_____________________
_Na Godfrey Kassim, PhD (Sayansi ya Chakula)_
______________________
Tulivyokua wadogo tulikua tukikatazwa kula sehemu yoyote isipokua nyumbani tu. Hayo ndio mafundisho halisi ya kiafrika tuliyorithishwa na wahenga.
Nilipoanza kusomea elimu ya sayansi ya chakula nikafahamu kwanini wazee wetu walikua wapo sahihi.
Wataalamu wa elimu ya chakula husema "You Are What You Eat" yaani chakula kina nafasi kubwa katika kumjenga mwanadamu.
Wataalamu wamebaini kwamba chakula hujenga afya ya mwili na akili sambamba na kuathiri tabia ya mwanadamu.
Kuna baadhi ya vyakula hudhoofisha akili hivyo kuathiri ufaulu katika elimu.
Vipo vyakula vingine vinadhoofisha afya ya uzazi na kusababisha ugumba hivyo kupunguza idadi ya watu.
Vipo vyakula vinavyochangia kupunguza/kufuta aibu hivyo kuchangia kwenye mporomoko wa maadili unaosababisha ongezeko la uhalifu.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba vyakula vinavyotolewa mashuleni si salama kwa mtoto kwasababu hubeba madhara mengi sana.
Kuna visa vingi vya vifo mashuleni katika nchi mbalimbali ulimwenguni vinavyosababishwa na kula chakula cha shuleni.
Sambamba na hayo, watafiti wanaeleza kwamba usalama wa chakula hupungua katika harakati za kuandaa chakula cha watu wengi kutokana na uangalifu kuwa mdogo.
Hata hivyo, ni rahisi kwa muhalifu kufanya hujuma ya kudhuru wanafunzi endapo chakula kinaandaliwa mashuleni.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Stanford huko Uingereza mnamo mwaka 2015 unaonesha kwamba chakula cha mashuleni ni hatari kwa sababu huwa na kiwango cha sumu hatari (
Stanford study indicates school meals may expose children to unsafe levels of BPA).
TUREJEE MAFUNDISHO YA WAHENGA*