wakuu salam....
Katika mikutano yake ya kampen mgombea wa ccm John magufuli ameonekana akinyenyekea kwa huzun na huruma kuomba kura.
Mgombea huyu alipo kuwa tanga alionekana anaomba kura kwa huruma mpaka watu wakawa wanamshangaa.
Ilifikia wakat watu tuliokaa huku nyuma tukawa tunacheka.
Hii inaonesha ni jinsi gani maguful alivyoona mambo si mazuri tena, hasa mwitikio wa wananchi katika kampen zake.
CCM kwa sasa ishakata tamaa kutokana na mwitikio wa wananchi kwa lowassa. Mbaya zaidi kinachowaumiza ni kwamba hata zile ngome zao hawana imani tena nazo kutokana na watu wengi kuitika vizur kwenye mikutano ya lowassa.
Juzi walipo kuja tanga, ililazimika kufanyia soko la tangamano tena siku ya soko ili ionekane watu wa sokon wamekuja kwenye mkutano, magar ya Ratco yalikodishwa kubeba watu pangan na vijijin ilimrad tuu uwanja ujae, lakini pamoja na yote hayo hakuweza hata kufua dafu kwa mkutano alioufanya Babu Duni.