Special thread: Mgogoro kati ya Urusi na NATO
v
Wao wa Rusia hawafi?

Ni kwamba West wanaenda kwa mahesabu katika hii vita. Kubwa zaidi ni kumdumaza Putin kiuchumi na hilo haliwezi kutokea kwa ghafla.
Subiri miaka 5 ijayo uone vilio kutoka kwa Putin.

arl
raha ya ngumi ni kutazama na sio kuingia ulingoni
 
China imeweka wazi kuwa haitahudhuria mkutano wa Ukraine Peace Conference utakaofanywa nchini Switzerland June 15-16, 2024

Wajumbe 160 wamealikwa kwenye mkutano huo kutoka nchi za G7, G20 na BRICS. Lakini Russia haikualikwa.

Sababu ya China kukataa kuhudhuria mkutano huo ni kutoalikwa kwa Russia.

Wanadiplomasia wa China wanasema ikiwa Russia wangealikwa kwenye mkutano huo basi kungekuwa na ushiriki sawa wa pande zote na majadiliano ya haki.
Saudi Arabia nayo yachomoa kwa sababu hizo hizo za uchina
 
Putin akijaribu kutumia nukes tu ameisha,hata tu akijaribu kutumia hizo tactical nukes mwisho wake ndio utakua umefika.
Ila Marekani akijaribu kutumia silaha za nyukilia ndio atabaki salama?
Kwa hiyo kwako wewe akitumia Marekani ni halali,lkn akitumia Urusi ni haramu.
Hivi nyinyi mmekula maharage ya wapi?
Kwa taarifa Yako Urusi sio Japan ukae ukijua hilo.
 
NATO (USA) wapepigana kwa kificho, wakashindwa wameona wajitokeze kiume.
Hivi karibuni Biden aliapa kushughukikia uchumi wa Urusi kivingine baada ya mkakati wa kutumia Ukraine kushindwa. Naona mbinu inawekwa hadharani.
Binadamu kiumbe dhaifu anapotos maelekezo yansyopelekea Vigo vya wengine ili hali yeye yupo kwenye kasri anagonga nvinyo.
Hakuna kitu kimewachanganya wamarekani kama umoja wa Brics jinsi unavyokua kwa Kasi kiasi Cha Kupelekea kuua USD.
Wamarekani wamepanik sana kuona USD Yao inaenda kuanguka.
Kwa kifupi hakuna namna ya kuiokoa.
Jambo jingine ni kwamba Dunia hivi Sasa haiiheshimu Tena Marekani wala haiiogopi Tena.
Hicho kitu USA anakiwaza sana.
USA anawaza anguko lake.
 
Uzi huu unaangazia kile kinachoendelea kuhusu mgogoro ulioibuka sasa wa NATO na Russia katika vita vya Ukraine.

Ikumbukwe kuwa katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, alitaka silaha za misaada kwa Ukraine sasa zianze kutumika kushambulia moja kwa moja ndani ya mipaka ya Russia hasa miltary targets. Kitaalamu mashambulizi haya yanaitwa long range strikes.

Tangu NATO wakubaliane kuhusu hilo, dunia ilikuwa ikisubiria tamko kutoka Moscow.

Hatimaye aliyewahi kuwa raisi wa taifa hilo ambaye kwa sasa ni deputy chief of Russia’s Security Council, Dmitry Medvedev amezungumza haya kufuatia tamko la NATO

Medvedev: "Nchi za Magharibi, ambazo zinadaiwa kuidhinisha matumizi ya silaha zao za masafa marefu kwenye eneo la Urusi (bila kujali kama inahusu sehemu za zamani au mpya za nchi yetu), lazima zielewe yafuatayo:

1. Vifaa vyao vyote vya kijeshi na wanajeshi wanaopigana dhidi yetu vitaharibiwa katika eneo la Ukrainia na katika maeneo ya nchi nyingine ikiwa mashambulizi yataanzishwa kutoka huko dhidi ya eneo la Urusi.

2. Urusi inatambua kwamba silaha zote za masafa marefu zinazotumiwa na Ukraine kwa sasa zinadhibitiwa moja kwa moja na wanajeshi wa NATO. Huu sio msaada wa kijeshi bali ni kushiriki katika vita dhidi yetu.

3. Msaada wa taifa moja moja kama huo kutoka kwa nchi za NATO dhidi ya Urusi, iwe ni kudhibiti makombora yao ya masafa marefu au kutuma wanajeshi Ukraine, itaongeza mzozo huu. Ukraine na washirika wake watakabiliwa na jibu la nguvu.

4. Baadhi ya maafisa wa NATO wanazungumza kwamba Urusi haitatumia silaha za nyuklia zisizo za kimkakati dhidi ya Ukraine achilia mbali nchi za NATO. Maisha yanaweza kuwa mabaya zaidi kuliko mawazo yao ya kipuuzi."


Kuna kauli nzito ambayo ameiotoa kama red alert
"West risks miscalculating the chances of nuclear weapons being used."

Tumebaki tukisubiri hatma na kupata majibu ya maswali haya:

Je, NATO wataogopa baada ya kauli hizo thabiti kutoka kwa Russia na kuachana na mpango wa silaha zao zitumike kushambulia ndani ya mipaka ya Russia?

Silaha za NATO zikitumika kushambulia ndani ya mipaka ya Russia, je, Russia watafanya kama alivyosema Medvedev?

Je, tutapata maana ya hii kauli ya Medvedev "West risks miscalculating the chances of nuclear weapons being used."

Je, itakuwa mwanzo wa vita kuu ya tatu ya dunia na kushuhudia matumizi ya silaha hatari za nyuklia?

Acha tuone yatakayojiri kwa updates mbalimbali.



VIONGOZI WA NCHI ZA MAGHARIBI WAKUTANA MADRID, SPAIN KUFANYA MKUTANO WA SIRI MOJA YA AJENDA KUIZUNGUMZIA RUSSIA

Wakati sintofahamu ikiendelea kati ya Russia na NATO na suala la geopolitical kati ya mataifa mawili yenye uchumi mkubwa duniani Marekani na China likiendelea kufukuta.

Wawakilishi wachache walialikwa kutoka Marekani, nchi wanachama wa NATO zilizopo Ulaya na Ukraine walikutana tarehe May 30–June 2, 2024 katika jiji la Madrid, kwenye hotel ya Eurostars Suites Mirasierra.

Mkutano unaisha leo lakini hakuna mainstream media yoyote imeutangaza, ndio ujue usiri wa mkutano huu ulivyo mkubwa. Kwani waalikwa huapa kwamba watahakikisha yaliyojadiliwa yanabaki kuwa siri.

Mkutano huu hufanywa kila mwaka tangu mwaka 1954 ulipoanzishwa. Unaitwa the Bilderberg Meeting. Wajumbe huwa ni political and business elites.

Ni mkutano wa siri ambao hakuna nafasi ya waandishi wa habari kualikwa hivyo hakuna taarifa yoyoye itakayotolewa baada ya mkutano huo na vyombo vya habari.

Ajenda za mkutano wa mwaka huu zilikuwa:
●Russia
●China
●Middle East
●Ukraine and the world
●State of AI
●AI Safety
●Changing Faces of Biology
●Climate
●Future of Warfare
●Geopolitical Landscape
●Europe's Economic Challenges
●US Economic Challenges
●US Political Landscape

Kwa nini Russia, China na Middle East ziwe ajenda kwenye mkutano huo?

Tuuachie muda nafasi tutapata jibu la swali hilo.

Ikumbukwe pia hivi karibuni raisi wa China aliwaalika viongozi wa nchi za Kiarabu jijini Beijing kwenye mkutano wa China-Arab Forum.

Pia ni ndani ya kipindi kisicho kirefu Xi na Putin walifanya mazungumzo jijini Beijing.

Miongoni mwa wahudhuriaji waliolikwa kwenye mkutano huu wa siri ni pamoja na:

●US Deputy Treasury Secretary Wally Adeyemo
●US Deputy National Security Advisor Jonathan Finer
●Finnish President Alexander Stubb ●European Council President Charles Michel
●NATO Secretary General Jens Stoltenberg,
●Prime ministers of the Netherlands and Estonia
●Foreign ministers of Spain, Ukraine, Sweden, and Poland
●The deputy prime minister of Ireland.

From the world of business:
●Pfizer CEO Albert Bourla
●BP CEO Murray Auchincloss
●Former Google CEO Eric Schmidt
●Several AI executives from Google, Microsoft, and Anthropic
PBC
Umeongea kishabiki Sana.... Russia Hana jipya fala mmoja
 
Wao wa Rusia hawafi?

Ni kwamba West wanaenda kwa mahesabu katika hii vita. Kubwa zaidi ni kumdumaza Putin kiuchumi na hilo haliwezi kutokea kwa ghafla.
Subiri miaka 5 ijayo uone vilio kutoka kwa Putin.

a
mkuu kudumaza afrika wanaweza, ila Russia hawawezi.....
yule amebadilisha masoko yake, anao watalaamu wa kuzalisha bidhaa ndani kwake, ana malighafi zote muhimu.....

saizi europe uzalishaji wa viwandani umeshuka, subiri utakapoanza kupamba uone watakavyorudi russia kununua gesi na mafuta!
 
Ikiwa nchi zitaamua kushiriki moja kwa moja katika mzozo huo, tunaweza kufanya vivyo hivyo - Putin
 
Katibu mkuu wa UN hatahudhuria mkutano wa wa Ukraine Peaceful Conference nchini Switzerland

Walianza China kukataa kuhudhuria sasa India, Saudi Arabia the list goes on na sasa UN chief secretary
 
Back
Top Bottom