Uchaguzi 2020 SPECIAL THREAD: Taarifa za Kampeni na Sera za Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda

Uchaguzi 2020 SPECIAL THREAD: Taarifa za Kampeni na Sera za Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda

Tatizo mnamchukulia kama muigizaji but ana point muhimu sana kuhusu lishe ya watoto wa shule na wagonjwa.Pili katoa muelekeo wa kisera hasa kwenye sekta ya afya na lishe.
Jambo jingine amesema haingii akilini eti sera au ilani kuzungumzia madaraja na vitu kama hivyo kwamba hiyo ni wajibu wa serikali kufanya na, miradi inapangwa na serikali na kisha kuletwa bungeni kujadiliwa na bunge
Pale nimemuelewa sana mzee rungwe.

Yani haiwezekani mtu uahidi utajenga madaraja,utajenga mashule,utajenga masoko.

Sasa haya si ndo wajibu hasa wa serikali wafanye hata kama hawakuahidi ?
Mzee namuelewa ila tu wengi hatuwezi kumuelewa vizuri.
 
Hahhahahahaha watu watakwea makruza mazuri tu
"Kipaumbele changu wananchi wapate ajira, hakuna watu kuzubaa barabarani..., kilimo ndio chanzo cha uchumi wa nchi hii..., wakilima watapata na viwanda, kwanza watoto watakula chakula cha maana" - Hashimu Sipunda Rungwe Mgombea wa kiti cha urais kupitia CHAUMA

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Wanaombeza Rungwe acha wammbeze ila sera yake itakuja kukumbukwa na vizazi vijavyo na itafanyiwa kazi ni sera nzuri na yenye tija kwa future ya jamii hasa watoto wa shule.
 
Kilimo cha mpunga kila kata 🤣anamuuliza mwandishi badala ya yeye kujieleza hahahahahahah burudaaaaaani ataziuza ndege zote watu wapige ubweche mpunga hahahaa,inaelekea mwandishi kachukia mzee rungwe ajatinga na hotpot la ubweche hahaha wa clauds walipiga ubweche huku wakimhoji
 
Bila sera endelevu kuku wa kienyeji wataisha ndani ya siku 100 afafanue namna atakavyokuza kilimo na ufugaji.
 
Hizo issue za kujenga ni kazi za taasisi na wizara kila mwaka zinatakiwa zipeleke bajeti yao bungeni zipitishwe, watu tunaompenda JPM tunamwambia ukweli, Sasa hivi anatakiwa atuahidi Mambo ya utawala ya serikali atayasimamiaje?

Issue za mivuke awaachie mawaziri, kwa mfano hatakiwi kuongelea issue ya barabara moja anatakiwa aseme ntashughulia mipango ya miundo mbinu ya kisasa, umeme wa uhakika mpaka vijijini, elimu ya kiwango Cha ushindani na regulate za ada zisimulemee mwananchi ataona watu watavyopiga makofi.
 
Mzee Hashim Rungwe anaharibu kipindi anahojiwa anamkaripia na kumshambulia bi Farhia Mido.

Bi Farhia anaonesha kabisa hayupo mchezoni anaboreka na Mzee Rungwe anavoongea na vile anavyomkaripia dada yetu...
mzee rungwe anaonekana ni mtu msomi na mwenye ukwasi
 
20200901_134946.jpg
 
Alipoulizwa juu ya kuibuka kwenye uchaguzi pekee,akajibu kuwa kwani wewe(mwandishi) hujui tumezuliwa kufanya siasa?

Mwandishi akabadili mada ghafla. Kutokufanya kazi wiki moja ni hasara kubwa kwa media company.
 
Pale nimemuelewa sana mzee rungwe.

Yani haiwezekani mtu uahidi utajenga madaraja,utajenga mashule,utajenga masoko.

Sasa haya si ndo wajibu hasa wa serikali wafanye hata kama hawakuahidi ?
Mzee namuelewa ila tu wengi hatuwezi kumuelewa vizuri.
Kwani unaweza kuahidi ambacho hakitafanwa na serikali?
 
Nimemsikia Mzee wa ubwabwa kumbe ana madini ya kutosha nilikuwa sijui nani nimpe kura ngoja nisikilize wagombea wengine ila nahisi nitampa huyu mzee.
Amezungumzia lishe sio ubwabwa kama wanavyoelewa watu wengi wanafunzi lazima wapate lishe bora ili wafanye vizuri, watu wapate lishe bora ili wafanye kaxi nafikiri ni mgombea pekee anayezungumzia kitu kinachoeleweka
 
Back
Top Bottom