Uchaguzi 2020 SPECIAL THREAD: Taarifa za Kampeni na Sera za Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda

Uchaguzi 2020 SPECIAL THREAD: Taarifa za Kampeni na Sera za Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda

View attachment 1554892

Mheshimiwa sana umetangaza kua katika sera zako moja wapo ambayo ndiyo sera kuu ni kugawa ubwa bwa. Ulisema pia wakati wa kampeni utagawa ubwa bwa huo kwa wote watakaokuja kusikiliza sera zako.

Mheshimiwa, ninaomba kazi ya kupika ubwa bwa wa kampeni. Pia ninajitolea kuosha masufuria ili niwe ninaondoka na matandu.

Niko tayari kusafiri Tanzania yote iwapo mume wangu Asprin ataniruhusu.
Niwie radhi my darling. Ruhusa imekataliwa...

Kaa nyumbani ulee watoto
 
Mzee Hashim Rungwe anaharibu kipindi anahojiwa anamkaripia na kumshambulia bi Farhia Mido.

Bi Farhia anaonesha kabisa hayupo mchezoni anaboreka na Mzee Rungwe anavoongea na vile anavyomkaripia dada yetu.

Farhia : Vipi mzee chama chako inaonekana kinaibuka wakati wa uchaguzi, kwanini hii ?

Rungwe ; Ah vipi bwana wee,unauliza hujui kama tulizuiliwa siasa hujui ?

Dah hatari kweli
 
Habari wadau.

Mgombea wa Urais wa CHAUMA ndugu Hashimu Rungwe alikuja na hoja ya chakula kwa watoto wa shule na wagonjwa hospitalini.

Ukimsikiliza ana mantiki,imagine watoto wa shule kukaa shule masaa takribani 10 huku hajala chochote sijui mtoto wa hivi ataachaje kuwa na utapiamlo na kudumaa kiakili na kimwili. Wote mnakumbuka ishu ya vijana wa Taifa stars kule Afcon, Watanzania tulionekena kuwa wafupi na wenye vimiili vidogo vidogo hivyo kushindwa kuhimili mashindano mbalimbali.

Leo hii uwezo wa watu kufikiri ni mdogo sana kutokana na lishe duni,uzoefu unaonesha kwamba mtoto huanza kudumaa kimwili na kiakili pindi akiachishwa kunyonya na kuanza kulishwa chakula ambacho sio balanced diet kutokana na maisha ya kuunga unga na kubabaisha ya watanzania wengi.

Naomba vyama makini hasa vya upinzani viichukue hii hoja na kuinadi kwa wananchi maana ni hoja ya msingi sana na yenye mashiko ikizingatiwa kwamba hapo awali miaka ya nyuma watoto walikua wanalishwa mashuleni na wagonjwa na wauguzi kupewa chakula.

Badala ya kila siku kunadi madaraja sijui barabara nk mambo ambayo ni wajibu wa serikali na bunge kuyaratibu kwenye bajeti ya kila mwaka,vyama vije na policy direction kwenye sekta za afya na lishe kama anavyofanya Mzee Rungwe, technicalitie za namna ya kuzitekeleza ndio itakuwa wajibu wa serikali iliyonadi sera husika. Watanzania tuache kuichukulia siasa kama mizaha ya utani wa jadi wa yanga na simba,siasa ni hatima ya maisha yetu. Tutafakari na tuchukue hatua.
 
Tatizo mnamchukulia kama muigizaji but ana point muhimu sana kuhusu lishe ya watoto wa shule na wagonjwa.Pili katoa muelekeo wa kisera hasa kwenye sekta ya afya na lishe.

Jambo jingine amesema haingii akilini eti sera au ilani kuzungumzia madaraja na vitu kama hivyo kwamba hiyo ni wajibu wa serikali kufanya na, miradi inapangwa na serikali na kisha kuletwa bungeni kujadiliwa na bunge
 
Back
Top Bottom