Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Nimekuwa nikifuatilia kampeni za ndg magufuli lakini naishia kusikia...serkali ya magufuli...hii ni njia ya kujitofautisha na kundi la mafisadi wa ccm wanaompigia kampeni au ni ishara kwamba ataunda serikali ya mseto bila kuwajumuisha wanachama mafisadi wa ccm wanamsaidia katika kampeni zake?
 
Nnachokisikia kwenye kampeni za mwaka huu ni Lowassa!!!!!!
 
ni mesikia serikali ya magufuli naona ameshajikatia tamaa na kuwa na serikali ya Tanzania
 
John F. Kennedy’s inaugural address inspired children and adults to see the importance of civic action and public service. His historic words, “Ask not what your country can do for you – ask what you can do for your country,” challenged every American to contribute in some way to the public good. In this lesson, students learn about a theme in President Kennedy’s inaugural address, civic action, and consider how it applies to their own lives.

Thinkers will not vote for UKAWA.

20150828091952593_640_640_1_0.jpeg
 
Mi mwenyewe huwa nahisi ni mgombea mwenza wa mh. Rungwe
 

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Martin Mtonda (kushoto) na mgombea udiwani wa CCM.

MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.

Bi. Samia Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa wa Ruvuma yaani Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu ili kuchochea maendeleo ya wananchi.

Alisema kwa kuwa mkoa huo unazalisha mazao ya mahindi na kahawa serikali itahakikisha inaanzisha viwanda eneo hilo vya kusaga na kuandaa unga wa mahindi kwa wakulima na kuwawezesha ili wauze unga na kunufaika zaidi tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wamekuwa wakilanguliwa.

Alisema viwanda vingine ambavyo Serikali ya CCM itavianzisha ni pamoja na viwanda vya kubangua kahawa na kuiandaa kikamilifu tayari kwa kutumika, jambo ambalo alisema licha ya kuongeza thamani ya zao hilo itaongeza ajira kwa vijana na kuchochea uchumi wa wakulima eneo hilo.

Akizungumzia miundombinu ya barabara ambayo bado ni changamoto kwa mkoa huo hasa vijijini alisema serikali itakayoundwa na CCM chini ya uongozi wa Dk. John Pombe Magufuli pamoja na yeye watahakikisha wanajenga na kuboresha barabara za maeneo hayo ili ziweze kupitika kwa uhakika.

Hata hivyo kiongozi huyo amesema Serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 imejipanga kuboresha vizuri huduma za afya kuondoa ukiritimba na rushwa, elimu kwa kutoa elimu bure toka darasa la kwanza hadi kidato cha nne pamoja na ujenzi wa mabweni na uwezeshaji vijana na akinamama kiuchumi popote walipo mjini na vijijini.

Ziara ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza huyo wa urais tiketi ya CCM, inaendelea leo katika Mkoa wa Ruvuma na ataingia Jimbo la Tunduru kuendelea kuinadi ilaya ya chama hicho kuomba ridhaa kwa wananchi ili waweze kurejeshwa madarakani na kuunda dola.

Pichani juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.







Pichani juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.

Baadhi ya wananchi na wanaCCM wa Kijiji cha Maguu wilayani Mbinga wakimsubiri mgombea mwenza wa urais, CCM, Bi. Samia Suluhu.







Pichani juu ni baadhi ya pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zilizompokea mgombea mwenza wa CCM urais, Bi. Samia Suluhu mara baada ya kuingia Wilaya ya Mbinga zikiwa zimeegeshwa pembeni huku mkutano wa hadhara ukiendelea.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya mgombea mwenza, Bi. Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi (hawapo pichani) katika Kijiji cha Maguu, Wilaya ya Mbinga.

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (kulia) akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, kabla ya kuanza kuhutubia katika mikutano wake wa kampeni.

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM ambao ni wenyeji wake mkoa wa Ruvuma.

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na mmoja wa vijana walemavu waliohudhuria mkutano wake wa hadhara Kijiji cha Maguu. Bi. Suluhu alimsaidia fedha kijana huyo.

Imeandaliwa na Tanzania Habari
 
[h=2][/h]

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu akishuka kwenye ndege baada ya kuwasili Uwanja wa Ndeg e mjini Songea kuanza kampeni za CCM leo
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akipokea heshima ya Kijana wa chipukizi wa CCM, Baada ya kuvalishwa Skafu alipowasili Uwanja wa Ndege mjini Songea
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akisalimia baadhi ya viongozi baada ya kuwasili mjini Songea
​
Ngoma za burudani zikihanikiza kumpokea Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia alipowaili Uwanja wa Ndege Mjini Songea
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia akiwasalimia baadhi ya viongozi baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini Songea
​
Masafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM ukiwa njiani kwenda Kingerikiti mkoani Ruvuma kufanya mkutano wa kampeni
​
Masafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM ukiwa njiani kwenda Kingerikiti mkoani Ruvuma kufanya mkutano wa kampeni
​
Mama samia akiwasili Uwanja wa Mkutano wa hadhara uliofanyika Kingerikiti katika jimbo awilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma
​
Mama Samia akihutubia mkutano mdogo wa kampeni uliofanyika Kingerikiti wilayani Nyasa mkoani Ruvuma
​
Mama Samia akihutubia mkutano mdogo wa kampeni uliofanyika Kingerikiti wilayani Nyasa mkoani Ruvuma
​
Mama samia akimnadi mgombea Ubunge Injinia Stela Manyanya katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kingerikiti wilayani Nyasa mkoani Ruvuma
​
Waanchi wakishangilia katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kingerikiti wiayani Nyasa mkoani Ruvuma
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia baada ya kuwasili Kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kingerikiti wilayani Nyasa mkoani Ruvuma
​
Mama Samia akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika








































​









Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wakiri kuwa Mama Samia ni mchapa kazi​
 
[h=3]MAMA SAMIA APENYA HADI KATIKA MAJIMBO YA NAMTUMBO NA TUNDURU MKOANI RUVUMA[/h]

​
Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhus Hassan, akiwa umesimamishwa na wananchi katika eneo la Njenga, katika jimbo la Tunduru mkoani Ruvuma wakati ukiwa njiani kutoka Songea Mjini kwenda Nalasi jimbo la Tunduru Kusini mkoani Ruvuma leo.
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akizungumza na waanchi baada ya Msafara wake kusimamishwa na wananchi katika eneo la Njenga, katika jimbo la Tunduru mkoani Ruvuma wakati ukiwa njiani kutoka Songea Mjini kwenda Nalasi jimbo la Tunduru Kusini mkoani Ruvuma leo.
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samaia Suluhu Hassani akizungumza na kijana Lucas Luchinga, mwenye ulemavu aliyemkuta enoel la Njenga, Jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma,leo.
​
Mwananmke akimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia Suluhu, alipohutubia wananchi waliosimamisha msafara wake katika kata ya Nalasi jimbo la Tunduru mkoani Ruvuma leo
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika mkutano wa kampeni aliofanya eneo la Magazini, jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma leo
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika mkutano wa kampeni aliofanya eneo la Magazini, jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma leo
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika mkutano wa kampeni aliofanya eneo la Magazini, jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma leo
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi kwenye mkutano wa kampeni aliofanya leo, eneo la Magazini, Jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma
​
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Nalasi jimbo la Tunduru Kusini mkoani Ruvuma leo.
​
Mgombea Ubunge jimbo la Mbinga mjini, Sixtus Mapunda ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, akigutubia kwenye mkutano wa Mama Sania uliofanyika leo, eneo la Nalasi jimbo la Tunduru Kusini mkoani Ruvuma leo. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
 
[h=3]MAGUFULI AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI TANGA NA KUAHIDI KUTIMIZA KILA AHADI ALIYOAHIDI[/h]

​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mashewa wilayani Korogwe kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa serikali yake itakuwa ya kuchapa kazi kwa maendeleo ya wananchi na nchi kwa jumla.

​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi Diwani wa kata ya Mashewa wilayani Korogwe,Ndugu Seif Ahmed Hillal kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kata ya Magoma wakati akiwa njiani kuelekea Korogwe mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Kwamazandu,Korogwe vijijini kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Ndugu Stephen Ngonyani kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kwamazandu, Korogwe Vijijini.
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea wa nafasi za udiwani kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Kwamazandu,Korogwe vijijini.
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na mgombea ubunge jimbo la Korogwe mjini Mary Chatanda (katikati) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ndugu Abdalla Bulembo kwenye eneo la mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya chuo cha ualimu Korogwe.
​
Amon Mpanju akihutubia kwa niaba ya walemavu wa Korogwe kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya chuo cha ualimu Korogwe.
​
Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Yusuph Makamba akitoa salaam za utangulizi kabla ya Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufulikuhutubia wakazi wa Korogwe.
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi kwenye viwanja vya chuo cha ualimu Korogwe.
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubiawakazi wa Korogwe mjini ambapo alisema pamoja na mipango ya kuboresha maslahi ya walimu pia itaenda sambamba na kuwajengea nyumba za kuishi.
​
Wananchi wakishangilia hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Korogwe mjini Mary Chatanda Ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya chuo cha ualimu Korogwe.
​
Mgombea ubunge jimbo la Korogwe mjini akionyesha Ilani ya Uchaguzi juu
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanandi wagombea wa udiwani toka Korogwe mjini.
​
Wananchi wa Mombo wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
​
Wakazi wa Jimbo la Bumbuli wakifuatilia kwa makini mkutano wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
​

​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Bumbuli kwenye viwanja vya Togotwe ambapo aliwaahidi kuwajengea barabara ya lami pamoja na kufuatilia suala la kiwanda cha Chai cha Mponde.
​
Hivi ndivyo uwanja wa Togotwe ulivyo jaa.
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Bumbuli Ndugu Januaty Makamba kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.

​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi mbele ya mgombea wa ubunge jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba
​
Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akihutubia wananchi wa Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
​
Katibu Mkuu Mstaafu Ndugu Yusuph Makamba akihutia wakazi Lushoto kwenye uwanja wa Saba saba.
​
Lushoto ikiwa imefurika watu tayari kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
​
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Ummy Mwalimu akihutubia wakazi wa Lushoto kwenye uwanja sabasaba kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Lushoto kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jitegeme.
​
Wakazi wa Lushoto wakifurahia mkutano wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
​
Original Komedi wakionyesha sanaa yako kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Togotwa



​




 
lowassa ndio mgombea wa urais anayekubarika zaidi hata makomeo mwenyewe anajua!​
 
Back
Top Bottom