwepa vyote hivyo hilo ndio kosa lake, ila sio kwamba ni kiwanda Feki
 
Hii sukari hatengenezi yeye isipokuwa anajumua Zambia then anakuja kuipaki kwenye vifungashio vya Tanzania ili auze maana akiacha na vifungashio vya Zambia anakamatwa
Ndio alipie kodi na tozo na ajisajiri TRA kwa Biashara hio bila hivyo anaonekana km haramia tu wa Biashara mboni wengine wanafuata utaratibu hawasumbuliwi?
 
Huyu ananunua Sukari ya Zambia kwa magendo kisha anaiweka kwenye vifungashio vya Sukari ya Tanzania kwa hiyo huyu ni mlanguzi
Nimeanza kuelewa..sijaona mazingira ya kiwanda hapo.
 
Hii sukari hatengenezi yeye isipokuwa anajumua Zambia then anakuja kuipaki kwenye vifungashio vya Tanzania ili auze maana akiacha na vifungashio vya Zambia anakamatwa
Serikali ipo serious sana kuhakikisha watu wake wanakuwa na maisha magumu. Yaani haiangalii hao wanunuzi watavyoathirika kwa mwokozi wao kukamatwa. Kama sukari ya Zambia ni bei rahisi - serikali si iwahimishie Zambia watu wake
 
Sasa unasema serikali ya hovyo hapo hapo unasema jeshi la police limesha wakamata 🥹🥹🥹🥹 u hovyo uko wapi?[emoji2959]
 
#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Songwe limekamata kiwanda feki cha kutengeneza sukari katika eneo la Mlowo lililopo wilayani Mbozi, mkoani Songwe, pamoja na watuhumiwa 5 wakiwa na kilo 440 za sukari pamoja na vifungashio ambavyo vinadaiwa kutengenezwa nje ya nchi.

#ITVUpdatesView attachment 2439057
lazima pia tuzikumbuke afya zetu, tukishangilia watu wanaoanzisha viwanda bubu vya vykaula badae tukianza kuathirika tutakuwa wa kwanza tena kuilaumu serikali. kama ni mjasiriamali , ana ujuzi wa kuanzisha kiwanda kidogo kama hicho angeenda SIDO,TIRDO, n.k wangempa suport nzuri tu.
 
Serikali ipo serious sana kuhakikisha watu wake wanakuwa na maisha magumu. Yaani haiangalii hao wanunuzi watavyoathirika kwa mwokozi wao kukamatwa. Kama sukari ya Zambia ni bei rahisi - serikali si iwahimishie Zambia watu wake
pia serious sana kuhakikisha afya za watz zinalindwa, huwezi kuachia uholela huu eti ili mradi tu, sukari toka zambia ni bei rahisi!!! unaijua kainunua wapi?!?, pengine hata huko ilikotoka ilishapigwa marufuku. iacheni serikali itimize wajibu wake kwa manufaa yetu wote, hivi kila mtu akiruhusiwa kuanzisha kiwanda cha chakula bila kufuata utaratibu unadhani itakuwaje?!? michele matani na matani inamwagwa inapogundulika haifai kwa matumizi ya binadamu, sembuse visukari hivyo!!!!
 
miwa ananunua wapi, acheni kubuni atakuwa naingiza kutoka nje kimagendo. Kuzalisha sukari ni jambo rahisi kihivyo
Viongozi wizi wananchi unataka wawe nani? Hii nchi bila ya dhuluma,wizi,utapeli na mission town huwezi kuishi.
 
Huyo mtu asaidiwe badala ya kukamatwa
Huko mbozi kila baada ya miaka kadhaa huwa wanabuni vitu halafu wanaishia kukamatwa,badala ya kuwaita wabunifu na kuwawezesha
 
pia serious sana kuhakikisha afya za watz zinalindwa, huwezi kuachia uholela huu eti ili mradi tu, sukari toka zambia ni bei rahisi!!! unaijua kainunua wapi?!?, pengine hata huko ilikotoka ilishapigwa marufuku. iacheni serikali itimize wajibu wake kwa manufaa yetu wote, hivi kila mtu akiruhusiwa kuanzisha kiwanda cha chakula bila kufuata utaratibu unadhani itakuwaje?!? michele matani na matani inamwagwa inapogundulika haifai kwa matumizi ya binadamu, sembuse visukari hivyo!!!!
Mbona tunakula unga fake Hadi andazi linakosa rangi
 
Kiwanda. Feki ndio kiwanda gani?? Sema kiwanda kisochofata taratibu za kisheria kuzalisha na kutoa huduma.
Feki ni kiwanda chochote kinachotengeneza bidhaa ambayo haijathibitishwa na TBS au mamlaka ya chakula na dawa

Unajuaje kuwa hiyo sukari yafaa kwa matumizi ya binadamu?

Una vipimo vya kuthibitisha? Halafu wewe tukuamini kama nani unatambuliwa wapi kama unatengeneza sukari yenye sumu ya kuua watu uachwe tu?
 
Kuna mtu aliyekufa kwa kula hiyo sukari?
 
pia serious sana kuhakikisha afya za watz zinalindwa, huwezi kuachia uholela huu eti ili mradi tu, sukari toka zambia ni bei rahisi!!! unaijua kainunua wapi?!?, pengine hata huko ilikotoka ilishapigwa marufuku. iacheni serikali itimize wajibu wake kwa manufaa yetu wote, hivi kila mtu akiruhusiwa kuanzisha kiwanda cha chakula bila kufuata utaratibu unadhani itakuwaje?!? michele matani na matani inamwagwa inapogundulika haifai kwa matumizi ya binadamu, sembuse visukari hivyo!!!!
Serikali ni pamoja na huyo aliyekamatwa, yeye anawasaidia watanzania wenzake, jukumu ambalo lilikuwa la viongozi wa serikali na wamefeli, anawasaidia kwa kuwauzia sukari kwa bei nafuu, walioshindwa kazi badala ya kufurahi na kumpongeza wao wanakuja kumkata na kuanza kuleta dhana dhahania kibao kama hizo zako za unajuaje haina sumu au imepigwa marufuku nk...

Acheni watu wasaidie watanzania wenzao ambao hamuwajali kwa lolote.
 
Hao jamaa hawatengenezi sukari ila ni wakwepa kodi,wanaingiza sukari kima gendo then wanatoa kwenye package yake na kuweka package inayopatikana tanzania.utakua na kiwanda bila shamba la miwa!?
Na hata ukiwa na shamba la miwa, gharama ya ''kupika'' sukari ni kubwa kulinganisha na faida. Ingekuwa ni rahisi kutengeneza nchi hii kusingekuwa na tatizo la sukari.
 
Serikali ni pamoja na huyo aliyekamatwa, yeye anawasaidia watanzania wenzake, jukumu ambalo lilikuwa la viongozi wa serikali na wamefeli, anawasaidia kwa kuwauzia sukari kwa bei nafuu, walioshindwa kazi badala ya kufurahi na kumpongeza wao wanakuja kumkata na kuanza kuleta dhana dhahania kibao kama hizo zako za unajuaje haina sumu au imepigwa marufuku nk...

Acheni watu wasaidie watanzania wenzao ambao hamuwajali kwa lolote.
labda mtafute nchi yenu ambayo haitakuwa na utaratibu. hakuna nchi yoyote duniani inaendeshwa bila utaratibu. yaani mtu aje na petroli yake kutoka huko ajuako yeye aanza kuiuza mtaani bila kufuata utaratibu eti aachiwe tu!!!! hiyo haiwezekani!!!!
 
Back
Top Bottom