Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Toa upu mbavu wako hapa na ulofa,wapi kamuombea Mrema kura,Mrema ndo kamuombea kura Magufuli na si vinginevyo.

Na wewe siku ukiweka picha yako halisi watu wata log out, unaweka picha ya dem mkalii kumbe sio wewe
 
Nimesoma,aliwaambia wamchague Shirima,ndo first choice hiyo,then akasema incase hawamtaki Shirima basi MREMA.Ila wewe lofa story ulivyoileta ni kama vile Magufuli first choice yake ni MREMA

Mkiambiwa muweke akiba ya maneno mnajifanya wabishi. Umebishaaaa...eti ooh, wapi kasema hivyo. Angalia sasa umeumbuka na mitusi yako. Magamba mna shida sana.
 
Magufuli amechoka sana hata pumzi imekata leo kaongea kwa upole sana sauti imekata kabisa
 
Magufuli Amtosa Mgombea Ubunge wa CCM Vunjo....AMNADI Mrema








Katika hali isiyo ya kawaida, mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, amemmwagia sifa Mbunge wa Jimbo hilo, Augustine Mrema kwamba ni kiongozi mchapakazi mwenye rekodi nzuri ambaye alisimamia haki wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Mgombea huyo aliwaambia wakazi wa Vunjo, mkoani Kilimanjaro jana kuwa kama wakishindwa kabisa kumchagua mgombea wa CCM, Innocent Shirima, ni heri wampe kura zao Mrema kwani ana moyo mwema na amewafanyia mengi wananchi wa jimbo hilo.

Mrema anawania ubunge wa jimbo hilo kupitia Tanzania Labour Party (TLP).

Akizungumza na wakazi hao maeneo ya Himo, Dk. Magufuli alisema Mrema amekuwa mtetezi mkubwa wa wananchi wa jimbo hilo anapokuwa bungeni, tofauti na mgombea ubunge kupitia NCCR-Mageuzi anayeungwa mkono na Ukawa, James Mbatia.

"Mimi nampenda sana Mrema hata kama yuko chama kingine, maana ni mpambanaji, ana shukrani sana na ni msema kweli, mkiona shida kabisa kumchagua Shirima, basi bora mumpe Mrema na mimi huyu Innocent nitampa kazi nyingine," alisema na kuongeza:

"Mimi nitakuwa rais mvua inyeshe isinyeshe, kwa hiyo endapo mtamchagua mgombea wa CCM, Shirima mimi siwezi kumwacha Mrema hivi hivi, nitamteua, maana rais ana nafasi nyingi sana za uteuzi….. namheshimu sana Mrema na dhamira yangu itanisuta sana kama atashindwa ubunge na nisimteue."


"Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni, Shirima ndiye anawafaa hapa Vunjo, lakini mkishindwa kabisa kumchagua basi mpeni Mrema, maana amewasaidia sana," alisema Dk. Magufuli.

Dk. Magufuli asimamisha msafara kumsalimia Mrema wakati msafara wake (Magufuli) ukitokea Himo Vunjo kuelekea Mwanga kwenye mkutano mwingine.

Mrema wakati huo alikuwa amekaa njiani na wafanyabiashara wadogo wadogo jirani kabisa na mizani ya Himo ndipo msafara wa Magufuli ulimfuata eneo hilo.

Dk. Magufuli alimfuata Mrema na kumpa nafasi ya kuzungumza, ndipo alipowaambiwa wananchi hao kwammba wasifanye makosa kwani rais anayefaa ni Dk. John Magufuli.

Mrema alisema ujio wa mgombea huyo jimboni humo ni neema kwani Dk. Magufuli amekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Vunjo kwa kuwatengenezea barabara za lami.

Mrema aliorodhesha kilomita za lami za jimbo hilo ambazo zimejengwa kwa usimamizi wa Dk. Magufuli, hali iliyoibua shangwe na nderemo kutoka kwa wafanyabiashara wa eneo hilo wengi wao wakiwa wanawake.

Chama chake cha TLP kimesimamisha mgombea urais ambaye ni Maxmilian Lyimo.

Hii si mara ya kwanza kwa Mrema kumpigia debe mgombea urais wa CCM wakati chama chake kikiwa kimesimamisha mgombea.

Mwaka 2010 Mrema alikuwa akimpigia debe Rais Jakaya Kikwete ambaye wakati huo alikuwa akiwania muhula wa pili wa urais unaomalizika mwezi huu, ingawa chama chake kilimsimamisha mgombea urais, Mutamwega Mgahywa.



CHANZO: NIPASHE
 
Carbohydrate foods huongeza nguvu mwilini, na nguvu hizi huwezatumika katika mambo mbalimbali kama vile.....? Kufanyia mazoezi mbalimbali kama push ups! Enhee mwingine? Kucheza muziki jukwaani, enheee mwingine, kubeba mizigo kuweka kwenye ndege, enheee mwingine, kuongea sana, enheeee wa mwisho? Kufukuzia wanyama wakali kama vile fisi...safi kabisa wote mmepata...jipigieni makofi...*..*...m! Tenaaaa *...*...m!
Vizuri sana.
 
Mbona update ya leo bagamoyo haijawekwa..?
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la makufuri ni mtu mwenye kiburi harafu hashauriki na wakati mwingine huwa anajikoroga mwenyewe.
 
Toa upu mbavu wako hapa na ulofa,wapi kamuombea Mrema kura,Mrema ndo kamuombea kura Magufuli na si vinginevyo.

Wewe kanone, jingalao, mr chin na ubora mtakuwa dugu moja. Mna ubishi usiyo na maana!
 
Labda yeye haoni shida kuwa na serikali ya mseto,who knows.
 
Nimesoma,aliwaambia wamchague Shirima,ndo first choice hiyo,then akasema incase hawamtaki Shirima basi MREMA.Ila wewe lofa story ulivyoileta ni kama vile Magufuli first choice yake ni MREMA

Mara sijaona akimuombea kura Mrema, mara alisema wamchague Shirima kama first choice incase hawamtaki bas Mrema! Kwa kweli umekong'otwa!
 
Ni mtu asiyetabilika.Saa zingine anafanya mambo kwa kukurupuka bila tafakari ya kina.

Ndio maana tulikuwa tunalilia katiba mpya ya wananchi ili kuwabana viongozi wenye hulka ya kukurupuka ili waweke masilahi ya wananchi mbele na sio mawazo yao yanavyowatuma.
 
Wewe kibaraka wa fisadi,hivi tarehe 27 utarudi CCM ama?maana boss wako atakuwa statusless
Acha kujidhalilisha. Lowassa lazima awe Rais wa TANZANIA, narudia tena! Lazima awe Rais wa Tanzania! Hakuna namna nyingine tena! Watanzania wazalendo tumeshakubaliana kwa kauli moja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…