Uchaguzi 2020 SPECIAL THREAD: Taarifa za Kampeni na Sera za Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda

Uchaguzi 2020 SPECIAL THREAD: Taarifa za Kampeni na Sera za Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda

Huyu jamaa anaanza lini kampeni na wapi? ili ninunue kabisa ndizi mbivu na pilipili, nikajipatie sahani yangu ya ubwabwa
 
Spunda, hapo nimekuelewa, ati sera za ubwawa za Spunda....!
😡😡😡
Asante mkuu....[emoji23][emoji23][emoji23]
IMG-20200830-WA0000.jpg
 
Huyu Rungwe anawadharau watanzania kwa kuwaona wananjaaa ya ubwabwa chama kilitakiwa kifutwe hakina sera wanakula ruzuku
Usichokipenda wewe, kuna watu wanakipenda.Ni vyema kufatilia na kuzijua sababu zinazoweza kupelekea chama kufungiwa kabla ya kuropoka hapa, hii inatufanya tukuchukulie Kama kiazi tu.
 
Hawajui watanzania huyo..ubwabwa wake wa nazi watu watakula na hawatompa kura.
 
Huyu jamaa anaanza lini kampeni na wapi? ili ninunue kabisa ndizi mbivu na pilipili, nikajipatie sahani yangu ya ubwabwa
Ameshasema watu wasihangaike na ndizi, pilipili sijui vijiko, kila kitu utakikuta huko. Anasema sera zake ni sera zinazotekelezeka, siyo sera za ahadi.
 
Mkuu bila kula huwezi kujenga taifa imara.Hata kujistawisha mwenyew unakuwa huwezi kabisa.Ama umesahau ule msemo kuwa mwili haujengwi kwa tofali.VIVA RUNGWE
 
Ameshasema watu wasihangaike na ndizi, pilipili sijui vijiko, kila kitu utakikuta huko. Anasema sera zake ni sera zinazotekelezeka, siyo sera za ahadi.
Hahah Ila huyu jamaa inabidi anogeshe kampeni kwa kuweka sahani kadhaa za ubwabwa kwa wachache watakaowahi, ili kuongeza mbwembwe
 
Ila hiki kama chama nadhani ilani hii iliundwa na kamati yao ya almashauri kuu ikiwashirikisha wajumbe, kwa hiyo kuna jopo la watu walikaa wakafikia kuamua hili [emoji38]

Sema nini , kafuata demokrasia, uhuru na haki zake kama binadamu....
 
Hivi wewe ukiambiwa nipigie kura ili ule ubwabwa wa bure, mtu huyo anakuchukuliaje?
Nawe kweli utampiga, nawe tukuelewe vipi ?

..Hashim Rungwe ameshindwa kutafuta namna bora ya kufikisha ujumbe wake kwa wananchi.

..lakini ni ukweli kwamba kuna tatizo la LISHE ktk kaya nyingi hapa Tanzania.

..wakati wa Mwalimu Nyerere kulikuwa na kampeni ya "MTU NI AFYA" na suala la lishe lilikuwa moja components za kampeni hiyo.
 
Kuna sehemu nyingi tu sera za ubwabwa haziuziki!
Watu wanamwona huyu Spunda ni msanii tu, akawatapeli waswahili huko Dar!
Hapo ni Ilomba, Mbeya.
IMG-20200831-WA0001.jpg
 
Mwalimu aliwahi kusema, mtu akikuambia kitu cha upuuzi, nawe ukajua ni upuuzi na usichukue hatua yoyote, mtu huyo amekudharau sana.
Hiki ndicho Rungwe anafanya, kuwadharau Watanzania na sera za ubwabwa.
Ukiwaona watu kwenye kampeini zake wanakuja kula ubwabwa kuna picha fulan hiv ww kwa akili yako ndogo uwez kuuona maana yake watunwana dhiki hata za vyakula majumban mwao

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Kuna sehemu nyingi tu sera za ubwabwa haziuziki!
Watu wanamwona huyu Spunda ni msanii tu, akawatapeli waswahili huko Dar!
Hapo ni Ilomba, Mbeya.
View attachment 1554827

..kaka huko Mbeya vipi?

..hebu tuhabarishe kinachoendelea huko kipindi hiki cha uchaguzi. ni muda mrefu hatujasikia kutoka kwako.

..kuna miaka wadau wa Mbeya mlikuwa mnalichangamsha sana jukwaa letu, I really miss those days.
 
1598915624745.jpeg

Mheshimiwa sana umetangaza kua katika sera zako moja wapo ambayo ndiyo sera kuu ni kugawa ubwa bwa. Ulisema pia wakati wa kampeni utagawa ubwa bwa huo kwa wote watakaokuja kusikiliza sera zako.

Mheshimiwa, ninaomba kazi ya kupika ubwa bwa wa kampeni. Pia ninajitolea kuosha masufuria ili niwe ninaondoka na matandu.

Niko tayari kusafiri Tanzania yote iwapo mume wangu Asprin ataniruhusu.
 
Back
Top Bottom